Madikteta wote duniani waliegemea kwa wanyonge. Na wana sababu za kufanya hivyo. Hao wanaoitwa wanyonge, wengi wao hawawezi kuhoji matendo yao mabaya. Hao wanaoitwa wanyonge, wengi wao hawana elimu wala uelewa. Hao wanaoitwa wanyonge, wengi wao huwa wapo tayari kuutumikia unafiki ili mradi tu wapate kula.
Ukiona kiongozi yeyote anatamka kuwa yeye ni kiongozi wa wanyonge, uwe makini. Wengi wao huwa watu wa hila, hulitumia kundi hilo kuficha uovu wao na kutafuta sifa ya kuonekana watu wenye huruma.
Mugabe mambo yalipomwendea vibaya alienda kwa wanyonge, akawafunika akili zao kwa kaniki kwa kunyang'anya mashamba wazungu na kuwagawia wanyonge (leo wanatafuta wawekezaji kwenye mashamba yale yale). Amin alipoingia madarakani, alitamka anataka kuwainua wanyonge, mpaka wakambeba na kumtembeza mitaani kuwa wamepata Rais wa wanyonge. Ndivyo alivyofanya Bokasa, Nguema, na wengine wengi.