Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Umaskini mbaya sana.. tafuta hela mkuu.

Hayo maviatu fake utaona ni uchafu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Comment Yako haipo fair.

Huenda hajafika anapotaka kufika katika maisha yake lakini ananunua anachotaka kwa hela yake bila kuiba kwa mtu.

Muache afurahie kidogo anachopata. Huenda unamuona yeye ni masikini kwa macho Yako ila na wewe hapo ni masikini wa kutupwa kwa mwingine.

We are not the same. Look at the fingers on your hand. They are not the same. Yes that's how we differ.
 
Hivi faida ya kuvaa viatu original iko wapi hasa?? Kwamba ufahari wa kuonekana umevaa maviatu ya gharama ndefu? Nani kwanza atajua kama umevaa OG au fake ikiwa kwa muonekano havina tofauti.
Faida ipo wewe. Juzi nimenunua Vans mpya hapo Kariakoo shimoni kwa 20k ila najua ina masharti kibao. Kwanza inabidi usiianike kwenye jua kabisa, yani bora uianike ndani hata wiki kuliko juani masaa mawili. Wakati huo ningenunua Vans original kwa 40k ningeanika juani kiasi mpaka ikauke. Pia material yanachoka mapema, unakuta mavitambaa yanatengeneza shape mbaya ukivaa.

Nina Air Jordan original kibongobongo (kule mbele bado ni fake) sijawahi ijutia mwaka wa pili sasa. Nina t-shirts fake hizi za Burberry zimeongezeka hapa bongo zishachoka miezi michache. Nilinunua haya matambala ya Zara yanapauka na kutanuka, kwanza yanachafuka haraka.
Nina Off-White original iko vizuri. Ukitaka kuona uzuri wa mavazi original nunua rangi nyeusi au nyeupe. Nikipata pesa ni vitu OG tu.
 
Nakusalimia kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Nimekumisi tu basi.... hamna kingine.

Kwa kikwetu, ili kuweka msisitizo, naeza sema I miss you, missn't I?
Miss you too.

🤣🤣🤣

Mi nilishindwa na kikwenu Bana.
 

Kaka umekuja mjini kwa shemeji yako lini?
 
Hizo raba ni nzuri maalim kikubwa matunzo tu, wanaosema feki kutoka China hali ya kua asilimia 80 ya Watz tunatumia vitu feki kutoka China,
Jamii forum ni ulimwengu wa matajiri wanaotumia vitu kutoka UK, GERMANY, FRANCE na USA,

Ukija kwenye uhalisia sasa,, vimechoka vimefubaa vingine hadi vyakimbia kuonana kwa aibu ya kufake maisha humu.
 
Tofauti ni durability. OG utadumu nacho zaidi maana imara
Kuna kiatu nilinunua duka flani hivi la wasabato pale Mwenge sijui kama bado lipo, aisee wale jamaa wanauza ngozi original kabisa. Yani kile kiatu mpak sasa hivi bado kiko vile vile na ninavaa kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…