Wanabodi,
Wakati sintofahamu kuhusu Hati Halisi za Muungano, ikiendelea, nawaomba Watanzania wenzangu tufike mahali tuambiane ukweli halisi kuwa
Hati Halisi za Muungano", hazipo popote!, nakala iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, yenye saini ya Nyerere na Pius Msekwa!, ile sio hati ya muungano (Articles of The Union" bali ile ni Sheria ya Muungano!, "The Act Of Union!" iliyotungwa na Bunge la Tanganyika, ku ratify the "Artcles of Union", ambayo imesainiwa na Nyerere, Speker wa Bunge na Msekwa kama Katibu wa Bunge wa Wakati Huo!.
Msekwa was never a signatory kwenye Artcles of The Union!".
Signatories kwenye "Artcles of The Union" ni
- Mwalimu Julius Nyerere-Rais wa Jamhuri ya Tanganyika
- Sheikh Abedi Amani Karume- Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
- Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika -Fifthfoot
- Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar (Wolfgang Dourado-Alipewa likizo ya lazima nje ya nchi, Akaletwa mwanasheria wa Ghana kuusimamia muungano, ukasainiwa na Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika pekee!)
Hati Hizi hazipo Idara ya Nyaraka na kumbukumbu za Taifa Nimezungumza na Mtanzania wa Kwanza kuwa mkuu wa Idara ya Kumbukumbu, Mzee Mongela, hakuwahi kuziona hati hizo wala hata copy yake!.
Nikazungumza na Mkurugenzi wa Nyaraka aliyepita Bwana Mlyansi, pia amekiri kutoziona hati hizi!. Nikazungumza na Mkurugenzi wa Nyaraka aliyeko sasa Bw. Magai!, hati hizo hazipo!.
Ule uongo wa kuwa eti hati ziko UN, nimewahi kuzifuatilia mpaka huko UN hati hizo hazipo!.
Kipindi hiki cha Bunge Maalum sasa ndicho kipindi muafaka tuelezane ukweli bayana kuwa hati hizo are no where to be seen!, tuelezwe vizuri tuu kuwa kwa bahati mbaya zililiwa na mchwa hivyo zimetoweka zote kwa pamoja!.
- Nakala halisi ya Serikali ya Tanganyika, imetoweka!
- Nakala halisi ya SMZ, imetoweka!
- Nakala halisi ya Bunge la Tanganyika-imetoweka!
- Nakala halisi ya BLW nayo imetoweka!
- Nakala halisi ya Mwanasheria Mkuu -imetoweka!.
- Nakala halisi ya Nyerere-imetoweka
- Nakala halisi ya Karume -imetoweka!
Hili suala la hati halisi za Muungano nimelizungumza
Hapa-
Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu?!
Na Hapa-
Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu?!.
Na Hapa-
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?!.
Na Hapa-
Jee Wajua Kuwa Kuna Uwezekano Tanzania Sii Nchi Halali Kisheria?!.
Kwa kuanzia jee Nakala Halisi za Muungano ziko wapi?.
Pasco