Kwenye mpunga ni Bora ukajua sampling wakati wa kununua. Kwa maana bei ya Michele huathiriwa zaidi na rangi ya Mchele, na unyoofu wa punje ya Mchele.
Lakini kama unajumua mpunga Kwa ajili ya kukoboa zingatia sampling ya mpunga. Kwa maana unaweza nunua mpunga Kwa mkulima lakini hajaupepemua vizuri au ilikuwa haujakomaa vizuri, aisee utapigwa kwenye kwenye kukoboa maana mchele utatota na kilo pungufu kuliko wastani. Hapa namaanisha hivi Kwa wastani gunia la debe 6 inatakiwa ukilikoboa update kilo 60 za Mchele, lakini unaweza kukuta unapata labda kilo 55 au 50 kabisa ambayo ni hasara Kwa biashara.
Pia Kuna baadhi ya wakulima Huchelewesha kuanika mpunga kutokana na sababu kadha wa kadha kama vile kukosa eneo la kuanika kutokana na maji au upatikanaji wa maturubai ya kuanikia. Hivyo mpunga huvundiana kwenye mifuko na kutengeza biriani kwenye Mchele (hii ni wanaovunia combaini lisilo na mtungi).
Pia Kuna ambao huvuna lakini mpunga huchangamana na matope ya shambani na kutengeza vidoa vyeusi kwenye mchele, ambayo moja Kwa moja huathiri bei ya Mchele sokoni.
Pia Kuna aina ya mpunga Huwa na nyufa sana ambao husababishwa kuwa mpunga unakua umefikia muda wa kuvunwa na haukuvunwa Kwa wakati na pia katika shamba maji yalikuwa yakusuasua ( mpunga na maji ni pacha , ni kama samaki). Ukipata mpunga wa hivi hesabia hasara iliyokuu maana utapata chenga sio za nchi hii.
Hivyo basi katika biashara ya kununua zao la mpunga ni vyema ukamtafuta mwenyeji ambaye anaweza kutafuta mpunga mzuri Kwa kuangalia sampuli ili usije ukala hasara kuu.
Mkuu samahani Kwa kukuingilia nilikuwa natoa hoja dhaifu kidogo kuhusiana na hii mambo ya kununua mpunga.