Ona Sasa? Halafu walivyokuwa wajinga wakishaona mteja kafika bei ya ofisi tu wao hawapati Cha juu wako radhi wamuache mteja huyo aondoke huku wakimkosesha mwenye duka ridhiki... Yaani wanachoangalia wao ni maslahi yao tu basi..Kariakoo wanakupokea jinsi unavyoenda, ukitaka usisumbuke kabla ya kwenda Kariakoo jaribu kusurvwy bei mtandaoni. Ukifika huko ujue kabisa lasivyo itauziwa mara mbili yake.
Nilienda kununua sabufa tena duka famous kabisa na bei yake nilikuwa naijua, hata imstagram page yake kaweka bei, kufika pale mawinga wakanipokea sabufa ya 175k wakaniambia 300k nikawaambia straight bei yake ni 175k najua bado wanabisha mwisho 270k.
Nikataka kusepa zangu ndio mwenye duka akaniambia njoo uchukue, yaani ni kero mno
Hebu angalia mfano kama wewe Ina maana endapo kama huyo mwenye duka asingekuwepo karibu basi siku hiyo angeikosa hiyo hela.... Halafu na pia imagine Kuna wateja wangapi wa aina yako wanaofika bei ya ofisi tu na kisha wanaondoka bila ya mwenye duka kujua??
Hawa nzi sio tu wanawapa hasara wateja Bali wanatia hasara mpaka kwa hao jamaa zao wamiliki wa maduka... Halafu watu kama huyu jamaa wa kujiita Kitali anakwambia eti biashara yake imekuwa Sababu ya mawinga!?