Karipio la Rais Samia: Unaiba hela ya Umma ikusaidie nini? Utazikwa nayo? Utajibu nini Mbele ya Mungu?

Karipio la Rais Samia: Unaiba hela ya Umma ikusaidie nini? Utazikwa nayo? Utajibu nini Mbele ya Mungu?

Akiongea kwa uchungu kufuatia Ripoti ya CAG kuonyesha viongozi wanaiba bila uwoga, Rais Samia amewauliza Wanaiba Fedha za Umma ili ziwasaidie nini? Je, watazikwa nazo? Na siku ya hukumu Mbele ya Mungu wataosema nini?

Hili karipio limenifikirisha sana na kunirejesha kwenye Kitabu kitakatifu Biblia, wala Rushwa ni vipofu na dhambi hiyo itawaenea Wana wao Kizazi hata Kizazi.

Ramadan kareem!

Na wizi wa chama chake kutumia nguvu kuiba kura asiusahau au Mungu Huo hauoni?
 
Ya kaisari mpe kaisari ya Mungu mpe Mungu hiyo. Watu wanaangalia matumbo yao tuuu kwa Mungu atajua huko huko akifika.
 
Alifikiri kujinyenyekeza kwa majizi/mafisadi watamuacha salama kumbe unawafanya wakuone huna lolote na wanakupiga vzr huku wakijitahidi kukupamba kuwa unaupiga mwingi na wewe ni bora kuliko mwendazake mama ukicheka na nyani utavuna mabua shauri yako
 
Hakimu wa haki ni Mungu
Sisi kama walokole tunasimama na kauli ya Mama.
Mungu atahukumu na watakufa wataziacha mali.
Mtu akikudhulumu ht usipambane ili kurudisha haki yako, ww tulia tuu ukimuachia Mungu ili lile neno la kuangamia kwa kukosa maarifa litimie
 
wezi wamevunja kanuni zilizowekwa ndo maana wanaiba na hakuna kitu kibaya kinawatokea, endelea kusema hukumu ya Mungu wakati watu walishavuka mstari hawana cha kuogopa na wanapiga kweli kweli.
Wamegeuza Katiba...maandishi yameangalia chini.Wanapiga tu bila kuangalia
 
Tukaze roho tupitishe sheria ya kifo kwa mtu yeyote ambaye atabainika kuhujumu uchumi kwa makusudi na kutoa rushwa.

Mtaona kama huu upuuzi utaendelea.
 
Mkuu Sheria ya kunyonga si bado ipo hai? Hebu tundika wawili watatu hv tukuelewe🤣🤣
 
Kama majitu malevi, mazinzi, matapeli unafikiria hata huyo Mungu wanamjua[emoji23][emoji23] wacha wapige mambo mengine bila ya imani ya kando huwezi kuzuia. Wewe unasema Mungu atahukumu je yeye anaamini hilo.

Ebu tufanyeni tathmini kwa nn China wanakuwa na hofu sana katika uwizi haswa viongozi wa umma ..wanachukuliwa utumishi ni kama devoted service na sio kimaslahi zaidi na pia uzalendo wanafundishwa tangu watoto.
Na ukiiba au ukila rushwa, sheria ni wanakutwanga risasi. Unafikiri wachina wamefikaje hapo? Hakuna mzaha kwenye mali ya umma. Wamagharibi wakawaita kila majina, ooh madikteta, waminyaji haki, waliziba masikio. Leo JPM ataendelea kukumbukwa.
 
Wawajibike na iwe fundisho kwa wengine. Mali zao zote zichunguzwe.
Ndo mambo aliyokuwa akipambana nayo Magu, baadhi ya viongozi waliozoea upigaji na wafanyabiashara wakamuona mbaya. Hii nchi kuna asilimia kiasi fulani ya biashara zinaenda kwa kulipa kodi kiujanja ujanja na udanganyifu. Malipo ya serikali ndo bei zinaongezwa sana bila kusahau wizi wa mali za chama. Ilibidi tu JPM aondoke. Leo hii kuna watu wanathubutu kusema "chama kimerudi kwa wenyewe" "msile sana" inafikirisha, sijui ili watu waendelee "kufanya walivyozoea" Kwamba yule msukuma alikuja "kuziba rizki zetu" Haya ndiyo matokeo, mengi yatajitokeza, bado sana
 
Akiongea kwa uchungu kufuatia Ripoti ya CAG kuonyesha viongozi wanaiba bila uwoga, Rais Samia amewauliza Wanaiba Fedha za Umma ili ziwasaidie nini? Je, watazikwa nazo? Na siku ya hukumu Mbele ya Mungu wataosema nini?

Hili karipio limenifikirisha sana na kunirejesha kwenye Kitabu kitakatifu Biblia, wala Rushwa ni vipofu na dhambi hiyo itawaenea Wana wao Kizazi hata Kizazi.

Ramadan kareem!
Maza anatuangusha sn hafai yaani aibu kuwa na mkuu wa nchi wa namna hii naameapa kulinda katiba ya nchi maanake ni maslahi ya kwa mali za umma, kama hawezi kulinda mali za umma hatufai hata kdg
 
Back
Top Bottom