Karibu kwetu tukuhudumie mkopo usio na riba wala dhamana

Karibu kwetu tukuhudumie mkopo usio na riba wala dhamana

Habari wakuu katika pitapita zangu humu jf nimekutana na huu uzi wa mkuu great kali binafsi nilikuwa na mawili au matatu ya kuzungumza juu ya hiyo kampuni japokuwa kila mmoja ana imani yake naomba nianze hivi mnamo tar 22/06/2018 nilikutana na tangazo la huyu jamaa na nambari zake za simu ni hizo hizo nikafanya nae mawasiliano nikihitaji mkopo wa tsh 4,000,000 nikamuuliza juu ya vigezo akinielezea finally shughuli ikaja kwenye kutuma pesa ya surveyor aje kukagua aisee kwa mambo ya mtandao yalivyo ilinichukulia takribani siku tatu kufikiria mwisho wa siku nikajitoa kimaso maso nikatuma pesa ya surveyor nikiamini kama nimehonga pesa yangu baada ya siku moja surveyor alifika ofisini kwangu na kukagua ilichukuwa siku moja kufika kwa sababu ofisi zao zipo mpanda baada ya surveyor kufika aliidhinisha mkopo wangu wa 4,000,000 kama picha inavyoonyesha hapo chini,sina la zaidi.
BARIKIWAView attachment 800855
Naona unajitekenya na kucheka mwenyewe. Kama kuna vichaa basi watavutika na ushuhuda wako
 
Wekeni ile TIN yako au yenu humu kwa uwazi na anuani ya ofisi..

Hayo ya gmail acha kutaka kuliza watu

Usajili wa kampuni kila kitu weka wazi..
 
Asiyejua maana usimwambie maana,maana ukimwambia maana ataharibu maana.
Utajibu kila aina ya misemo ya kiswahili, lakini ukweli ni kuwa unachofanya ni utapeli tu.

Mimi naonea huruma watanzania masikini na wajinga wanaoweza kuingia katika utapeli wako na kweli wakakutumia pesa

Sielewi ni kwa vipi Mods wamekuachia mpaka sasa unaendelea ku post ujinga huu
 
Hivi ukimchaji Tshs 100,000/= ya surveyor kwa anayekopa 100,000/= hapo utakuwa umemsaidia ama umemuuzia deni? Hapo hujaweka gharama nyingine kama fomu nk! [emoji21]
 
Ofisi zao zipo mpanda katavi, mkopo ndani ya saa sita baada ya surveyor kuthibitisha, je kwa Mie niliyopo dar, mwanza, iringa, kigoma N.K mnaweza kunifikia kunipa mkopo wangu huo pamoja na kufanya survey?

Acheni utapeli ndugu zanguni ni bora mjikite kwenye kilimo na shughuli halali za kuwaingizia kipato, mtakufa siku si zenu.
 
Ni vyema sasa matangazo yoyote Yale yanayowekwa na kutolewa sehemu mbalimbali wahusika iwe ni lazima waambatanishe namba za usajili wa makampuni yao ili watu wawe wanathibitisha brela kama kampuni limesajiliwa au la hata kama utapeli ukitokea basi wahusika na wamiliki wa kampuni waweza kupatikana..

JESHI LA POLISI MSIMAMIE HILI NA WIZARA YA AJIRA NA KAZI WEKENI UTARATIBU KWA KUUNDA SHERIA /KANUNI NDOGO NDOGO ZA NAMNA YA UTOAJI MATANGAZO MBALI MBALI.
 
KAMPUNI YA KUTOA MIKOPO "AKOK LOANS"

Ni taasisi ya kifedha inayohusika na utoaji mikopo nafuu iliyokuwa na riba nafuu kupitia mfuko maalum uitwao AKOK Credit & Loans kwa dhumuni la kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa nchini Tanzania kwa kuwapatia mikopo ya pesa NA Pembejeo za kilimo na Ufugaji kwa lengo la kuwainua kiuchumi
na kuwaletea maendeleo ili waweze kujikimu kimaisha kwa dhana yakinifu kutaka kutokomeza umasikini.

Kampuni ya AKOK LOANS
Ilianzishwa mwaka
2008 ikiwa kama tawi zawa lisilojitegemea ambapo iliingia ubia na Bank ya NBC ( National Bank of
Commerce) kwa makubaliano ya mikataba ya muda.
Ndani ya muda wote huo, kampuni ilikua inashughulika kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali tu wakiwemo walimu ambao walipewa kipaumbele kikubwa.
Kampuni ya AKOK Loans imemaliza mikataba rasmi na Bank ya NBC hivyo imeanza rasmi kujitegemea na kuunda mfuko
huu wa AKOK Credit & Loans.
Kampuni ya AKOK Loans imeanza hatua za kutaka kusambaza
matawi yake mikoa yote nchini Tanzania ili kila mtanzania aweze kupata huduma za mikopo kwa ukaribu.
Kwa sasa kampuni ya Inuka Loans ina ofsi moja ambayo ndio makao makuu ya kampuni hii.

MTANZANIA ATAWEZAJE KUPATA MKOPO?

Mikopo inatolewa kwa kila mtanzania bila ya kuwepo na
ubaguzi wa aina yoyote. Huduma zetu ni stahiki kwa
kila mtanzania ambae ni mjasiriamali, mtumishi wa serikali au mfanyakazi wa kampuni binafsi, wote wanastahili kujiunga na kuwa
washirika wetu na
tutawapatia mikopo.
Wakati tukiwa katika
maandalizi ya kusambaza matawi yetu katika mikoa mbalimbali, inamlazimu mteja wetu ambae atahitaji mkopo
kuweza kujiunga au kutuma maombi ya mkopo ambayo atawasiliana na afsa mawasiliano wa kampuni kwa njia ya email au kwa njia ya WhatsApp.
Baada ya mteja kuwasiliana nasi, mkopo wake yataidhinishwa na atapatiwa mkopo wake wa pesa aliyo omba ndani ya masaa 6 tu baada ya MKAGUZI KUFIKA.

SIFA ZA MWOMBAJI.

Sifa kuu za mwombaji anaetaka kuomba mkopo ni kama zifuatazo:-

(i) UWE MWAMINIFU

(ii) *UWE NA AKILI TIMAMU*

(iii) *UWE NA UMRI KUANZIA MIAKA 18 AU ZAIDI*

(iv) *UWE NI MTANZANIA*

(v) *UWE NA KITAMBULISHO*
*KIMOJA WAPO KATI YA HIVI*

MPIGA KURA, KITAMBULISHO CHA KAZI, CHUO, LESENI YA BIASHARA, LESENI YA DREVA, KITAMBULISHO CHA TAIFA au PASSPORT YA KUSAFIRIA

*KWANINI* *TUNATOA MIKOPO*
*NAFUU YENYE* *MASHARTI RAHISI?*

Watanzania wengi wanaweza kujiuliza kwanini kampuni ya AKOK Loans inatoa mikopo kwa
watanzania yenye masharti rahisi sana tofauti na asasi
zingine walizozizoea kama bank na nyinginezo!
Sababu kuu ya kuweka masharti rahisi ni kutaka kumsaidia kila mtanzania kuweza kupata mikopo bila kumuwekea vikwazo vigumu ambavyo vitakatisha ndoto zake na kumfanya awe dhaifu katika maendeleo yake kwa kukosa mkopo kutokana na vigezo
vyetu kua vigumu kwa maana dhamira yetu kuu ni kutaka
kumsaidia kila mtanzania, hivyo hakuna sababu
yakuweka ugumu wa upatikanaji wa mikopo.

*MTEJA ATAUPOKEA MKOPO*
*WAKE KWA MUDA GANI?*

BAADA YA KULIPA ADA NA KUJAZA FOMU .
Mikopo yetu haicheleweshwi
kwa mteja wetu atakae timiza vigezo na masharti atapatiwa mkopo wake ndani masaa 6 baada ya MKAGUZI KUFIKA na kurejesha TAARIFA kwetu.

*MTEJA ANARUHUSIWA KUKOPA KUANZIA SHILINGI NGAPI?*

Mteja anaruhusiwa kuomba mkopo kuanzia (LAKI MOJA ) 100,000 Hadi Tshs. 10,000,000 (MILLION KUMI)

*MTEJA ATAPOKEA MKOPO BAADAYA MASAA SITA BAADA YA MKAGUZI KUFIKA KATIKA ENEO LAKO LA KAZI*
*Tumeanzisha utaratibu huu wa*
*kufanya mikopo kwa njia ya mtandao* *kulingana na sababu* *kubwa ya upungufu au ukosefu wa* *matawi yetu kutoenea katika mikoa yote Tanzania hivyo* *tumemrahisishia kila* *mtanzania ambae* *yupo mkoani na anahitaji kupata mkopo*


*KIASI CHA MKOPO, ADA NA MUDA WA MAREJESHO*

1. MKOPO WA LAKI MOJA, (100,000) UNACHUKUA MIEZI MINNE AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA SH. ELFU ISHIRINI NA TANO ( 25000) BILA RIBA.

2. MKOPO WA LAKI MBILI (200,000) UNACHUKUA MIEZI SITA AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA SH. ELFU THELATHINI NA TANO (35000) NA MWEZI ULE WA MWISHO UTATEJESHA (25000) BADALA YA 35000

3. MKOPO WA LAKI TATU (300,000) UNACHUKUA MIEZI NANE AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA ELFU THELATHINI NA SABA MIATANO (37500)

4. MKOPO WA LAKI NNE (400,000) UNACHUKUA MIEZI KUMI AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA ELFU HAMSINI (40000)

5. MKOPO WA LAKI TANO (500,000) UNACHUKUA MIEZI KUMI NA MBILI AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA ELFU AROBAINI NA MOJA MIA SABA (41700)

6. MKOPO WA LAKI SITA (600,000) UNACHUKUA MIEZI KUMI NA NNE AMBAPO KILA MWEZI UNAREJESHA ELFU AROBAINI NA MBILI MIA TISA (42900)

7. MKOPO WA LAKI SABA (700,000) UNACHUKUA MIEZI KUMI NA SITA AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA ELFU AROBAINI NA TATU MIA SABA HAMSINI (43750)

8. MKOPO WA MILLION 5(5,000,000) UNACHUKUA MIEZI KUMI NA NANE AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA ELFU AROBAINI NA NNE MIA TANO (44500)

9. MKOPO WA MILLION 6 (6,000,000) UNACHUKUA MIEZI ISHIRINI AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA ELFU (90,000)

10. MKOPO WA MILIONI KUMI (10,000,000) UNACHUKUA MIEZI ISHIRINI NA MBILI AMBAPO KILA MWEZI UTAREJESHA LAKI NNE NA HAMSINI (450000)

*LAKINI PIA MTEJA UNARUHUSIWA KULIPA NA KUMALIZA DENI LAKO KWA MUDA WOWOTE ULIO NDANI YA MKATABA NA SIO NJE YA MKATABA*

ENDAPO UTASHINDWA KULIPA DENI, AU KUCHELEWA KULIPA PASIPO KUTOA TAARIFA, HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA IKIWEMO KUKAMATWA WEWE PAMOJA NA WADHAMINI WAKO WATANO, KUFILISIWA MALI ZAKO NA KUSHITAKIWA MAHAKANI KWA KOSA LA KUWA MDAIWA SUGU

*KARIBU SASA* *UPATE MKOPO WA* *HARAKA NA* *NAFUU*

+255 762 322 970
Email: kaziajira01@gmail.com
6000000 unapewa unarudisha 90,000 kwa miezi 20 = 1800000 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16] duh kweli za kuambiwa changanya na zako
 
Mtoe tu mikopo bila faida yoyote ile? Hata nyie wezi. Fafanueni hiyo ada ya kujiunga tuone
Kuna kitu wanafaidika hapo, we soma vizuri utagundua ada yako ya kujiunga ili kupata mkopo huo ndio faida yao, lakin pia ukishindwa kulipa ndani ya wakati imekula kwako na wao hufaidika mara nying zaid
 
6000000 unapewa unarudisha 90,000 kwa miezi 20 = 1800000 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16] duh kweli za kuambiwa changanya na zako
Hapana kuna vitu hataki kuvitaja hapa nadhani hiyo 1,800,000= ndio riba anayoita ADA na mkopo(Principal) upo pale pale... = 6,000,000 gawa 20 =300,000 + 90,000= sh 390,000 @ mwz
jumla utalipa sh 390,000 x 20 = 7,800,000 ni sawa na riba ya 32% wakati wao bank wanakopa 18%, Biashara iko wazi hajui tu kujieleza japo riba ni kubwa sana hakuna msaada hapo anaokota pesa nyingi sana kwa wajinga
 
Hapana kuna vitu hataki kuvitaja hapa nadhani hiyo 1,800,000= ndio riba anayoita ADA na mkopo(Principal) upo pale pale... = 6,000,000 gawa 20 =300,000 + 90,000= sh 390,000 @ mwz
jumla utalipa sh 390,000 x 20 = 7,800,000 ni sawa na riba ya 32% wakati wao bank wanakopa 18%, Biashara iko wazi hajui tu kujieleza japo riba ni kubwa sana hakuna msaada hapo anaokota pesa nyingi sana kwa wajinga
Hakuna mkopo ukitaka kujua kuwa ni utapeli eti mawasiliano whatsapp na kwa email, wakulima wengi hawatumii hivyo vitu. Halafu ebu tumia akili ya kawaida ni nani akukope ela bila collateral? wanachotaka hapa ni watu wanaopenda mterezo waingie king wapigwe hiyo ela ya ada basi hakuna jambo lingine na nina hakika washapigwa.
We hata hakuna sehemu alipokutajia ofsi zao zilipo yani hawana physical address
 
Humu naona wanaotetea ndo hao hao wanaitangaza hiyo mikopo...tumieni akili zaidi...bora kukosa pesa nyingi kuliko kutapeliwa laki moja. Hizo laki moja wakizipata 100, kwa awamu hii wako vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom