supatolu
Senior Member
- Aug 7, 2022
- 140
- 189
Nilienda pale Villa Park, nikaagiza niletewe lunch. Daaah, nikaletewa bonge la samaki sato (mzima mzima) wa kuchoma na dona, na mazagazaga mengine kibao. Sasa ukitaka kuujua utamu wa sato, anza kula kichwa, halafu ndio unashuka chini. Jamani sato ni mtamu, mimi sio mlaji wa ugali, lakini siku hiyo nilimaliza ugali wote! Sasa baada ya kumaliza, nikajua inakuja bonge la bili, nikawa na wasiwasi! Inakuja bili, kumbe ni shs 12000/= tu, nikalipa, then nikasepa na kwenda kiwanja cha Bundesliga (maeneo ya Buzuruga). Nakumbuka nilienjoy sana kwa wiki mbili nilizokaa Mwanza. Mwanza patamu!
Hujaongelea swala la mazeze, au hukukurupusha zeze hata angalau?