Mpwayungu Village
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 14,540
- 30,875
KARANI WA SENSA APORWA KISHIKWAMBI USIKU, MUMEWE AJERUHIWA
KARANI wa Sensa ya Watu na Makazi Jiji la Arusha, Sarapia Kiwango ameporwa kishikwambi chake wakati akijiandaa kwenda kuhesabu makundi maalum jana usiku huku mume wake akijeruhiwa.
Akizungumza na mwandishi wa HabariLEO, Mratibu wa sensa ya watu na makazi katika Jiji la Arusha, Maneno Maziku amesema Kiwango aliporwa kishikwambi usiku wakati akienda kuhesabu makundi maalum huku mume wake akijeruhiwa kichwani.
Amesema baada ya tukio hilo Karani huyo alipewa kishikwambi kingine na anaendelea na kazi. "Ni kweli aliporwa kishikwambi na mume wake kujeruhiwa kichwani lakini ameshapewa kishikwambi kingine anaendelea na kazi lakini pia majeruhi hali yake inaendelea vizuri,” amesema Maziku.
Chanzo: Habarileo