Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
CCM ina miaka 47 ni vigumu sana kwa kizazi cha walio hai sasa kutokuwa na ushawishi au mahusiano na hiki chama.Hapo ndipo tunapoachana Mkuu - kwamba siku zote tunafanya mambo ili kufaidika. Mtu anachaguliwa kuwa waziri na tunatarajia afaidike. Unaamua kuchagua upande fulani ili ufaidike. Kwa nini hatufanyi mambo ili Tanzania ifaidike?
Mie ningekuwa raisi wa Tanzania, ningewakuza sana watu wa upinzani ili nchi ifaidike. Ningehakikisha nawajengea uwezo hadi wawe washindani halisi wa CCM, ili kuwe na ushindani wa kweli na chama kinachotawala watambue kwamba wakifanya uzembe wataondoka, kama ilivyo UK au USA. Na ningewaamsha watu wafikie mahali wasikipigie kura chama kwa sababu tu wao ni wanachama wa chama hicho. Ningewajengea falsafa kwamba unaweza kuwa CCM ukakipigia Chadema, au ukawa Chadema ukaipigia CCM. Tukifika hapo Tanzania itaendelea kwa kasi sana, tunawaeza hata kuwazidi South Africa, Nigeria na Egypt kwa kuwa na uchumi ulio na nguvu, biggest economy in Africa.
Naikitika sana hakuna mtu atakaetokea kuwa raisi atakuwa na mawazo kama yangu, na mie sina mpango wa kuingia kwenye huo wendawazimu wa siasa za Tanzania zinazotaka lazima uwe na roho mbaya
Huyo Msigwa aliyekuwa hatari sana huko CHADEMA alitoka upinzani akaja CCM na kupokelewa katika mkutano mmojawapo kule Dodoma. Na wengi tu hufanya hivyo.