Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Tunaelekea kwenye uchaguzi wa 2025, na ghafla tunaanza kusikia ofa za ufadhili wa Simba na Yanga, wakati timu za ligi kuu zipo nyingi. Kwa nini?
Tatizo sisi Watanzania huwa tunaghiribiwa kirahisi sana. Tuliwahi kuuza nchi na watu wetu huko nyuma kwa zawadi za shanga na vioo vya kujitazamia kutoka kwa Waarabu. Haka katabia kabaya bado tunako. Hatuangalii mbali, hassa pese inapotembezwa. Sasa nawaonya Watanzania wenzangu, tuwe macho, kwamba hizi mbinu za kusema tunafadhili au tutawatafutia ufadhili wa timu ambazo wengi wenu mna ushabiki nazo isije ikawa ni kwa ajili ya kuwalainisha kutoa kura zenu 2025.
Kumbukeni kwamba, nikigombea uraisi, na 60% ya wanachama na mashabiki wa Simba na Yanga wakanipigia kura, napita kuwa raisi kiulaini sana!
Kuleni fedha za ufadhili watakazowaletea, lakini pigeni kura kuchagua watu wanaotufaa sio kwa sababu ya shukurani kwa ufadhili wa timu yako!
Pia soma:Uzi Maalum wa Kauli tata na za kushangaza kutoka kwa Viongozi na Wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025