Ameona uvivu kuhesabu watu
Tayari Tozo yangu iliyonunua I Pad imepigwa
Karani, Karani, Karani, Nakuita tena Karani wa Sensa mbona umejigawia tozo bila utaratibu wa kibajeti kwa kukimbia na I Pad ya serikali
Sio mambo ya kuchekesha ni staili mpya ya vijana kupiga Mali za serikali baada ya kukaa kitaa kwa muda mrefu
Hao ndio vijana wanaoitwa Dot. com
Kuna Dada mmoja alipita kitaa kunihesabu yaani ni mzito balaa, Nikamuuliza tangu asubuhi umepita nyumba tatu tu na yangu ni ya nne, Ulicheck muda saa tano asubuhi, Bado nyumba zaidi ya ishirini
Ameamua kujigawia mapema I Pad baada ya kuona hana uwezo wa kuhesabu watu kwa kuuliza maswali mia moja kila mtu
Hao ndio Graduate waliopo kitaa, Ukizubaa tu umepigwa
Kijana amefikiria idadi ya maswali atakayouliza watu na muda atakaotumia akaona bora ajigawie I Pad ya serikali kama malipo
Kwa staili hata wakijua idadi ya watu kuna Maendeleo yatapatikana kweli, siku ya kwanza tu I Pad imepigwa na Karani Sasa hiyo keki ya Taifa si itaishia huko huko juu