Karolina leavit Tumeongeza ushuru kwa uchina kutoka 125% hadi 145%

Karolina leavit Tumeongeza ushuru kwa uchina kutoka 125% hadi 145%

Huu mpambano utafika hatua inayofanana kabisa na total ban; hapo ndio mlio utakuwa mkali watarudi mezani kuzingumza
 
Eti wezi wa technology km rahisi kuiba technology mbona nyinyi mnashindwa kuiba hyo technology hzo tarrif anazoweka usa hata hazitomsaidia kurudisha viwanda ndani ya usa ndio kwanza iphone wanataka kuhama china wahamie india
Kwa elimu ipi, hii ya VETA ama hii ya kukaririshana madesa ya COET, DIT n.k....Pole sana!
 
Hivi kati ya China yenye watu 1.4 b.
Na Marekani yenye watu 340 m.
Ni soko gani hasa la kuvutia wazalishaji?
Soko lolote linategemea watu.
Nadhani China ijikite zaidi barani Afrika yenye watu 1.5 b na ijipanue zaidi kwenye bara lake lenye watu 4.9 b kuepukana na masoko yenye utata kama Marekani.
Hahaha tatizo siyo idadi ya watu, hapa swala ni soko linalolipa. Hao wachina Bilioni 1.4 sio wote wanauwezo kununua bidhaa zao humo ndani, na kumbuka kuna bidhaa zinatengenezwa china lakini haziuzwi China kabisa.

Halafu sisi Afrika hatuna uwezo kumudu kununua hizo bidhaa, tuko wengi lakini Masikini haswa, na ahatuna pesa za kuweza kuwa soko la bidhaa, sisi ni soko la Taka taka, unaona tuna nunua mabakuli ya Plastic, na vijiko vya plastic hatuwezi kununua Gari za umeme.

Unaongelea Afrika soko la Kanga, na Vitenge wao wanaongelea bidhaa zenye akili na pesa za maana.
we unaona tunaletewa uchafu na wachina unaita biashara?
 
Asilimia ngapi ya bidhaa za China zinazouzwa nje zinategemea soko la Marekani?
 
Watoto wa kichina wanafundishwa kwa vitendo wakiwa shule
Watajifunza mambo mengi sana kwa vitendo.

Tatizo letu sisi hata viwanja vya michezo vimeuzwa.

Nchi ambazo zimegoma kujiendeleza na sisi tumo.

Ukiwaweka vijana wa vyuo vikuu kwenye general knowledge tu, nina uhakika wengi watafeli kwa mambo ya kawaida sana

Hatuna faida na dunia hii bora hata mchwa
CCM
 
Asilimia ngapi ya bidhaa za China zinazouzwa nje zinategemea soko la Marekani?
Unachanganya mambo, kuna bidhaa zinatengenezwa China kwa ajili ya Marekani na nchi za Ulaya tu, na kuna hayo mabakuli ya plastic, na vikombe vya udongo na nguo za hovyo hovyo ndio zinakuja Afrika.

Afrika siyo Soko, ndio maana huoni wakiiongelea kabisa, sisi ni sioko la uchafu. Used phones, refurbished stuff na vitu visivyo na maana kama kanga, mashuka, hivyo.

sasa wakuongelee unanunua nini cha maana.
 
Kwenye hilo swali ni wapi nimekutajia Afrika?
Huoni kuwa wewe ndiye unaye jichanganya!!
China ana soko la bidhaa zake Duniani kote, swali " Katika mapato ya bidhaa zake zote anazouza nje, ni asilimia ngapi anapata kwa mauzo ya Marekani"?
Tafadhali sipo kwenye ushabiki, twende tuelimishane.
Tunataka tuone akilipoteza soko hilo atapungukiwa nini?
 
Kuna bidhaa hazihitaji wingi wa watu bali uwezo wa watu wa kununua.

Mfano, uzalishaji mali wa Afrika yote kwa mwaka 2024 ulikuwa around $2.8T -3.4T wakati USA pekee alizalisha $29.7T .

Pia inakadiriwa kwa mwaka huo 2024 China ilipata around $580B kwa kufanya biashara na USA huku USA akipata $140B akifanya biashara na China kwa mwaka.

China alifanya biashara na Afrika yenye wakazi zaidi ya 1+B isiyofika $300B

Kwa uchache unaona soko bora liko USA kidogo na Ulaya kuliko maeneo mengine
Je hudhani kuwa wakulima wa Marekani bado wana uhitaji wa soko la uhakika kuuza bidhaa zao kama Maharage na Soya kwa soko la China, ambalo pamoja na mambo mengine mwaka uliopita wameuza $140b kama ulivyoanisha hapo juu?
 
Uhitaji upo ila anayepata zaidi ya $580B ana uhitaji zaidi ya huyo anayepata $140B.
 
Back
Top Bottom