Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetangaza kuanza zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wa Kariakoo wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi ya barabara pamoja na kwenye njia za watembea kwa miguu.
Hoja hii ilianzia hapa ~ Usalama wa watembea kwa miguu Msimbazi - Kariakoo, Je, Mamlaka wanaliona tatizo?
Katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo, yamebandikwa matangazo yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Jiji, Elihuruma Mabelya, yakiwataka wafanyabiashara wote wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi, hususan barabarani na kwenye njia za watembea kwa miguu, kupisha maeneo hayo.
Maagizo hayo yameelezwa kuwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, yaliyotolewa wakati wa ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo katika hafla iliyohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika hafla hiyo, Chalamila alisema kuanza kwa shughuli katika soko hilo kutaambatana na kufunguliwa kwa barabara zote zinazoingia na kutoka Kariakoo ili ziwe wazi kwa matumizi ya umma.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mdau wa JamiiForums alidai kwamba watembea kwa miguu wanaotumia Barabara Kuu, kipande cha Msimbazi, usalama wao upo hatarini kutokana na njia yao rasmi kuzibwa na wafanyabiashara wadogo (machinga) pamoja na bodaboda.