Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Faida ipo wewe. Juzi nimenunua Vans mpya hapo Kariakoo shimoni kwa 20k ila najua ina masharti kibao. Kwanza inabidi usiianike kwenye jua kabisa, yani bora uianike ndani hata wiki kuliko juani masaa mawili. Wakati huo ningenunua Vans original kwa 40k ningeanika juani kiasi mpaka ikauke. Pia material yanachoka mapema, unakuta mavitambaa yanatengeneza shape mbaya ukivaa...
Sijaona umuhimu wa OG.

Sasa kama unanunua kitu ili ukivae mwaka duh mbona ni indicator ya umasikini?

Vaa viatu miezi kadhaa then tupa kulee.

Unamiliki kitu mwaka wakati dukani kila siku something new is arising.

#YNWA
 
Sijaona umuhimu wa OG.
Sasa kama unanunua kitu ili ukivae mwaka duh mbona ni indicator ya umasikini?

Vaa viatu miezi kadhaa then tupa kulee.
Unamiliki kitu mwaka wakati dukani kila siku something new is arising.

#YNWA
Ni umaskini mkubwa sana kununua vitu ili uishi navyo muda mfupi kwa vile vitaharibika mapema.

Ni tabia za watu maskini kununua counterfeit, knockoffs, fake products zenye bei nafuu na ubora hafifu huku wakijisifia wamebana matumizi.
Ni umaskini vilevile kupenda kuwa na vitu vipya ila feki. Yani mtu kuhesabu idadi ya pair za aina ileile ulizonunua kwa mwaka kisa zilikuwa feki hazidumu ndio umaskini wenyewe. Badala yake ungejivunia kitu halisi.

Nenda kwa wenye hela unakuta ana collection ya viatu kibao quality vina miaka hata minne anavaa hata 6× per year. Kiatu nakinunua 30k nakitunzaje miaka
 
Duuh... The power of social media.
Kila mtu ana hela. Kila mtu mjanja.
Kila mtu ananunua vitu vyote OG.
Kila mtu tajiri, masikini hawapo.
Kila mtu anavaa viatu vyenye thamani kuanzia 50,000 kupanda juu!!

MATAKO YANGU MIEEEEE MASIKINIIII
 
Safi mimi maskini. Haya wewe tajiri una hela gani kapuku tu... Zaidi ya kuning'iniza kengele na mrija wa mkojo una nini hasa unachojivunia? Taja namie nitaje.

[emoji23][emoji23][emoji23] huwa unanifurahisha unaenda nao hivyo hivyo
 
Sijaona umuhimu wa OG.
Sasa kama unanunua kitu ili ukivae mwaka duh mbona ni indicator ya umasikini?

Vaa viatu miezi kadhaa then tupa kulee.
Unamiliki kitu mwaka wakati dukani kila siku something new is arising.

#YNWA
Ulichozungumza hapo ni tabia ya kimasikini. Hakuna tajiri anae nunua kiatu bei rahisi ili kiishe baada ya wiki anunue kingine.
 
I don't care. Uzuri nikivaa hakuna anayejua nimevaa fake boots. Naonekana nimevaa viatu vya gharama kubwa sana. Huoni mimi ndio mjanja?
Wake za watu hamtakagi ujinga nyie. Leo unapika nn kwenye futari?
 
Hizo raba za 60K au 70K siwezi nunua kwanza sina pesa pili itaniuma nijibane vyote hivyo halafu kiatu hicho hicho nikute ni sare maua.

Kuhusu mleta uzi ni dhahiri hiki kiatu siyo ishu. Utakuta soli ni plastic, kitambaa ni cha kuteleza na masponji ni mengi.

So raba na viatu vya ofisi hua nanunua za mtumba. Karume.
 
Kila mtu tajiri, masikini hawapo.
Kila mtu anavaa viatu vyenye thamani kuanzia 50,000 kupanda juu!!
1619417034395.png

Wachache hatuna makuu.
 
Duuh... The power of social media.
Kila mtu ana hela. Kila mtu mjanja.
Kila mtu ananunua vitu vyote OG.
Kila mtu tajiri, masikini hawapo.
Kila mtu anavaa viatu vyenye thamani kuanzia 50,000 kupanda juu!!

MATAKO YANGU MIEEEEE MASIKINIIII
Na kila mtu Passo kwake ni gari ya kuendea sokoni mfanyakazi wake wa ndani.
 
Kariakoo baba lao.

Nilikua nimeenda kununua Tende pale Msimbazi msikiti wa Idrisa kwa ajili ya iftar (kufuturisha Waislamu wenzangu nipate thawabu kwa Mola wangu. Yaani pamoja na kuwa na tabia chafu ya kutembea na wake za watu lakin najivunia kuwa Muislamu aisee. Inshallah mwaka huu nikioa nitatulia).

Sasa wakat naondoka nikapita mitaa ya katikati mule, nikaona meza moja Raba kali kinoma, zile wanaziiitaga Air Jordan, Nike, NBA snickers. Kuulizia bei zake akaanzia 20,000!

Daaah nikavikagua na kuanza kujisemea moyoni hivi si naonaga akina David Sportswear, Robyone, NjooKariakoo2020 wanauza kuanzia 65,000 mpaka 70, 0000!!!

Nikamwambia mshikaji mie nina 14,000 akanitolea nje. Nikasepa, akaniita akasema ongeza buku. Nikampa 15,000 nikabeba.

Wakuu, kumbe madukani huwa mnaibiwa. Vitu vya kijanja kwa bei za kijanja vyote vipo Kariakoo.

View attachment 1764016
Kakupiga zinauzwa 10. Ia hakuna kitu hapo
 
Back
Top Bottom