Benito Amilcare Andrea Mussolini alizaliwa mwaka 1883 na kufariki mwaka 1945. Mwanzoni alikuwa ni mwanamapinduzi ya kijamaa.
Nchi ya Italia ilipoingia kwenye mgogoro wa kisiasa mwaka 1922, Mussolini alisema yeye pekee ndiyo anaweza kutuliza mgogoro huo, na akapewa mamlaka hayo kama Waziri Mkuu.
Taratibu Mussolini alivunja Taasisi zote za kiutawala na kidemokrasia. Kufika mwaka 1925, akawa dikteta kamili maarufu kwa jina la "Il Duce" ("Kiongozi").
Alikuwa na falsafa yake iliyosema " Il Duce ha sempre ragione (Mussolini was always right).
Athari za ufashisti wa Mussolini kwa nchi ya Italia zilikuwa;
1.Baada ya kuwa Waziri Mkuu, Mussolini alipunguza ushawishi wa Mahakama
2.Akapandikiza vyombo vya habari mamluki
3. Alikamata wapinzani wa kisiasa na kuwafunga jela
3. Aliendelea kufanya kazi ndani ya mfumo wa bunge angalau kidogo hadi Januari 1925, wakati alipojitangaza kuwa Dikteta wa Italia
4. Kufuatia mfululizo wa majaribio ya mapinduzi mnamo 1925 na 1926, Mussolini alizidi kushikilia msimamo wake, na kupiga marufuku vyama vya upinzaji
5. Aliwafuta wabunge zaidi ya 100, na kurudisha adhabu ya kifo kwa wapinzani wa kisiasa
6. Kusitishasha uchaguzi wa serikali za mitaa.
7. Wakati wa vita II ya dunia Mussolini alikuwa upande wa Nazi akimuunga mkono Hitler wa Ujerumani.
Kutokana na falsafa yake ya "Mussolini was always right' nchi ya Italia iliathirika sana kiuchumi kiasi kwamba maisha ya wananchi yalikuwa magumu sana.
Tarehe 28 April 1945 Mussolini na mkewe walishikwa karibu na mpaka wa Switzerland wakijaribu kutoroka kwa kuvaa mavazi kama askari wa Nazi.
Lakini wananchi waliwatambua wakawashika na kuwaweka yeye na mkewe kwenye Jiwe maalum na wakapigwa risasi (firing squad) kwenye mji wa Giulino Azaro kisha miili yao ikawekwa Milan na watu wakaipiga mawe.