Uongozi wa Klabu ya Africain ya Tunisia umetuma mashushu ili kuja kuangalia mechi kati ya Yanga na Simba itakayofanyika siku ya tarehe 23 Oktoba. Wataalamu hao wa kusoma mchezo yaani 'match analysts', wanatarajiwa kushuka nchini siku ya Ijumaa na taarifa za ndani zinasema washapata tiketi kwa msaada wa mawakala wanaowapokea walioaminiwa na Ubalozi wa Tunisia.
Watunisia hao wameonekana kuipa umuhimu mechi hiyo ili wajitengenezee mazingira ya kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho kwa kishindo, hivyo Klabu ya Yanga inapaswa kuwa makini katika siku hiyo ya mechi yao dhidi ya Simba kwa kuficha baadhi ya mbinu zao.