Karibuni tupambane huku Malmö, Sweden. Malipo si mabaya

Karibuni tupambane huku Malmö, Sweden. Malipo si mabaya

Pako vizuri sana , sisi wengine tuliobahatika kupita njia hiyo tukielekea kuunganisha kwenda Denmark tunafahamu maisha ni mazuri lakini pia ujira sio mbaya, Kuna kamji kadogo down south kanaitwa Kalmar nilikaa huko kuna watu weusi wachache sana na hakuna ubaguzi tatizo connection ya kufika huko na kwa kipindi hiki cha Corona ndio balaa kabisa , kwa vijana wa bongo wanaotafuta future hivyo vimiji vidogo ndio mpango mzima lakini siyo stokholm
 
Safi mwana share vijana waangalie fursa. Lakini na shauri usikimbilie nje ukiwa hauna kitu mfukoni
Wiki iliyopita nilileta habari ya kutoka Norway na kuja Malmo kwenye kazi. Wapo waliofurahi na kuniombea heri na wapo ambao walikasirika na kunitukana. Yote sawa.

Nipo huku kwa kazi kama zile nazofanya Norway, vibarua vya bandarini. Nilipewa huu mchongo, faster tu wala sikutaka kujiuliza mara mbilimbili kwa kuwa kusafiri hivi ni mwanzo wa pia kuongeza uwezo wangu. Ila baada ya wiki kazi ikiisha narudi tena home Norway kupiga mzigo.

Malmo ni pazuri sana sijui hata nielezaje, wenzetu kweli wanafanya kazi kujenga nchi zao, Ila naona kama hii corona inawapa kikwazi sana.

Wenzetu ni kweli hawakuwa wavivu, sijui ni lini bongo tunaweza kuja kuwa hivi.

Mtaa niliofikia ni ngumu kumkuta mtu kizembezembe barabarani au kakaa nje ya nyumba yake.

Haya ndio maisha niliyokuwa nayapenda, watu wanapaswa kuishi bila kufatiliana wala kujuajuana sana.

Kwa hakika huu ni mji mzuri sana, japo bado mgeni ila nimepapenda sana, Africans pia wapo wengi tu hasahasa niliowatambua ni Nigerians, sema ndio hivyo huwa sipendi shobo nao kila mtu afate kilichompeleka.

Hata huku mambo sio mabaya kwenye malipo, na pia kazi zipo sana tu ila ni zile za unskilled.

Chini kuna picha ya nyumba-camp napoishi na mtaa ambao nilipo. Nyumba ni ya ku-share nilivyofika niliambiwa kabisa kuwa Kuna sehemu ya kulala hivyo kuhusu kodi hainihusu kabisa na hivyo sijui kabisa gharama yake kukaa kwa siku au mwezi.

View attachment 1824663View attachment 1824664
 
Back
Top Bottom