Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Tatua kwa kutumia cheti cha shule ya msingi darasa la nne utafanikiwa kupata umri sahihi, hana cheti achana naye.Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema ana mpango wa kuifuta Ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) kutokana na changamoto ya udanganyifu wa umri wa wachezaji.
Akizungumza katika kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM, Karia alisema badala yake anapendekeza kuanzishwa kwa ligi ya akiba (reserve league) ambayo itazijumuisha timu za wachezaji waliosajiliwa kwenye klabu za Ligi Kuu na Ligi ya Championship lakini hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye timu za wakubwa.
Kwa mujibu wa Karia, mfumo huo utasaidia kuwapa wachezaji hao muda wa kucheza, kuendeleza vipaji vyao na kupunguza changamoto ya udanganyifu wa umri inayodaiwa kujitokeza katika ligi za vijana
==============
"Kwa hiyo ni ligi ya under 20 mimi kwanza nataka niifute."
"Udanganyifu mkubwa sana... hawachezi kwenye umri wao. Vidabu vinatudanganya."
"Kwa hiyo mimi nataka turekebishe nataka niongee na mdhamini tuite reserve lige... kama South Africa."
"...ichezwe wale wanaowaita under 20 na wengine ambao wa timu kubwa ambao hawapati nafasi ya kucheza waweze kucheza kwa sababu pia inatusaidia hata wachezaji wetu hawa ambao ni national team potential ambao wanasajiliwa na na timu kubwa hizi alafu hawapati nafasi za kucheza basi wacheze kwenye zile reserve ligi ili tuweze kuwalinda lakini pia na kukwepa huo udanganyifu. Amesema Karia
Ndio akili za mapowerfool hizoo.Ndio namna pekee ya kusolve hilo?
Typical Tanzanian leaders mindset… Zuia, piga marufuku , funga, bomoa.
ina maana mchezaji akikosa tu namba kwenye timu kubwa anaenda kucheza reserve leagu na vipi vile vilabu vinavyofanya rotation ya wachezaji? Au huyo aliyekosa namba akishapata namba kwenye klabu yake atakataliwa kwenye reserve league? Mambo ni mengi ila ngoja nisubiri majibu ya haya machache.Sasa akifuta ligi ya vijana hao wachezaji wa baadaye kwenye vilabu watapatikana kwa kutegemea hiyo reserve league yake itakayojaa wachezaji waliokosa namba kwenye vilabu vyao?
Ni kwamba amekosa kabisa njia mbadala ya kudhibiti udanganyifu wa umri kwenye timu za vijana? Kwa hali basi hata ile timu ya vijana U17 ya Tanzania iliyofika fainali msimu huu, haina uhalisia wa kweli kwenye umri.
Hersi anahusika nini na hili, au Karia na yeye ni msomaliSectors za zimeshikiliwa na wahamiaji haramu, huyo msomali hawatakii mema vijana wa Tanzania
Ndio hersi ni mkimbizi jambazi, si alikuwa anashikilia mkataba wa fei , fei hakukata tamaa akaitafuta haki yake , leo fei toto anakula matunda ya mapinduzi matukufuHersi anahusika nini na hili, au Karia na yeye ni msomali
Njaa isikufanye kuwa mbaguzi, hata wewe ukifatilia utajikuta sio mtanzania halisi,
Kuwa na pua kubwa na nywele za kipilipili hakukufanyi kuwa mtanzania halisi