mathsjery
JF-Expert Member
- Sep 26, 2015
- 2,249
- 1,813
======
MAGO, Amechangia hii mada na kusema;
Nimeona clips kadhaa za wasanii wa Wasafii eti wako kwenye isolation (kalantin) kwa sababu za mwenzao Salam kukutwa na maambukizi baada ya kuwa safari ya pamoja katika nchi za ulaya.
Makosa ambayo yanafanywa na wasanii na bila kupewa muongozo wa watu wa afya wa namna/maana ya quarantine.
Kwanza katika kipindi hiki cha kuwa in isolation hupaswi kuwa na any form of physical contact na watu ama vitu ambavyo vitatumiwa ama kuguswa na wengine, kifupi unakuwa katika mahala pa peke yako.
Hii ni kwa sababu katika kipindi hiki unaweza kuwa umeambukizwa ila symptoms ama vipimo visionyeshe maambukizi. Ni kipindi cha tahadhari dhidi ya kuambukiza wengine na pia kuona preliminarily kama utapata any symptom related to COVID.
Sasa hawa jamaa kukaa katika one house kukiwa na all forms of physical contacts baina yao ama na vitu ambavyo huguswa na wenzako inaondoa maana nzima ya karantini?? Why
Endapo kuna mmoja tu miongoni mwao alikuwa ameambukizwa na subject 1 ambaye ni Salam basi na wengine wote wanaweza kuwa katika risk ya kuambukizwa humo walikolundikana.
Hivyo basi ilipaswa kila mmoja awe katika chumba chake kwa kipindi chote cha siku 14 ili kutimiza matakwa ya quarantine.
Sent using Jamii Forums mobile app