Karibu Tujifunze: VICOBA na changamoto ya utunzaji wa Kumbukumbu

Karibu Tujifunze: VICOBA na changamoto ya utunzaji wa Kumbukumbu

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
1,698
Reaction score
1,783
Wana Jukwaa Habari!

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu kuanzisha na wengine kujiunga kwenye VICOBA. Na ki-uhalisia imekuwa msaada mkubwa sana kwa watu ambao wamekosa sifa za kukopesheka kutoka kwenye mifumo rasmi ya kukopa, mfano bank.

Nakumbuka miaka mitatu (3) iliyopita nikiwa na Vijana wenzangu, nikatoa wazo la kuunda kikundi kwa mfumo wa VICOBA. Tukaweka mikakati, na tukakubaliana kuwa VICOBA tutakayoanzisha haitakuwa na ukomo, yaani hakuna “Kuvunja” na lengo letu ilikuwa baada ya miaka 5 iwe SACCOSS.

Basi bwana, tukaanza mchakato wa kusaka wanachama, ndani ya mwezi mmoja tukawa na wanachama wapatao 20. Tukachagua uongozi, kwa maana ya Mwenyekiti, Katibu, Mhazini na Afisa Mikopo. Kwa kuanza tulikubaliana kutumia platform ya M-KOBA.

Tukaanza mchakato wa kutengeza katiba, tukaweka sheria za mikopo, ununuzi wa hisa na ulipaji wa pesa za jamii.

Mwaka wa Kwanza, tulianza kwa kutumia mfumo “manual” wa utunzaji wa kumbukumbu, yaani tukatengeneza excel yetu, ikawa inakaa kwenye laptop ya katibu. Ki ukweli, palikuwa na changamoto nyingi sana za utunzaji wa kumbukumbu. Mfano utunzaji wa taarifa za miamala ya ununuzi wa hisa, ulipaji wa jamii, ulipaji wa mikopo n.k. Mwaka wa kwanza ulikuwa wa kujifunza zaidi.

Kutokana na changamoto za utunzaji kumbukumbu kwa mwaka wa kwanza, tukapata wazo la kuwa na mfumo wetu wa utunzaji wa kumbukumbu, ambao ni online. Hapo tulipata suluhisho la tatizo la utunzaji wa kumbukumbu.

Kupitia Mfumo:
  • Wanachama wanauwezo wa kuomba mikopo kupitia online/digitally
  • Ufanyaji wa reconciliation umekuwa rahisi zaidi.
  • Utunzaji Taarifa za ununuzi wa hisa, ulipaji wa mikopo na ulipaji wa pesa ya jamii umerahisishwa zaidi
  • Utoaji wa Mikopo umekuwa digitalized, yaani system inamruhusu kila mwanachama kuomba mkopo kulingana na “credit history” yake, ununuaji wa hisa, na historia ya ulipataji wa mikopo yake ya awali.
  • Mfumo wetu tumeunganisha na huduma ya automated sms kwa ku click single button kisha sms inatumwa kwa wanachama. Hii husaidia kukumbusha wanachama ambao tarehe zao za marejesho zimekaribia, kukumbusha ununuzi wa hisa na taarifa zingine za chama
Kwa sasa hivi, mfumo huu tumeufanya uweze kutumika na VICOBA vingine kwa mfumo wa subscription.

Lengo letu ni kuhakikisha Jamii inaondokana na matumizi ya makaratasi katika usimazi wa VICOBA na kuhamia katika mfumo wa digital ambao ki msingi unatoa uhakika wa “going concern” kuliko ule wa kawaida ambao taarifa zikaa kwa katibu/mhazini/mwenyekiti.

Kama ungependa kujaribu mfumo wetu, wasiliana nasi kupitia:
Email: [email protected]
WhatsApp: 0656142433
 
nimekuja mbio mbio kujifunza kumbe ni tangazo,, enwei ngoja waje
 
Back
Top Bottom