Karibu umalizie nyumba kwa mkataba kisha uhamie. Nahama kikazi

siumesema ukimleta ndg yako Toka kijijini itabidi uwe unamgharamia ...Sasa hilo usiogope wewe kamlete gharama hizo unazoogopa ..nitatoa Mimi kwa niaba yako ...undugu kufaana
Asante sana na nashukuru mno.
Ngoja basi tuone tutakapofikia uzi huu kisha tutafahamishana
 
Madalali wa Dodoma kwa ishu kama hizi wanasema huwa zinakuwa na sintofahamu ya mgawanyo maana wanasema wanataka robo bei ya mmaliziaji na mimi mmiliki.
Yaani wachukue kote kote.
Hapo haifai kwa kweli. Hapo pana hitaji utulivu, na Dodoma kwa migogoro hawa jambo. Bora umalizie taratibu mwenyewe.
 
Naomba kueleweshwa hii sentensi tafadhali.

"Pia naweza kumuachia aendelee kukaa bure kama ataimalizia ili aendelee kuniangalizia".
Okay ni hv.
Labda tumepiga hesabu umetumia labda 6Mil.
Na katika mkataba ikaonekana unakaa labda miaka 4 au 3.
Mimi kwa kuwa sitarudi tena Dodoma, naweza kukwambia wewe ukimaliza miaka yako hiyo 4 ya mkataba, endelea tu kuishi bila kunipa kodi (bure) ili uwe unaniangalizia nyumba (hapa pia panahitajika umakini)
 
Safi sana.

Ingelikuwepo option ya kuinunua ingalikuwa poa sana kwangu.

Hiyo mitaa ya Dachi ni sehemu nzuri mno kwa Dodoma.
 
Nakushauri tafuta mtu ailinde uimalizie mwenyewe au akupe fedha uimalizie akae na siyo aimalizie kuna watu siyo waaminifu ataimalizia kwa 10M ataongeza interest ya 10 M utadaiwa 20
 
Duh hapo ndio zile stages za maneno ya Kiingereza. Ujenzi ndio kama unaanza.
 
Safi sana.

Ingelikuwepo option ya kuinunua ingalikuwa poa sana kwangu.

Hiyo mitaa ya Dachi ni sehemu nzuri mno kwa Dodoma.
Pazuri mno.
Ukisimama kwangu, unaiona hospitali ya jiji la Dodoma kwa kule juu mbele.
Pia option ya kuuza ilikuwa ndio kipaumbele changu kabla ya wazo hili.
Ngoja tuone tutakapoishia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…