DOKEZO Karagwe: Watu wengi hawajaweza kuunganishiwa umeme kutokana na gharama ya kununua nguzo

DOKEZO Karagwe: Watu wengi hawajaweza kuunganishiwa umeme kutokana na gharama ya kununua nguzo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari, ndugu mteja.

Ndo maana tumesema kua nguzo ni mali ya TANESCO na hua gharama zikitozwa ni kutokana na huduma inayotelewa ya kumuunganishia mteja na huduma ya umeme.

Asante. ^HN.
Ninaomba sana huko vijijini kuna watu wanauziwa nguzo. Nenda Tarawa ya mashati kijiji cha Mahorosha, peleleza utaambiwa ulipitishwa mchango wa nguzo.
Habari, ndugu mteja.

Ndo maana tumesema kua nguzo ni mali ya TANESCO na hua gharama zikitozwa ni kutokana na huduma inayotelewa ya kumuunganishia mteja na huduma ya umeme.

Asante. ^HN.
Huko vijijini tena REA kuna wanaonunua nguzo. Fanya uchunguzi wilaya ya Rombo, tarafa ya mashati kijiji cha mahorosho, walichanga ili kununua nguzo. Ukanda wa chini mpakani na Kenya.
 
Kwa umbali wa mita 500 njia moja gharama imekaaje.?

kwa sehemu za vijijini (same). Mlisema mradi wa REA nafuu lakn nimefatilia naambiwa nguzo tano 1.5 Million apo bado gharama nyingine.

Ni sahihi ?
Habari JaxenDL, asante kwa kuwasiliana nasi,

Ni kweli gharama kwa mtazamo wa kawaida ni kubwa lakini kwa umbali wa mita hizo mpimaji akipita atakupa makadario.
Aidha, miradi ya REA ndani ya mita 30 gharama yake ni 27,000/

Pia ni muhimu kuelewa shirika linaendela na utekelezaji wa miradi ya kusogeza miundombinu kila mwaka ili kuhakikisha huduma inawafikia wananchi kwa urahisi.

Asante. ^GK
 
Okay. Shukrani kwa muongozo
 
Wakiunganisha hata kama ni mbali, baada ya mda ile faida inafidia nguzo! Nguzo ni BURE. Kuna wakati waziri mmoja aligusia hilo ila immediately akapewa "speed governer".
Pesa inayokatwa unaponunua umeme kwa ajili ya REA inatosha kabisa kununua nguzo, kazi yao ni kuweka umeme kwa 27000 na si vingenevyo.
 
Kwa umbali wa mita 500 njia moja gharama imekaaje.?

kwa sehemu za vijijini (same). Mlisema mradi wa REA nafuu lakn nimefatilia naambiwa nguzo tano 1.5 Million apo bado gharama nyingine.

Ni sahihi ?
Habari ndugu mteja,

Asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022.
•Gharama za kuunganisha umeme ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
•Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
•Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
•Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
•Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
•Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/=
Gharama hizi ni kama ilivyoelekezwa na EWURA. ^RS
 
Pesa inayokatwa unaponunua umeme kwa ajili ya REA inatosha kabisa kununua nguzo, kazi yao ni kuweka umeme kwa 27000 na si vingenevyo.
Habari, ndugu mteja. Asante kwa kuwasiliana nasi.

Tafadhali fahamu kuwa nguzo ni mali ya TANESCO na haziuzwi kwa mteja. Mteja hulipia gharama ya kuunganishiwa huduma ya umeme kulingana na taratibu na makadirio husika.

Aidha, katika maeneo ya vijijini, huduma ya kuunganishiwa umeme inaweza kutolewa kwa gharama yenye ruzuku, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuleta unafuu katika kupata huduma za umeme.

Asante. ^RS
 
TANESCO yenye tija kwa Wananchi ni ile ya Wazi Medard Matogolo Kalemani. Hii ya sasa siiamini
Habari, ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu. Tumepokea ujumbe wako.

Tafadhali tufahamishe endapo kuna changamoto umepata juu ya huduma zetu kwa msaada zaidi.^NI
 
Back
Top Bottom