Karani wa sensa aporwa kishikwambi Arusha Ungalimited

Karani wa sensa aporwa kishikwambi Arusha Ungalimited

Hizi products ni latest hivyo sina shaka zina mfumo wa kuzi track....hao/huyo Kibaka akamatwe atiwe adabu.
 
😀😀😀unga limited kuna siku nilipita mchana kuna nyumba zimechoka balaa na watu wamechoka balaa kwa pombe na madawa , wamejianika nje ya kila nyumba jichanganye uulize njia😀😀umeyakanyaga
Mmoja wa uliowaona ni mimi. Hapa mitaa ya Engosheraton
 
Ipoje hiyo mkuu maana kuna lisimu hapa ungalimi nimeuziwa elf 15 ila ni li smartphone likubwa jipyajipya halifanani na hiyo bei au ndo nimeshaingia kwenye 18 za chief hengaya
Mamaee ukidakwa umeumia
 
KARANI WA SENSA APORWA KISHIKWAMBI USIKU, MUMEWE AJERUHIWA

KARANI wa Sensa ya Watu na Makazi Jiji la Arusha, Sarapia Kiwango ameporwa kishikwambi chake wakati akijiandaa kwenda kuhesabu makundi maalum jana usiku huku mume wake akijeruhiwa.

Akizungumza na mwandishi wa HabariLEO, Mratibu wa sensa ya watu na makazi katika Jiji la Arusha, Maneno Maziku amesema Kiwango aliporwa kishikwambi usiku wakati akienda kuhesabu makundi maalum huku mume wake akijeruhiwa kichwani.

Amesema baada ya tukio hilo Karani huyo alipewa kishikwambi kingine na anaendelea na kazi. "Ni kweli aliporwa kishikwambi na mume wake kujeruhiwa kichwani lakini ameshapewa kishikwambi kingine anaendelea na kazi lakini pia majeruhi hali yake inaendelea vizuri,” amesema Maziku.

Chanzo: Habarileo

View attachment 2332504
Nyie hii nchi watu hawapendi maendeleo
 
Mtu kachoka zake unaanza kumuuliza maswali ya kiwaki, au unaenda kwa wahuni kuwahesabu wameshalewa na wengine mateja unategemea nini[emoji3][emoji3]karani kama wa kike anaweza ata kubakwa
Mkuu rodilofa ulipata kazi, Kuna bar wanahitaji muuza vinywaji unakuwa kaunta
 
Mtu kachoka zake unaanza kumuuliza maswali ya kiwaki, au unaenda kwa wahuni kuwahesabu wameshalewa na wengine mateja unategemea nini😀😀karani kama wa kike anaweza ata kubakwa
Hiyo mibangi, ugoro, gongo na gundi wanapata wap nguvu You kubaka aiseee.
 
Back
Top Bottom