Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

GUSSIE,
Anapoelekea huyu Jamaa ni kuanza kuorodhesha hospitali, shule pamoja na vyote ambavyo vilijengwa na wazungu miaka kabla ya uhuru na kuuliza huu ndio ukoloni....Tumsamehe Bure tu
 
Inaonyesha Kardinali Pengo hajawahi kusikia ule msemo wa panya "panya anakutafuna huku anakupuliza". Pia labda hajawahi kumsikia Gaddafi na namna alivyokuwa akiwatunza wananchi wake wote kwa huduma nzuri sana toka elimu, matibabu, social care, kazi na malazi lakini bado alikuwa akiongoza nchi ya Libya kwa udikteta. Sisemi kuwa Rais wetu ni ditekta ila kujenga barabara, kutoa elimu bure na kujenga hospitali sio ishara kuwa rais wa nchi si dikteta.
 
"Huyu Pengo sijui kala maharage ya wapi?"
Gwajima
 
Ndio maana ya tofauti ya mtizamo
Kwako logic kwa wengine maharage and vice versa,tulia tu na kufanya mambo mengine.
Mambo mengine nayofanya ni hili la kumbagaza yeyote anayewalisha watu maharagwe yaliyochacha baada ya yeye kuvimbiwa
 
Kumfananisha magufuli na dikteta Mussolini na Hitler yupo sahihi kabisa ndivyo alivyo hao walikua wauaji wakuu na wakati huo wakiungwa mkono na katoliki.
Kanisa katoliki lina historia kubwa sana ya kuunga mkono mabeberu na madicteta, anza na hitler, musollini, franco wa spain, pinochet wa argentina na wengi we gineo, ukiwasikiliza roma umekuwa mtumwa, na usithubuthu kuwaachia watoto wako wa kiume
 
Huyu Pengo akapumzike tu. Ni askofu wangu siwezi kunvunjia heshima lakini AKAPUMZIKE
 
Pengo huyuhuyu aliyeandika vitabu vya kuwafundisha watu namna ya kuwapata viongozi kabla ya uchaguzi wa 2009, JK akamvumilia na kukaa kimya, kipindi cha utawala wa awamu ya nne alikuwa anaongoza kutoa matamko yaliyokuwa yanapinga matendo ya watawala, mi nahisi mzee akapumzike aache kuonesha kaupendeleo fulani.
 
Binafsi siamini kuwa yaliyoandikwa na mleta uzi ndiyo yaliyotamkwa na Askofu mkuu mstaafu. Kama Askofu mkuu mstaafu Kardinali Policarp Pengo katamka kuwa Musolini na Hitler wanaonewa kwa kusemwa kwa mabaya tu, basi ni heri kusema kapotoka. La sivyo, atoe ufafanuzi wa kina kwa kauli hiyo.
Kakengeuka. Kilangila.
 
Kizazi kisichopenda ukweli kitakosoa mpaka Viongozi wateule. Dini inatawaliwa na dhana ya IMANI kama huwezi amini katika Maono ya Viongozi wako wa Kidini huna Imani. Ya Kardinali Pengo tuachieni walengwa yatuwashe maaana ndiye mhimili wetu wa Imani na kwa mujibu wa mafundisho kauli za Kidini hazihitaji too much Reason mwishowe Utakufuru.
Baba Pengo tunasema AMINA.
Lakini kumbuka tu jambo moja kwamba hata hao viongozi wa dini ni binadamu tu kama mimi na wewe na wana mapungufu yao mengi tu!
 
@GUSSIE,l Pengo
Pengo ni wa ajabu kama leo anaweza kuhalalisha udikteta wa Mussolini na Hitler kwa sababu ya mazuri waliyofanya.

Ni sawa ni kumsifia mtu aliyekuja nyumbani kwako akabaka mke au binti yako kisha anapotoka akafunga mlango. Unamsifia eti mbakaji pamoja na kubaka mke wako, alikuwa ni mtu mzuri kwa vile alifunga mlango.
 
Nenda Uganda uwaambie Waganda eti Idd Amin Dadah alikuwa dikteta uone kama utapata maji ya kunywa au sehemu ya kulala.
 
Huyu hata kumwita Kadinali haifai kabisa, tulishamzoea na chuki zake dhidi ya Rais Kikwete na utawala wake, leo hii kazi yake kubwa ni kujipendekeza na kulamba miguu.
 
Pengo ni Mtumishi wa Mungu huwa hana unafiki
Kama si unafiki basi ni upofu wa kutoona maovu yanatendeka kwenye jamii. Hakuna asiyeona mazuri anayofanya rais na serikali yake lakini pia kuna maovu mazito yanayofanyika ambayo ni muhimu kuyakemea kwa sababu kukemea maovu kuna matokeo chanya zaidi kuliko kusifia nazuri. Tusisahau kwamba watanzania walimchagua rais ili awatedee mazuri. Kwahiyo akitenda mazuri ni wajibu wake akitenda maovu akemewe kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom