Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Ona Sasa? Halafu walivyokuwa wajinga wakishaona mteja kafika bei ya ofisi tu wao hawapati Cha juu wako radhi wamuache mteja huyo aondoke huku wakimkosesha mwenye duka ridhiki... Yaani wanachoangalia wao ni maslahi yao tu basi..

Hebu angalia mfano kama wewe Ina maana endapo kama huyo mwenye duka asingekuwepo karibu basi siku hiyo angeikosa hiyo hela.... Halafu na pia imagine Kuna wateja wangapi wa aina yako wanaofika bei ya ofisi tu na kisha wanaondoka bila ya mwenye duka kujua??

Hawa nzi sio tu wanawapa hasara wateja Bali wanatia hasara mpaka kwa hao jamaa zao wamiliki wa maduka... Halafu watu kama huyu jamaa wa kujiita Kitali anakwambia eti biashara yake imekuwa Sababu ya mawinga!?
 
Dalali si mtu mzuri,kuna mwaka nilikua nauza gari basi madalali wa chipolopolo magomeni wakamleta mteja,yule mteja alifika kwenye bei niliyokua naitaka na kidogo ila madalali walitaka cha juu zaidi,basi waliondoka nae yule mteja huku roho ikiniuma,yule mteja kumbe alikuja na ndugu yake na mimi nilikua na mdogo wangu,wakati madalali wanataka kumpiga na kuniyimisha mimi mteja kumbe yule jamaa wa yule mteja akili ikamcheza na kumgundua mdogo sio miongoni mwa madalali,huku madalali wakivutana jamaa akachukua namba ya mdogo kinyemela,akamshtua ndugu yake waondoke,walipoondoka dogo akaniambia jamaa wa mteja ana namba yetu,baada ya mida jamaa wakampigia dogo tukafanya biashara pasipo wale madalali,baada ya kama miezi 2 hivi madalali wakajua mchezo uliofanyika,aisee walinikuta mtu mwenyewe nawamudu tu ila waliongea hao balaa 😀
 
Watu wenyewe ndiyo wanawaendekeza hao mawinga
Unaenda dukani,duka unaliona
Hakuna haja wala kupoteza muda kumsikiliza winga

Ova
Majuzi nimeenda kwenye duka Moja ukivuka kidogo mataa ya msimbazi.. nilikuwa nimeenda kununua Blender, kufika pale namkuta jamaa mmoja mwenye asili ya kiasia namuuliza kama ntapata blender ya Kenwood... Pale pale akanyanyuka kumuita kijana wake, eti aje anioneshe blender halafu Sasa blender yenyewe ilikuwa pembeni yake alipokuwa amekaa.. aisee baada ya kuona huo upuuzi nikatoka na nje.
 
Wapuz sana hao wenye maduka ndy wanaulea huo ujinga
Dawa ni kuondoka tu,kko upuz mwingi sana

Ova
 
Hao washenzi wakishaletaga mteja huwa wanajionaga wao ndio Wana haki Zaid ya kumuuzia bidhaa kuliko wewe mwenye Mali, yaani walishindwa kumuuzia wao wanaona ni heri huyo mteja asinunue kabisa hiyo bidhaa kwako, na ukifanya nae biashara huwa wanaumia sana na mnaweza mkaingia hata kwenye uhasama mzito..

Yaani wapumbafuu wakishamleta mteja basi haki za mauziano zinakuwa mikononi mwao hata kwenye nyumba za kupangisha ni hivyo hivyo tu, akimletea mteja aione nyumba halafu wakashindwana bei kisha huyo mteja arudi baadae na kupata bei na mwenye nyumba, jamaa wakija kujua wanaweza kutumia hata majambazi usiku huyo mteja... Yaani huwa wanaumia sana utafikiri na wakati kazi yenyewe wanayoifanya ni ya kuongea ongea tu... Wajinga sana hao
 
Mtaa wa masoko.
Akili kubwa hii
 
Ukitaka kurogwa uje ujaribu huo mchezo wako ,
Uje uwageuke madalali wa vyumba , tutakutupia majini
 
Acha kelele huna duka Wala Nini wewe ni winga tu tajiri hawezi kuja hapa kupiga kelele na tunaraka serikali ifukuze mawinga wote ni wezi wakubwa mwanaume mzima unakuaje winga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…