Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

Kwa njaa hii uliyonayo tukija jumapili najua tutakuta umekula sakramenti zote peke yako
Kila mbuzi hula kwa kadri ya urefu wa kamba yake, makasisi, wachungaji na wahubiri, hula vya madhabahuni, jambo tunahimizwa kumtolea Mungu sadaka, unadhani hizo fedha wanampelekea Mungu kule mbinguni?.
Na wao wanaishi kwa mana kutoka mbinguni?.
P
 
Hitler aliuwa raia wema milioni 43 ikiwemo wayaudi milioni 6.Inaonekana Pengo anapenda mauaji ya raia wema.Huenda pia Pengo ni shabiki wa Idi Amini sababu alinunua ndege 63.
Hitler walimtengeneza wao kwa sababu za kidini kujaribu kuwafutilia mbali wayahudi


Mussolini ndio aliwarudishia mamlaka yao ya kidini na kiserikali nakuwapa mji wa Vatican kua kama Nchi makao Makuu ya Rumi .. Ukumbuke baada ya Napoleon kumakamata papa nakumuua mwaka wa 1798. Rumi ya kiserikal ilochangamana na udini haikuweko tena.. Mpaka 1900+++ mwaka fulan ambao Mussolini wakasaini mikataba na Rumi..... So hapa lazima wamuenzi Mussolini ambaye ni DIKITETA.
 
Eeh Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi nakuomba utende lililo jema na linafaa juu ya huyu kiongozi wa dini aliyegeuka na kuwa mwasiasa. Amen.
 
"Viongozi wahubiri amani na mshikamano, kama hawawezi basi waendelee kuhubiri dini na mambo mengine. Tayari kuna watu wanaamini Kanisa haliwezi kukemea serikali inapofanya hujuma kwa wapinzani kisa Rais ni mkatoliki"
 
Maneno yake mwenyewe na sio
Msimamo wa kanisa katoliki. Akae kimya kama
Papa Benedict
 
Benito Amilcare Andrea Mussolini alizaliwa mwaka 1883 na kufariki mwaka 1945. Mwanzoni alikuwa ni mwanamapinduzi ya kijamaa.

Nchi ya Italia ilipoingia kwenye mgogoro wa kisiasa mwaka 1922, Mussolini alisema yeye pekee ndiyo anaweza kutuliza mgogoro huo, na akapewa mamlaka hayo kama Waziri Mkuu.

Taratibu Mussolini alivunja Taasisi zote za kiutawala na kidemokrasia. Kufika mwaka 1925, akawa dikteta kamili maarufu kwa jina la "Il Duce" ("Kiongozi").

Alikuwa na falsafa yake iliyosema " Il Duce ha sempre ragione (Mussolini was always right).

Athari za ufashisti wa Mussolini kwa nchi ya Italia zilikuwa;

1.Baada ya kuwa Waziri Mkuu, Mussolini alipunguza ushawishi wa Mahakama

2.Akapandikiza vyombo vya habari mamluki

3. Alikamata wapinzani wa kisiasa na kuwafunga jela

3. Aliendelea kufanya kazi ndani ya mfumo wa bunge angalau kidogo hadi Januari 1925, wakati alipojitangaza kuwa Dikteta wa Italia

4. Kufuatia mfululizo wa majaribio ya mapinduzi mnamo 1925 na 1926, Mussolini alizidi kushikilia msimamo wake, na kupiga marufuku vyama vya upinzaji

5. Aliwafuta wabunge zaidi ya 100, na kurudisha adhabu ya kifo kwa wapinzani wa kisiasa

6. Kusitishasha uchaguzi wa serikali za mitaa.

7. Wakati wa vita II ya dunia Mussolini alikuwa upande wa Nazi akimuunga mkono Hitler wa Ujerumani.

Kutokana na falsafa yake ya "Mussolini was always right' nchi ya Italia iliathirika sana kiuchumi kiasi kwamba maisha ya wananchi yalikuwa magumu sana.

Tarehe 28 April 1945 Mussolini na mkewe walishikwa karibu na mpaka wa Switzerland wakijaribu kutoroka kwa kuvaa mavazi kama askari wa Nazi.

Lakini wananchi waliwatambua wakawashika na kuwaweka yeye na mkewe kwenye Jiwe maalum na wakapigwa risasi (firing squad) kwenye mji wa Giulino Azaro kisha miili yao ikawekwa Milan na watu wakaipiga mawe.
 
Mzee Wetu Pengo amezeeka sasa anaanza kuharibu. Na hata waliomualika leo wamemualika kimkakati ili aongee aliyoyaongea.

Wanajua fika kuwa mzee hana mamlaka sasa Katika kanis la Jimbo Kuu la Dar, wenye mamlaka wapo na hawakualikwa. Ila waliamua wamualike yeye na wammezeshe maneno ya kusema.

Mapadre wengi wanaumizwa na yanayoendelea nchini kwa sasa. Wanaamua kukaa kimya kulinda kiapo cha Utii walichoapa mbele ya Mungu na kanisa kuwa watamtii askofu wa kanisa mahalia.

Hata hivyo, mashirika ya Kijasusi ndan ya kanisa inabidi yafanye kazi yao kuwamonitor wazee wa aina ya Pengo.
 
Pengo ni Mtumishi wa Mungu huwa hana unafiki

Ni hatari sana tunatengeneza hii, watumishi wa Mungu hawapaswi kuonesha wazi wazi wapo mrengo gani wa kisiasa, Coz kinachofuata ni viongozi wa dini wa upande wa upinzani nao watakuja na kongamano lao, then waumini nao wataanza kujigawa kutokana na vyama vyao
 
"...Bwana tumewaona watumishi wako wakila na wanyang'anyi..."

Haka kamstari kama naanza kukaelewa elewa hv
 
Back
Top Bottom