Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

Kanisa Katoliki DRC iliukataa udikteta wa kabila, Kanisa Katoliki huku TZ inatetea Udikteta. Mimi ndio maana Jumamosi huwa nanywea hela zote nilizonazo ili Asubuhi ya Jumapili niamke sina sadaka.
Hata viongozi Wa dini Wa Kenya awafungamani na wanasiasa wanaokiuka haki za watu awampambi mtu hawana unafiki blue uita blue.Sababu mfumo wao Wa maisha hauamuliwi na mwanasiasa.Kanisa katoliki Congo limechangia pa kubwa kumfurusha dikteta kabila aliyetaka kuzidi kukaa madarakani kwa kutokuheshimu katiba na makubaliano ya wakongomani.
 
Kumfananisha magufuli na dikteta Mussolini na Hitler yupo sahihi kabisa ndivyo alivyo hao walikua wauaji wakuu na wakati huo wakiungwa mkono na katoliki.
 
Pengo anasema dikteta hawezi toa huduma bure, tumkumbushe Hitler alitoa sana huduma bure kwa Wajerumani na wakati wote alisema yuko kwa ajili ya wanyonge wa Ujerumani.

Pamoja na kutoa huduma bure nadhani dunia haitamsahau kamwe vizazi na vizazi.

Suala la kutoa huduma bure sio kigezo cha mtu kutokuwa dikteta, Wakina Stalini wote walitoa service bure ila wanajulikana walivyokuwa.

NS-Volkswohlfahrt.svg.jpeg
 
Hana hasara ashamaliza dunia yuko saa 10 jioni.Asikitikii kizazi kilichobaki.Amelelewa ktk mfumo wa udikteta wa kanisa ambapo muumini uruhusiwi kuhoji juu ya mafundisho yeyeto ya kanisa zaidi ya kuyapokea.
... kumi jioni!, do you know your time?, chunga kijana..
 
Naunga mkono hoja

P

Naamini hii kauli yako ina maana nyingine ndugu paskali
 
Sina maneno mengi
 
Ametumia Uhuru wake wa kutoa maoni, ila akumbuke kuna watu wanazuiwa kutoa maoni kisa tu hayawafurahishi watawala

Pengo na ww ujitafakari katika hili
Jino kwa jino
 
Pengo ni binadamu Kama walivyo binadamu wengine tu, hvyo niaki yake kutowa maoni yake na kuonyesha mapenzi yake kwa kile anacho kiamini.
 
,HAMNA MTU ALOUMIA SANA KWA SPEECH HII KAMA JPM ...JPM hatolala usingizi mtamu tena, angelala kama Askofi angejaribu kuunga mkono kama alivyofanya Benjamini.


Kwa lugha nyepesi nikwamba, JPM atakapomaliza muda wake iwe ni 2020 au 2025 atalazimika kuheshimu Katiba na kuachia ngazi ili wengine waongoze !!

JPM na Benjamini kama nawaona!!
 
Back
Top Bottom