Karibu umalizie nyumba kwa mkataba kisha uhamie. Nahama kikazi

Karibu umalizie nyumba kwa mkataba kisha uhamie. Nahama kikazi

siumesema ukimleta ndg yako Toka kijijini itabidi uwe unamgharamia ...Sasa hilo usiogope wewe kamlete gharama hizo unazoogopa ..nitatoa Mimi kwa niaba yako ...undugu kufaana
Asante sana na nashukuru mno.
Ngoja basi tuone tutakapofikia uzi huu kisha tutafahamishana
 
Madalali wa Dodoma kwa ishu kama hizi wanasema huwa zinakuwa na sintofahamu ya mgawanyo maana wanasema wanataka robo bei ya mmaliziaji na mimi mmiliki.
Yaani wachukue kote kote.
Hapo haifai kwa kweli. Hapo pana hitaji utulivu, na Dodoma kwa migogoro hawa jambo. Bora umalizie taratibu mwenyewe.
 
Naomba kueleweshwa hii sentensi tafadhali.

"Pia naweza kumuachia aendelee kukaa bure kama ataimalizia ili aendelee kuniangalizia".
Okay ni hv.
Labda tumepiga hesabu umetumia labda 6Mil.
Na katika mkataba ikaonekana unakaa labda miaka 4 au 3.
Mimi kwa kuwa sitarudi tena Dodoma, naweza kukwambia wewe ukimaliza miaka yako hiyo 4 ya mkataba, endelea tu kuishi bila kunipa kodi (bure) ili uwe unaniangalizia nyumba (hapa pia panahitajika umakini)
 
Okay ni hv.
Labda tumepiga hesabu umetumia labda 6Mil.
Na katika mkataba ikaonekana unakaa labda miaka 4 au 3.
Mimi kwa kuwa sitarudi tena Dodoma, naweza kukwambia wewe ukimaliza miaka yako hiyo 4 ya mkataba, endelea tu kuishi bila kunipa kodi (bure) ili uwe unaniangalizia nyumba (hapa pia panahitajika umakini)
Safi sana.

Ingelikuwepo option ya kuinunua ingalikuwa poa sana kwangu.

Hiyo mitaa ya Dachi ni sehemu nzuri mno kwa Dodoma.
 
Nakushauri tafuta mtu ailinde uimalizie mwenyewe au akupe fedha uimalizie akae na siyo aimalizie kuna watu siyo waaminifu ataimalizia kwa 10M ataongeza interest ya 10 M utadaiwa 20
 
Habari za mchana wadau wenzangu wa Jamii Forums.
Iko hivi,
Nilihamishwa Dodoma kikazi mwaka 2019.
Na sasa nimepata uhamisho wa kwenda jijini Mbeya.

Wakati naishi huku Dodoma, nilibahatika kujenga nyumba ila kutokana na majukumu kunizidia nikajikuta nashindwa kuimalizia vyema.

Sasa nakuja kwenu wana Dodoma mnisaidie kitu kama inawezekana.
Je, naweza pata mtu wa kupanga hio nyumba kwa makubaliano kuwa aimalizie finishing kisha ahamie?
Tupigiane mahesabu kuwa ametumia kiasi gani ili tukae chini tujue tunafanyaje?

Pia naweza kumuachia aendelee kukaa bure kama ataimalizia ili aendelee kuniangalizia.
......Hii ni kama Ofa......

Nyumba ina vyumba viwili vyote master, chumba kimoja cha master ni kikubwa (cha baba na mama),

Ina public toilet,
Ina jiko,
Ina stoo.
Ina sebule kubwa.

Nyumba nimeshaipaua tayari na ina vyoo ndani (master kubwa ina choo cha kukaa, public na master ingine ina vyoo vya kuchuchumaa) Vyote vipya.

Nimeshafanya hatua za awali za wiring bado kuingiza nyaya kwenye switch tu.

Nimeshafanya brandering kwa ajili ya gypsum

Karo la choo na chemba zake ziko tayari.

Ina madirisha ya grill na mageti mawili (la mbele na nyuma yenye vitasa vya funguo)

Na mbele ya nyumba kuna eneo kubwa tu limebaki kwa ajili ya ufugaji au kililo akitaka mpangaji.

Atakachomalizia yeye mpangaji.
1. Madirisha ya aliminium
2. Plasta ndani na nje
3. Mlango wa mbele na wa nyuma
4. Kama ataweka gypsum sawa.
5. Kuingiza nyaya za umeme kwenye switch.

Mahali nilikojenga ni Ndachi, hospitali mpya ya Jiji la Dodoma.
Kumejengeka na huduma zote muhimu za kijamii zipo.

Je, naweza pata mtu wa kufanya hivi hapa Dodoma?
Karibuni kwa ushauri, maoni au maswali.
Picha zinakuja hivi punde.
View attachment 3230426

View attachment 3230431
Duh hapo ndio zile stages za maneno ya Kiingereza. Ujenzi ndio kama unaanza.
 
Safi sana.

Ingelikuwepo option ya kuinunua ingalikuwa poa sana kwangu.

Hiyo mitaa ya Dachi ni sehemu nzuri mno kwa Dodoma.
Pazuri mno.
Ukisimama kwangu, unaiona hospitali ya jiji la Dodoma kwa kule juu mbele.
Pia option ya kuuza ilikuwa ndio kipaumbele changu kabla ya wazo hili.
Ngoja tuone tutakapoishia.
 
Back
Top Bottom