Karibu Mama Samia Suluhu Hassan, Timu JPM Tunakuunga Mkono100%

Karibu Mama Samia Suluhu Hassan, Timu JPM Tunakuunga Mkono100%

Team JPM

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2018
Posts
1,307
Reaction score
2,037
Pamoja na majonzi na masikitiko makubwa ya kumpoteza Team Leader wetu, Hayati Dkt John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba yetu imetupa faraja kwamba Mama yetu Mpendwa unashika rasmi kiti cha Urais.

Tunaishukuru sana katiba hii na wale walioiandaaa maana vinginevyo ingekuwa patashika nani awe Rais wa awamu ya Sita.

Sisi Timu JPM, tunakupokea kwa mikono miwili na tunaahidi kukuunga mkono katika kulitumikia taifa kwa cheo cha Urais.

Tunaamini kwamba, ndani ya miaka sita ukifanya kazi bega kwa bega na Mheshimiwa Rais Magufuli, umejifunza mengi na kupata maarifa, ujuzi na uzoefu katika Uongozi, siasa, uchumi, huduma za jamii, ulinzi wa taifa, chaguzi, usimamizi wa miradi, mahusiano ya kimataifa n.k
Tunaamini yapo mema utakayoyaendeleza na yapo utakayoboresha zaidi.

Tupo nawe pamoja, chapa kazi mama.

Kwa bandiko hili, niwashawishi wenzangu wooote Timu Magufuli tumuunge mkono Mama huyu Muungwana na mwenye hekima ili aongoze vyema. Usiku na mchana, mvua au jua, tusimame pamoja maana ameondoka Baba, Tumebaki na Mama, Tumuunge mkono.

Hongera sana Mama yetu, Tupo Pamoja nawe
 
Tupo pamoja, tupo nyuma yako, ng'ong'o ng'ong'o ng'ong'o!
Hivi maisha bila kulamba viatu vya watawala hamuwezi?
Si ni nyie ndo mlikuwa mnasema hakuna mtu wa kuongoza nchi hii zaidi ya marehemu?
Kumbe Samia anaweza? Nyambafu zenu.
Mmeanza kujipenyeza kwa mama ili mkaponze tu mpate kula yenu siyo?
Mhe, rais wetu, kaa mbali na MATAGA, nasisitiza kaa mbali na MATAGA.
Wakajiajri mtaani KENGE hao
 
Mama ssh tunakuomba mama achana kabisa na team jpm watakufitini hao achana nao kabisa mama na ukitaka ubarikiwe jitenge Nao watakuharibia ila napata faraja kuona wazanzibari sio wanafiki na uislam hautaki wanafiki.
 
Namuona MUSIBA hapo katika ubora wake!!! Tulizeni bori mama Samia atengeneze team yake!!! Wale waliookotwa jalalani hawana nafasi kwa mama ; sasa hivi ni team mama, JIWE alikuwa hawathamini wanawake hivyo msishangae mkaona mama Asha Rose Migiro anarudi mambo ya nje!!!
 
Mimi naomba ile desturi yetu tuliyojiwekea wana-CCM ya kumwachia mgombea wetu wa kiti cha urais kugombea awamu ya pili bila kuwa na mshindani iendele kama kawaida.

Hivyo ieleweke mgombea wetu wa mwaka 2025 ni mama yetu SSH na si vinginevyo.

Wengine labda wajipange 2030 huko.
 
Mimi naomba ile desturi yetu tuliyojiwekea wana-CCM ya kumwachia mgombea wetu wa kiti cha urais kugombea awamu ya pili bila kuwa na mshindani.
Hivyo ieleweke mgombea wetu wa mwaka 2025 ni mama yetu SSH na si vinginevyo.
Wengine labda wajipange 2030 huko.
Sio jambo la kuongea kwa woga, rais wetu mama Samia Suluhu ni mpaka 2030 akitupendeza zaidi basi nae tunamuongezea muda
 
Serikali iko imara sana,

Ashukuriwe sana John Pombe Magufuli kwa kumchagua Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake awamu ya kwanza..... na kumchagua tena awamu ya pili.

Hakika Mungu alijua kumtumia Magufuli kuanzia kuijenga Tanzania hadi kuandaa warithi makini katika kuliongoza taifa

Viongozi makini huchagua wasaidizi makini sana

Kila la heri Madame President Samia Suluhu Hassan ❤🇹🇿💥

Lala salama shujaa wetu John Pombe Magufuli 💔💔🙏
 
Serikali iko imara sana,

Ashukuriwe sana John Pombe Magufuli kwa kumchagua Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake awamu ya kwanza..... na kumchagua tena awamu ya pili.

Hakika Mungu alijua kumtumia Magufuli kuanzia kuijenga Tanzania hadi kuandaa warithi makini katika kuliongoza taifa

Viongozi makini huchagua wasaidizi makini sana

Kila la heri Madame President Samia Suluhu Hassan [emoji173][emoji1241][emoji95]

Lala salama shujaa wetu John Pombe Magufuli [emoji174][emoji174][emoji120]
Teh teh teh kweli ukiwa mnafiki na mishipa ya aibu inakata,hivi ile mitano tena imeishia wapi?
 
Sio jambo la kuongea kwa woga, rais wetu mama Samia Suluhu ni mpaka 2030 akitupendeza zaidi basi nae tunamuongezea muda
Kuna viongozi wakisoma comment kama hii wanaishia kusonya tu.

Watu walikuwa wanasubiri miaka mitano tu ili wagombee, sasa itabidi wasubiri miaka kumi, January Makamba tu atakuwa na mzee wa 50+ sijamtaja Lukuvi hapo.
Huu utaratibu wetu wana CCM ufuatwe kama miaka yote, 2025 ni Samia.
 

Tupo pamoja, tupo nyuma yako, ng'ong'o ng'ong'o ng'ong'o!

Hivi maisha bila kulamba viatu vya watawala hamuwezi?
Si ni nyie ndo mlikuwa mnasema hakuna mtu wa kuongoza nchi hii zaidi ya marehemu?
Kumbe Samia anaweza? Nyambafu zenu.
Mmeanza kujipenyeza kwa mama ili mkaponze tu mpate kula yenu siyo?
Mhe, rais wetu, kaa mbali na MATAGA, nasisitiza kaa mbali na MATAGA.
Wakajiajri mtaani KENGE hao[emoji23]
 
Back
Top Bottom