Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema ana mpango wa kuifuta Ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) kutokana na changamoto ya udanganyifu wa umri wa wachezaji.
Akizungumza katika kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM, Karia alisema badala yake anapendekeza kuanzishwa kwa ligi ya akiba (reserve league) ambayo itazijumuisha timu za wachezaji waliosajiliwa kwenye klabu za Ligi Kuu na Ligi ya Championship lakini hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye timu za wakubwa.
Kwa mujibu wa Karia, mfumo huo utasaidia kuwapa wachezaji hao muda wa kucheza, kuendeleza vipaji vyao na kupunguza changamoto ya udanganyifu wa umri inayodaiwa kujitokeza katika ligi za vijana
==============
"Kwa hiyo ni ligi ya under 20 mimi kwanza nataka niifute."
"Udanganyifu mkubwa sana... hawachezi kwenye umri wao. Vidabu vinatudanganya."
"Kwa hiyo mimi nataka turekebishe nataka niongee na mdhamini tuite reserve lige... kama South Africa."
"...ichezwe wale wanaowaita under 20 na wengine ambao wa timu kubwa ambao hawapati nafasi ya kucheza waweze kucheza kwa sababu pia inatusaidia hata wachezaji wetu hawa ambao ni national team potential ambao wanasajiliwa na na timu kubwa hizi alafu hawapati nafasi za kucheza basi wacheze kwenye zile reserve ligi ili tuweze kuwalinda lakini pia na kukwepa huo udanganyifu. Amesema Karia