Karani wa sensa aporwa kishikwambi Arusha Ungalimited

Karani wa sensa aporwa kishikwambi Arusha Ungalimited

Karani wa Sensa ya Watu na makazi Jiji la Arusha, Sarapia Kiwango, ameporwa kishikwambi chake, wakati akijiandaa kwenda kuhesabu makundi maalum, usiku wa kuamkia leo, huku mumewe akijeruhiwa.

IMG-20220823-WA0022.jpg

Akizungumza Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi katika Jiji la Arusha, Maneno Maziku, amesema, karani Kiwango aliporwa kishikwamb hicho na kwamba alipatiwa kingine kuendelea a kazi.

“Ni kweli aliporwa kishikwambi, huku mume wake akijeruhiwa kichwani, lakini ameshapewa kishikwambi kingine anaendelea na kazi, pia majeruhi hali yake inaendelea vizuri” amesema.

Naye Diwani wa Kata ya Unga Limited, Mahamod Said na Mtendaji wa Kata hiyo, Sophia Laizer walizungumzia tukio hilo kwa nyakati tofauti na kusema alivamiwa na watu waliokuwa a bodaboda.

“Jana usiku hawa makarani wa sensa waliitwa kwa mtendaji, wakati wanakwenda huko, ndiyo akakutana na vibaka waliokuwa kwenye bodaboda wakamjeruhi mumewe na kumpora kishikwambi, kisha kutoweka kusikojilikana,” amesema diwani huyo.

Machalii ya ngalimi sio watu wazuri.
 
Ameona uvivu kuhesabu watu

Tayari Tozo yangu iliyonunua I Pad imepigwa

Karani, Karani, Karani, Nakuita tena Karani wa Sensa mbona umejigawia tozo bila utaratibu wa kibajeti kwa kukimbia na I Pad ya serikali

Sio mambo ya kuchekesha ni staili mpya ya vijana kupiga Mali za serikali baada ya kukaa kitaa kwa muda mrefu

Hao ndio vijana wanaoitwa Dot. com

Kuna Dada mmoja alipita kitaa kunihesabu yaani ni mzito balaa, Nikamuuliza tangu asubuhi umepita nyumba tatu tu na yangu ni ya nne, Ulicheck muda saa tano asubuhi, Bado nyumba zaidi ya ishirini

Ameamua kujigawia mapema I Pad baada ya kuona hana uwezo wa kuhesabu watu kwa kuuliza maswali mia moja kila mtu

Hao ndio Graduate waliopo kitaa, Ukizubaa tu umepigwa

Kijana amefikiria idadi ya maswali atakayouliza watu na muda atakaotumia akaona bora ajigawie I Pad ya serikali kama malipo

Kwa staili hata wakijua idadi ya watu kuna Maendeleo yatapatikana kweli, siku ya kwanza tu I Pad imepigwa na Karani Sasa hiyo keki ya Taifa si itaishia huko huko juu
 
Ipad hizo zimetolewa msaada na wasouth Korea mzee

Ova
 
Barabara ya Unga ltd nimeishia tu NSK hosp.. huko uswazini kwa waporaji sipajui 😂

Sakina sijawahi porwa., Njiro nikija ibiwa/ porwa ndio nitaona Arusha ni hovyo.. but for now Arusha is my second home 😍
Jina tu lenyewe linatishia amani😄

2nd? 1st ni Mo au?
 
Back
Top Bottom