KARMA - Kidamali: Wewe Mwenyewe Ndiye

KARMA - Kidamali: Wewe Mwenyewe Ndiye

Je, bado nina haki ya kumchukia mama Maila ama niwe mpole kama mfalme Daudi?

  • Una haki ya kumchukia (we all have a past lakini alichokifanya sicho)

  • Unavuna ulichopanda (It's Karma!)

  • Nipo katikati (Matukio hayana uhusiano kwangu; so reaction zote mbili naziona justified)

  • Sijui (bado sijaamini kilichotokea, nimeshindwa kutafakari, ...)


Results are only viewable after voting.
Karma ndo kitu gani? Anyone?
Tumia hiyo definition ya urban dictionary hapo...ni rahisi kuelewa zaidi.
Screenshot_2018-04-10-23-21-01.jpg
 
Hah hah kile kisa ni noma

Hivi nikiwa Lindi si ndo yule jamaa mchimba chumvi aliniloga?

Ila mkuu tangu kipindi kile sijawahi kutembea na mke watu tena! Nilikoma...

Tafadhali mpendwa, sema neno zaidi nami nitapona...
Nimemaliza kusoma sasa, nilihitaji kusoma nikiwa nimetulia, mimi ni shabiki yako baada ya kuona uzi wako nikafungua nicoment wa kwanza hahaha
Hahah I am humbled mkuu!

Natumai umejifunza jambo hapo...
 
Tafadhali mpendwa, sema neno zaidi nami nitapona...

Pole sana mpendwa.
Pia asanteh sana kwa somo maana nimejifunza na kupata woga wa kutendea wengine mabaya kwasababu huwezi kujua wakati sahihi wa kukurudia hayo mabaya.

Tuishi kwa hofu, tupendane tuthaminiane na kutendeana mema siku zote za duniani, malipo ni hapa hapa.
 
Hivi nikiwa Lindi si ndo yule jamaa mchimba chumvi aliniloga?

Ila mkuu tangu kipindi kile sijawahi kutembea na mke watu tena! Nilikoma...


Tafadhali mpendwa, sema neno zaidi nami nitapona...
Hahah I am humbled mkuu!

Natumai umejifunza jambo hapo...
Mentor, you are a real Mentor of mine, nina mengi ya kujifunza kutoka kwako
 
thank you for asking. I meant the whole karma thing. it doesn't work. it's a no no.

Mkuu, huenda kutumia neno KARMA kunakuudhi...

Naomba usome maelezo niliyoyatoa. Sijawahi kuandika kisa/mkasa na kuutolea maelezo ya kwa nini nimekiandika lakini kwa hili imenibidi niandike.

Kwa mara ya kwanza naomba niandike maelezo ya ziada;

- Kisa hiki ni kisa cha ukweli kabisa (wahusika wamebadilishwa kuficha uhalisia)

- hata mimi mwandishi bado nipo kwenye dilemma ya kujua nani hasa ahukumiwe (au ahukumiwe zaidi) na ndiyo maana nikafikiria kuweka poll hapo juu.

Zaidi sana, ni lengo la mimi kuelezea mkasa huu;

- HUKUMU: Kabla hujamchukia na kumhukumu mtu kwa alilokufanyia, jichunguze kama hukuwahi kufanya kama yeye. Haimaanishi kwa kila kosa basi tunastahili adhabu lakini itatufanya kuwa wapole wakati mwingine tunapofikiria kumuumiza mtu mwingine. Mara nyingi, hasa kwenye mahusiano (na hii imenikuta hivi karibuni) unamchukia mtu kwa kosa alilokufanyia. Unamtukana na kutumia maneno makali kuwa hakukupenda ndiyo maana akakufanyia A, B, C. lakini ukikaa kidogo ukafikiria 2012 huko Kidamali, utagundua nawe uliwahi kumfanyia mwingine sawa (au zaidi) ya yale uliyofanyiwa. Ila kwa kuwa sasa kibao kimegeuka kwako, huuoni uovu wako ila wa yule aliyekutenda sasa. BIN ADAMU!

- HISTORIA: Uliyoyafanya kwa kificho, yatadhihirishwa mwangani siku moja. Mara nyingi tunafanya mambo kwa kuamini hayatakuja kutuumbua mbeleni. Kuna nyakati tunafanikiwa. Lakini, amin nakuambia, ipo siku uovu unaoufanya ukijua ni uovu utakuja kuku-haunt.

- NAFASI: Unayo nafasi ya kurekebisha na kuanza upya. Zaidi sana, unayo nafasi sasa ya kutafakari na kuishi sawa. Mfalme Daudi kwenye aya niliyoandika, alijuta na kutubu (kwa bahati mbaya kwake dhambi yake ilisababisha kifo/vifo) lakini alirejeshewa baraka zake. Alirekebisha mwenendo wake na Mungu akamrejeshea ufalme wake. Kwa kiingereza kuna mahali imeandikwa, "God considered him, a man after God's own heart." Inawezekana kurekebisha, inawezekana kuanza upya kwa usahihi na inawezekana kutafakari sasa na kuepuka kufikia kwa Daudi na Mentor.

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

Kama huamini hiyo philosophy ya KARMA basi labda unaifahamu ile GOLDEN RULE; usimtendee mtu usilotaka kutendewa.

Ni kweli kabisa kuwa huenda yaliyonipata hayahusiani na uovu nilioutenda (maana pia kiuhalisia nimetenda mwingi zaidi ya niliyoyaandika). Lakini kuna ile dhana ya kumkasirikia mtu kwa kukutendea jambo ambalo wewe mwenyewe ukitafakari utakumbuka ulishamtendea mwingine sawa au zaidi ya hilo. Basi kwa hilo, point ya kuchukua ni kutokukasirika yanapokukuta, KARMA or no KARMA.

Lakini pia, ni mkasa ambao unatoa funzo la kutafakari sasa (NOW) yapi tunayotenda kwa watu na kujiuliza tukitendewa hayo tutafurahi? Nadhani tukienenda kwa kujiuliza hivyo ni mara chache tutaruhusu udhaifu wetu wa kibinadamu (au nia ovu) kuathiri maisha ya wengine.

Naamini wenye dini na wasio na dini wote tunakubaliana na the golden rule. Basi tusitumie kutokukubaliana nami kutumia neno KARMA kisha ukasahau somo zima la mkasa huu. Tukubaliane kuwa tujitahidi kuwatendea wengine kama ambavyo tungependa kutendewa sisi. Haiondoi maumivu ikitokea umetendwa vibaya lakini itakusaidia kupona haraka unapojua hukumtendea mwingine uovu kama huo. Lakini zaidi ni, kila mmoja wetu akijitahidi kuishi hivyo, we can make our lives here on earth 'little paradise'.


Cheers!
 
Back
Top Bottom