Karatu: CCM yakata Tamaa, yakubali kuachia Jimbo, Chopa ya Chadema yatikisa

Karatu: CCM yakata Tamaa, yakubali kuachia Jimbo, Chopa ya Chadema yatikisa

Makubaliano ya kuachia Jimbo yamefikiwa leo baada ya Chadema kuvurumisha mikutano ya hadhara isiyo na idadi (Tunatafuta calculator isaidie kujumlisha), ambayo wananchi wameielewa kabisa, Hakika kisicho ridhiki hakiliki!

Lissu ametoa Elimu ya Haki kwa Raia na kwamba hawapaswi kutishwa na yeyote , huku Mbowe akiwajaza wananchi Ujasiri wa kupinga ccm kwa sababu ndio Chanzo kikuu cha dhiki, Umasikini na Maisha Magumu, kitu ambacho Vitabu vya Mungu vinatafsiri kama dhambi kuu iliyojaa laana.

Ikumbukwe kwamba Hakuna Masikini atakayeuona Ufalme wa Mbingu

Zaidi jionee kidogo.

Pia Soma:
- Kuelekea 2025 - Mbowe: Siwezi gombana na Lema, mama yake atanipigia Simu

View attachment 3023234View attachment 3023235View attachment 3023236View attachment 3023239View attachment 3023240View attachment 3023497
Ma Hawa wa ccm walisema cdm imehawanyika
 
Hatuandiki jf ili kushindana na mtu, wala hatujawahi kuwaza mashindano, lengo letu ni kusambaza habari njema kwa watu wote, ni bahati mbaya kwamba tunatafsiriwa tofauti, bali tunakubaliana na kila tafsiri inayoletwa maana ndio uhuru wa JF huo
Huenda, na inaelekea hukuelewa ujumbe wangu nilionuia kuuwasilisha. "...kusambaza habari njema..." ni kwa faida ya wote, ni jambo jema. Ni aina ya "usambazaji", kama kipengele hicho nilicho nyanyua...
Habari njema inapotea kwenye mambo ambayo yanaongezwa kwenye usambazaji huo na kuifanya hiyo habari kupoteza uzuri wake. Ni staili tu, ya uwasilishaji, ndiyo naona imebadilika sana nyakati hizi.

Haya ni maoni tu, kwa uande wangu. Kama hiyo staili ya uwasilishaji ndiyo inayofanya wasomaji waelewe zaidi habari inayowasilishwa, mimi sina neno wala uwezo wa kubadili chochote.. Ilikuwa ni ushauri tu!

Kila njia inayoonekana inafaa kuing'oa CCM, itumike, hilo ndilo lengo. Haya mengine ni madoido tu.
 
Back
Top Bottom