INAUZWA Karibu ununue Mchele, Mahindi na mazao mengine kutoka Mbeya

Kukoboa au kusaga vyote ni 1000,
Akikoboa anabaki na pumba anauza,that's why ni 1000

Hiyo ni bei ya mahindi mapya,ya zaman YAPO, bei haipungui 20000/
Ni machache sana
Mapya yamekauka,kias ukidai ya zaman unaweza pewa mapya yaliovunywa mwez wa tatu mwanzon sehemu inaitwa umalila

Debe linaweza toa kilo 17 Hadi 19, inategemea na aina ya muindi, muindi wenye punje ndogo una Unga mwingi,

Ukikoboa unaweza pata kilo ,14 Hadi 16, pia aina ya mahindi inahusika
So

Kwa gunia ni wastan wa 17x 6=102 (wastan wa chin)Dona

Na 14x6=84kwa sembe

Karibu
Aisee shukrani sana
 
So sorry, Debe au plastic ni kipimo Cha kilo 20, karibu dada angu
Hapana kaka, nadhani debe moja la mahindi inaweza kuwa zaidi ya kilo 20 au pungufu. Kwa maana itategemeana na density ya mahindi husika. Kwa mfano uzito wa mahindi yanayo limwa Songwe-Mbozi kwa debe moja ni mdogo kuliko yale mahindi ya Malawi mpakani na Isongole-Ileje pia yote kwa yote uzito wa mahindi pia husaidia katika kujua unga utakuwa mwingi kwa kiasi gani. Kwa maana mahindi mepesi huwa yanakoboleka sana katika mashine kuliko yale mazito, na hivyo kilo chache za unga.

Lakini kwa mahindi kutoka mbeya Ogopa mahindi ya ukanda ule wa tukuyu kuanzia Ntokela mpaka karibia na Kyela maana mahindi yao wanayakausha ndani na hivyo kuwa mepesi na ugali huwa mbaya , unaweza hisi haujaiva hata uweke moto kiasi gani. Kuhusu swala la mahindi kukaushia ndani ni kwamba ukanda wa Tukuyu jua ni changamoto sana kuwaka mda wote.

Mahindi mazuri ni kutoka bonde la Usangu- Mbarali, Mbeya vijijini, Mbozi, chunya ( ingawa huwa na contamination na heavy metals sababu ya machimbo), mahindi ya Rukwa na Ya Malawi kupitia mpaka wa Isongole- ileje pia bila kusahau mahindi ya zambia.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi kaka. Mi najuaga maindi mazuri n Yale yenye punje ndogo,ambayo kwa Mbeya mengi naona ni Yale yanatoka mbozi na umalila, ila kwa maelezo Yako umeniongezea ufahamu zaidi
Hapana kaka, nadhani debe moja la mahindi inaweza kuwa zaidi ya kilo 20 au pungufu. Kwa maana itategemeana na density ya mahindi husika. Kwa mfano uzito wa mahindi yanayo limwa Songwe-Mbozi kwa debe moja ni mdogo kuliko yale mahindi ya Malawi mpakani na Isongole-Ileje pia yote kwa yote uzito wa mahindi pia husaidia katika kujua unga utakuwa mwingi kwa kiasi gani. Kwa maana mahindi mepesi huwa yanakoboleka sana katika mashine kuliko yale mazito, na hivyo kilo chache za unga.

Lakini kwa mahindi kutoka mbeya Ogopa mahindi ya ukanda ule wa tukuyu kuanzia Ntokela mpaka karibia na Kyela maana mahindi yao wanayakausha ndani na hivyo kuwa mepesi na ugali huwa mbaya , unaweza hisi haujaiva hata uweke moto kiasi gani. Kuhusu swala la mahindi kukaushia ndani ni kwamba ukanda wa Tukuyu jua ni changamoto sana kuwaka mda wote.

Mahindi mazuri ni kutoka bonde la Usangu- Mbarali, Mbeya vijijini, Mbozi, chunya ( ingawa huwa na contamination na heavy metals sababu ya machimbo), mahindi ya Rukwa na Ya Malawi kupitia mpaka wa Isongole- ileje pia bila kusahau mahindi ya zambia.
 
Kwa haraka haraka bei plus ya udalali plus nauli .ni bora nka nunua eneo niliopo tu teh teh
 
Umenyooka vizuri sana kimaelezo hadi nimekuelewa mkuu. MUNGU akubariki.
 
Mtumie pesa ya gunia 10 za mchele ndiyo utaujua uaminifu yake.
Nabeba maumivu ya watu kwa kufikiria ikiwa nitawafanyia Tabia mbaya, shortly, msingi wa maisha yangu ni "Sheria ya dhahabu"...karibu kiongozi,
 
Kwa haraka haraka bei plus ya udalali plus nauli .ni bora nka nunua eneo niliopo tu teh teh
Sijaandika tangazo kwa ajiri ya sehemu zote rafiki yangu,,,,,
Nimeandika kwa ajiri ya wateja,unaweza usiwe mteja Leo kwa sababu uko sehemu fulan, ila kesho ukawa mteja kwa sababu uko maeneo ambayo nimetarget, nitakukaribisha pia , Tena kwa upendo
 
Pia,. Sijaweka mabadiliko ya bei Muda Sasa sababu bei haipo stable ,sababu kuu ni mipaka kutokufungwa, so Mazao mengi bei imebakia vilevile na mengine kama Mchele kupanda zaidi,,,,mpunga shambani kwa Sasa ni sh elfu themanini mpaka Laki na Bado haupatikani, maindi Debe kumi na nne, mjini ,shamba kumi na Moja Hadi kumi mia Tano kwa Debe, ,,,,kwa hiyo inawezekana mwaka huu mwezi wa kumi na mbili vyakura vikawa bei zaidi ya mwaka Jana. Kama una sehemu unaweza nunua Sasa hivi,nunua utunze, mfano mpunga,maindi na maharage,

Tuko pamoja
 
Kwenye mpunga ni Bora ukajua sampling wakati wa kununua. Kwa maana bei ya Michele huathiriwa zaidi na rangi ya Mchele, na unyoofu wa punje ya Mchele.

Lakini kama unajumua mpunga Kwa ajili ya kukoboa zingatia sampling ya mpunga. Kwa maana unaweza nunua mpunga Kwa mkulima lakini hajaupepemua vizuri au ilikuwa haujakomaa vizuri, aisee utapigwa kwenye kwenye kukoboa maana mchele utatota na kilo pungufu kuliko wastani. Hapa namaanisha hivi Kwa wastani gunia la debe 6 inatakiwa ukilikoboa update kilo 60 za Mchele, lakini unaweza kukuta unapata labda kilo 55 au 50 kabisa ambayo ni hasara Kwa biashara.

Pia Kuna baadhi ya wakulima Huchelewesha kuanika mpunga kutokana na sababu kadha wa kadha kama vile kukosa eneo la kuanika kutokana na maji au upatikanaji wa maturubai ya kuanikia. Hivyo mpunga huvundiana kwenye mifuko na kutengeza biriani kwenye Mchele (hii ni wanaovunia combaini lisilo na mtungi).

Pia Kuna ambao huvuna lakini mpunga huchangamana na matope ya shambani na kutengeza vidoa vyeusi kwenye mchele, ambayo moja Kwa moja huathiri bei ya Mchele sokoni.

Pia Kuna aina ya mpunga Huwa na nyufa sana ambao husababishwa kuwa mpunga unakua umefikia muda wa kuvunwa na haukuvunwa Kwa wakati na pia katika shamba maji yalikuwa yakusuasua ( mpunga na maji ni pacha , ni kama samaki). Ukipata mpunga wa hivi hesabia hasara iliyokuu maana utapata chenga sio za nchi hii.

Hivyo basi katika biashara ya kununua zao la mpunga ni vyema ukamtafuta mwenyeji ambaye anaweza kutafuta mpunga mzuri Kwa kuangalia sampuli ili usije ukala hasara kuu.

Mkuu samahani Kwa kukuingilia nilikuwa natoa hoja dhaifu kidogo kuhusiana na hii mambo ya kununua mpunga.
 
Sahihi bro
 
Tunaomba updates za hali ya bei ya sasa kwa mazao ya mchele, maharage na mahindi kwakuwa wakulima wa kanda hii wameanza kuvuna.

Sent from my SM-M515F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom