View attachment 1184843
1. Mwanzo kabisa kule panaitwa Gerezani hapo kuna karakana zinatengeneza vitu achaaaa, Kuanzia dude la kupikia vitumbua hadi PIMP my ride! Hapo hapo karibu Building and construction materials.
2. Ukivuka Uhuru street pia kuna construction materials kiasi, ikafuata nguo na Viatu hasa mtaa wa Congo na Mtaa wa Narung’ombe (hapa huna hata pa kukanyaga ( Wanapaita China Town sasa) Hapa ndio soko la viatu, Ndio penyewe.
3.Jengo lenyewe la kariakoo kama kawa, una pata kila kitu hadi plau pezi [emoji23]. Pesticides etc
4 . Shuka chini kidogo mtaa wa mafia unakutana na Pikipiki, Na spare parts.
5 Chini kidogo unapata pia Kila spare parts ya gari yoyote hadi wana Toyota Tanzania ( Genuine Parts)
6. Hapo tunazungumzia Upande wa Kushoto wa Msimbazi street. Kulia kuna maeneo ya Agrey, pale unapata simu yoyote unayoijua wewe na pia unatengenezewa simu yako hata kama imeharibika vipi, ukishika chini upande huo huo wa kulia kuna soko la vitambaa. Hatari.
Hapo kariakoo usiku ndio utajua Kariakoo sio ya mchezo, kila mtaa unazibwa containers zinashusha mizigo.
Zimbwabean, Zambian, Namibian, Botswana , Congo , Shelisheli, Comoro wanadaka mzigo hapo.
Ukitaka kujua nani anakuja sana kuchukua mizigo Hapo kariakoo, Tembelea Hotel zote za karikaoo.
Hadi sasa kuna vijana kazi yao ni kupack mizigo, wamespecialize Wanajua jinsi ya kupanga bwana. Corona vya wazambia na wazimbabwe lazima vishindiliwe vizuri.
Yaani ni Guangzhou ya bongo Maana Kule hadi wanaigeria wamespecialize Kupack mizigo. [emoji23]
Sijaongelea kule lumumba, Duh, Car accessories , Music mnene wa gari yako , Tairi etc ndio pale . Inapark Modern Coast na Tahmeed.
Kulingana na mizigo inayobebwa hapo, kama hadi godoro mtu kapakia, Labda awe anashukia Tanga, Hata kama anaenda nalo mombasa, Basi litakua bora sana , Au lipo cheap kuliko huko? Au kapewa bure zawadi, yote yanaweza tokea [emoji23]
Kariakoo noma bwana.
Kuna jamaa alipost Malls hapo juu.
Mkuki House, Aura Mall, City mall zote zipo in a walking distance .
Nadhani hakuelewa maana ya mkuu Hapo juu.