A
Anonymous
Guest
Kwa sasa ni siku kadhaa hali imekuwa hivyo, yanatiririka barabarani, hali hii imekuwa kero kubwa kwa watembea kwa miguu, hasa pale wanapopishana na Vyombo vya Moto na kurushiwa maji hayo taka.
Hali hii inaweza kuhatarisha afya za wananchi na kuongeza uwezekano wa mlipuko wa magonjwa, hasa kwa kuwa maeneo hayo yapo karibu na Wafanyabiashara wa vyakula ambao hutuhudumia kila siku.
📍 Eneo: Likoma & Masasi Street, Kariakoo – Dar es Salaam
Mamlaka husika zifuatilie na kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo hili kabla halijasababisha madhara makubwa zaidi kwa afya na usalama wa wananchi.