Pre GE2025 Karibu Watanzania wote wana asili na ushabiki wa Simba au Yanga; basi angalieni ofa za ufadhili wa timu zenu isiwe kampeni ya uchaguzi mkuu 2025!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM ina miaka 47 ni vigumu sana kwa kizazi cha walio hai sasa kutokuwa na ushawishi au mahusiano na hiki chama.
Huyo Msigwa aliyekuwa hatari sana huko CHADEMA alitoka upinzani akaja CCM na kupokelewa katika mkutano mmojawapo kule Dodoma. Na wengi tu hufanya hivyo.
 
Huwezi kuelewa. Hizi ni topics zinahitaji akili kubwa kuzi discuss.
Hakuna akili yoyote kubwa siasa za nchi hii ndivyo zilivyo na huwezi kufanya lolote lile kuzibadili.

Kubali uishi kama jamii inavyoishi au toka nje nenda kaishi huko Kenya au Somalia.
 
Kuna siku wataondoka tu, kwa namna moja au nyingine. Walikuwepo KANU Kenya, UNIP Zambia, UPC Uganda, wako wapi? Inahitaji tukio moja tu watu kuamua, kuna siku itatokea
Ni ngumu polisi, tume fake ya uchaguzi, mahakama, TISS na jeshi vyote ni matawi ya CCM
 
Hakuna akili yoyote kubwa siasa za nchi hii ndivyo zilivyo na huwezi kufanya lolote lile kuzibadili.

Kubali uishi kama jamii inavyoishi au toka nje nenda kaishi huko Kenya au Somalia.
Kwa hiyo Tanzania ni taifa la watu waliokata tamaa?
 
Kuna mwandishi maarufu alisema tatizo la Africa ni kwamba ni bara pekee duniani ambalo wezi wanashangiliwa na wale wanaoibiwa!
 
Hakuna mahali nimesema si sawa wanachama wa Simba na Yanga kuwa na uanachama wa vyama vya siasa. Elewa mada Mkuu
 
Kwa hiyo Tanzania ni taifa la watu waliokata tamaa?
Kuzipenda Simba na Yanga na kuupenda mpira sio kukata tamaa, achana na haya mawazo hasi yanayojaa chuki, hasira na roho mbaya.

Kuna watanzania wenzetu wengi tu wenye kufaidika na kukua kwa hizi timu. Ni walipa kodi wenzetu hivyo dunia uliyonayo kichwani mwako sio halisia.
 
Hakuna mahali nimesema si sawa wanachama wa Simba na Yanga kuwa na uanachama wa vyama vya siasa. Elewa mada Mkuu
Yanga na Simba kuwa hivi zilivyo hakuna tunachoweza kufanya kuibadilisha hali. CCM imezaliwa kutoka kwa TANU na ASP ambavyo ni vyama vyenye uhusiano wa moja kwa moja na mpira wa Tanzania.

Laumu historia yetu vinginevyo unapaka rangi upepo.
 
tatizo ni upinzani wanajitenga na fursa nyingi za siasa.
kama akuna kosa kisheria sawa tu kwani mbaya nini!
 
Inashangaza mpaka leo hujui kuwa Simba na Yanga ndio siasa ya Tanzania. Pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…