Karani wa sensa aporwa kishikwambi Arusha Ungalimited

Karani wa sensa aporwa kishikwambi Arusha Ungalimited

Hiyo unga ltd wanaleana sana, sehemu zingine Arusha ujinga huu umekomeshwa

Huko unga limited kuna nyumba nyingi za kupanga za bei ndogo, mazingira kama hayo huchangia vijana wengi kuishi kwenye chumba kimoja na kupanga uhalifu.

Hao vijana wanaopora kwa kutumia boda boda hujulikana kwa jina maarufu la "tatu mzuka" Ni kundi hatari sana na linazidi kupata nguvu. Lisipodhibitiwa mapema litazidi kukua na likipata nguvu itakuwa vigumu kulidhibiti. Mchelea mwana kulia ...
 
Ameona uvivu kuhesabu watu

Tayari Tozo yangu iliyonunua I Pad imepigwa

Karani, Karani, Karani, Nakuita tena Karani wa Sensa mbona umejigawia tozo bila utaratibu wa kibajeti kwa kukimbia na I Pad ya serikali

Sio mambo ya kuchekesha ni staili mpya ya vijana kupiga Mali za serikali baada ya kukaa kitaa kwa muda mrefu

Hao ndio vijana wanaoitwa Dot. com

Kuna Dada mmoja alipita kitaa kunihesabu yaani ni mzito balaa, Nikamuuliza tangu asubuhi umepita nyumba tatu tu na yangu ni ya nne, Ulicheck muda saa tano asubuhi, Bado nyumba zaidi ya ishirini

Ameamua kujigawia mapema I Pad baada ya kuona hana uwezo wa kuhesabu watu kwa kuuliza maswali mia moja kila mtu

Hao ndio Graduate waliopo kitaa, Ukizubaa tu umepigwa

Kijana amefikiria idadi ya maswali atakayouliza watu na muda atakaotumia akaona bora ajigawie I Pad ya serikali kama malipo

Kwa staili hata wakijua idadi ya watu kuna Maendeleo yatapatikana kweli, siku ya kwanza tu I Pad imepigwa na Karani Sasa hiyo keki ya Taifa si itaishia huko huko juu
Hahaha
 
ningeshangaa zoezi liishe hv hv bila mtu kuporwa....si kwa arsh hii
Itakuwa na nyingine wanafanya siri, ila kuna baadhi ya sehemu mgambo walimwagwa wengi tu. Huko ungalimtd, ngarenaro na sehemu nyingine za hatari
 
Barabara ya Unga ltd nimeishia tu NSK hosp.. huko uswazini kwa waporaji sipajui 😂

Sakina sijawahi porwa., Njiro nikija ibiwa/ porwa ndio nitaona Arusha ni hovyo.. but for now Arusha is my second home 😍
Sakina na Njiro sio rahisi kuporwa.
Tatizo unga ltd Kuna chochoro nyingi haswaa mtu akipiga hatua tano hamumpati.
 
Back
Top Bottom