Kaseja atua yanga kwa milioni 40

Kaseja atua yanga kwa milioni 40

Mtasema yote lakini hakuna kama Kaseja

Ni kweli Kaseja bado mzuri, tatizo lake ni kuwa hana mapenzi na Yanga. Kama ni kuwakomoa Simba wasimpate hapo tumewawahi. Kwa ujumla sijapenda huyu jamaa kusajiliwa Yanga.
 
Yanga nia yao si mashindano ya kimataifa tu bali pia wamewahi SIMBA ili wasimpate.

Simba wasimpate vipi wakati wao ndio walimtema na kasota mzunguko wa kwanza bila timu?
Unazi ukizidi unaleta upofu.
 
Yanga wanasajili bila mipango ili kuikomoa Simba, hebu soma hii

Yanga: Tulimsajili Kondo wa Simba usiku

KAMATI ya Usajili ya Klabu ya Yanga, imekamilisha maumivu mengine kwa watani wao Simba, baada ya kumalizana na straika aliyekuwa njiani kutua kwa Wekundu hao, Shaban Kondo, lakini bosi mmoja wa Yanga anasema Simba walizembea.
Awali, Kondo alitua Simba siku chache tangu timu hiyo ilipoanza mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi lakini mabosi wa Msimbazi walichelewa kumpa mkataba na Yanga wakatumia mwanya huo.
Taarifa ambayo Championi Jumatano limethibitishiwa, imesema Kondo alitekwa na viongozi wa Yanga usiku akiwa matembezini na kupewa mkataba.
Kondo ambaye aliwahi kutua nchini Msumbiji alikokwenda kusaka timu, alikuwa tayari ameshakaribia kulamba mamilioni ya Simba, lakini Yanga wakashtuka haraka na kufanya utemi huo.
"Unajua kuna siku nilikuwa nazungumza na rafiki yangu mmoja akaniambia Mwalami (Mohamed) anasema kuna straika mmoja kinda amekuja hapa nchini akitokea nchini Msumbiji.
"Alimsifu kuwa ni hatari sana, tukawatuma watu wetu wakatuambia ni kweli yupo Simba anajaribiwa, tukaanza kumsaka taratibu," alisema bosi mmoja aliye katika Kamati ya Usajili ya Yanga huku akiongeza kwa kusema:
"Tulipata nafasi ya kuonana naye usiku tukabaini kwamba bado hajamalizana na Simba, hilo alituthibitishia yeye mwenyewe na tulipompa ofa yetu akaikubali tukamsainisha. Ni mchezaji mzuri, utamuona siku yoyote kuanzia kesho (jana)," alisema bosi huyo.

NB: Huyo mchezaji hajawahi kupangwa hata katika mechi moja ya ligi tangu 'asajiliwe usiku'
 
Na utafiti wa kinyuma nyuma(wewe si umefanya wa kichini chini,wenzio wamefanya mwingine) uliofanyika imebaini kuwa Kaseja anakukula 0713...,na mkeo naye pia anagongwa na Kaseja!
Watu wengine mnakera,samahani sana mods hapa penyewe nimejitahidi kupunguza ukali wa maneno!

Ha Ha Ha Ha Ha Ha Usijali, tumekusamehe.
 
Napenda kuwapongeza sana viongozi wetu wa yanga kwa kuangalia mbele na hasa ligi ya mabingwa, nadhani kama kuna sehemu imepwaya sana ndani ya kikosi chetu linapokuja suala la ligi ya mabingwa ni golini, pia ninashauri pia tusajili beki wa kati mmoja na nimemwona beki wa Liberty professional ya Ghana ambaye ni kapten wao anavaa jezi no:20, huyu angetufaa sana akicheza na Yondani. Nadhani tuna tatizo la kufungwa magoli ambayo hata huwezi elewa yanapitaje nadhani pia tunahitaji kiungo mkabaji mfano wa Jerry Santo na hapo tutakuwa na kikosi imara ambacho naamini tutafika mbali kwenye ligi ya mabingwa. Mwisho naomba kuuliza hali ya mwenyekiti wetu wa baraza la wadhamini mzee Kifukwe je kweli anaugua? Mwenye kujua tafadhali anijulishe.

Ahsante sana, huyu mtu anaeitwa Jerry Santo na Echessa ni hatari sana, sijui ilikuwaje wakatimuliwa Simba.
 
Kweli bongo kila kitu siasa + uchawi wajomba huyu karudi kwa mganga kamwomba msamaha tayari kashautwa yanga
 
Wachezaji wanasajiliwa kutokana na viwango vyao,hatusajili wachezaji wa kucheza na Simba tu.Chuji,Barthez,Yondani na Dida wameonyesha kiwango cha juu walivyotua Yanga kuliko walivyokuwa Simba.
Sana sana Barthez, ameonyesha kiwango cha juu sana, he he heee :biggrin1: :biggrin1::biggrin1:
 
Wamemsajili kama mganga wa timu sio kama golkipa jamani
 
Ni kweli Kaseja bado mzuri, tatizo lake ni kuwa hana mapenzi na Yanga. Kama ni kuwakomoa Simba wasimpate hapo tumewawahi. Kwa ujumla sijapenda huyu jamaa kusajiliwa Yanga.
Mkuu Kaseja hahitaji kuwa na mapenzi na Yanga kwa sababu hajasajiliwa kuja kushangilia, yeye anakuja kufanya kazi na kwa uzoefu wake sidhani kama mapenzi na timu nyingine yataathiri uwezo wake, sanasana mpeni tu ushirikano na muondoe mawazo hasi juu yake.

Hata hivyo mimi nimefurahi Kaseja kupata timu bila kujali ni timu gani, ilikuwa haingii akilini kwa golikipa kama yeye kutokuwa na timu halafu kina Rage wanatumia mamilioni kuleta wageni nafasi ambayo wazawa wengi tu wanaiweza.
 
Ahsante sana, huyu mtu anaeitwa Jerry Santo na Echessa ni hatari sana, sijui ilikuwaje wakatimuliwa Simba.
Mkuu hawa watu hawakufukuzwa Simba, mikataba yao iliisha tena kama Hilary Echesa mkataba wake uliisha zamani sana na Jerry Santo mkataba wake uliisha na hakutaka kuongeza maana alikuwa ameshapa timu nje nadhan Vietnam au Lebanon lakini baadaye akawa amechelewa na kwenda na matokeo yake akajiunga na Coastal united.
 
Ngoja mimi niendelee kuweka kambi Mbeya City Fc,hao wazee wa fitina waache waendelee kuzikana wao kwa wao
 
Kaseja hajawahi kuwa na mapenzi ya dhati na yanga,sasa usajili wake utakuja kuwaumiza mashabiki mnaojifanya mna msimamo
 
Mkuu Kaseja hahitaji kuwa na mapenzi na Yanga kwa sababu hajasajiliwa kuja kushangilia, yeye anakuja kufanya kazi na kwa uzoefu wake sidhani kama mapenzi na timu nyingine yataathiri uwezo wake, sanasana mpeni tu ushirikano na muondoe mawazo hasi juu yake.

Hata hivyo mimi nimefurahi Kaseja kupata timu bila kujali ni timu gani, ilikuwa haingii akilini kwa golikipa kama yeye kutokuwa na timu halafu kina Rage wanatumia mamilioni kuleta wageni nafasi ambayo wazawa wengi tu wanaiweza.

Ntale Masuke, haya ni ya moyoni?
 
Last edited by a moderator:

unamzungumziaje Ngasa,alipokuwa simba,Azam na alivyo hivi sasa Yanga?
 
Ngoja mimi niendelee kuweka kambi Mbeya City Fc,hao wazee wa fitina waache waendelee kuzikana wao kwa wao

Hao MCC pale walipoishia ndiyo mafanikio yao ya juu, hawatazidi hapo zaidi ya kuporomoka. Enzi zake Moro United waliongoza ligi zaidi ya nusu msimu lakini mwisho waliangukia pua. Nafasi haitoshi ningeandika habari za Reli Morogoro, Sigara na Nyota Nyekundu.
 
Ntale Masuke, haya ni ya moyoni?

Sina cha kuogopa kuandika yaliyo moyoni mwangu, Kaseja hakuwa mtu wa kukosa timu na hata kama Simba walionyesha nia ya kumsajili na yeye akaamua kwenda Yanga lazima tuheshimu maamuzi yake na ndo maana jana usiku usiku nilivyosoma hii habari sikusita kuwapongeza Yanga kwa kumsajili na yeye mwenyewe kwa kupata timu na kwa sababu naamini kabisa Juma anajitambua na anajua kazi yake hataleta mambo ya kwamba ooh sijui sina mapenzi na hii timu kwa hiyo nicheze chini ya kiwango.

Mimi nilikuwa namhurumia sana Kaseja kwa jinsi alivyokuwa anafanyiwa na mashabiki wa Simba hasa zile mechi za Mtibwa na Polisi mwaka jana, hata kwenye ile mechi na Yanga mliyoshinda 2-0, mtu anapiga free header halafu lawama anapelekewa Juma.

Tukiacha mambo ya ushabiki na kutumia ubinadamu lazima uone ni jambo la heri kwa mwenzako kupata ajira kwa sababu mimi mwenyewe najua hali anayokuwa nayo mtu asipokuwa na kazi maana mimi mwenyewe ilishawahi kunitokea.

Narudia tena nawapongeza sana Yanga pamoja na Juma kwa kukamilisha hilo deal na najua asilimia kubwa ya Mashabiki wa Simba wapenda maendeleo ya vijana wenye vipaji watakuwa wamefurahishwa na Juma kupata timu bila kujali ni timu gani na kuthibitisha hili hutaona mashabiki wa Simba wakimzomea Kaseja labda kwa wachache wang'oa viti. Hata kama Yanga wamemsajili baada ya kuona Simba wanamtaka sawa tu maana yeye ndo kazi yake na ana haki ya kucheza kokote na watu wa Simba hawatakiwi kumlaumu na kwa uwezo wake lazima atapata nafasi tu ya kucheza hata kama si kila mara kama alivyokuwa akicheza wakati akiwa Simba.
 
Last edited by a moderator:
Walio Muacha kaseja walipepesa macho na kutikisa masikio
Mkuu, mimi ni Yanga , lakini katika hili siungani kabisa na uongozi, sasa mgogoro wa Kaseja na Barthez unahamishiwa Yanga, sidhani kama walifikiri katika hili, hapa hawajawakomoa Simba maana walishamuacha huyo, na sidhani kama tatizo la Yanga ni golikipa. Utasikia sasa gogoro la magolikipa sasa ndani ya Yanga
 
unamzungumziaje Ngasa,alipokuwa simba,Azam na alivyo hivi sasa Yanga?

Ngasa pamoja na utoto wake wa kuonyesha hadharani kwamba ana mahaba na Yanga lakini bado alipokuwa na Azam alicheza vizuri na kuonyesha uwezo wake, hata alipoenda Simba pamoja na kwamba alienda kishingo upande lakini bado alijua ile ni kazi yake na alijituma sana, bado nasema hawa wachezaji ni binadamu kokote anakosajiliwa hasajiliwi kwenda kushangilia lakini anasajiliwa kwenda kucheza, ni kweli asilimia kubwa ya vijana wetu hawana weledi kihivyo lakini ila akili ya kawaida ya kujua kwamba hawa ni waajiri wangu na natakiwa kuwatumikia wanayo.
 
Sina cha kuogopa kuandika yaliyo moyoni mwangu, Kaseja hakuwa mtu wa kukosa timu na hata kama Simba walionyesha nia ya kumsajili na yeye akaamua kwenda Yanga lazima tuheshimu maamuzi yake na ndo maana jana usiku usiku nilivyosoma hii habari sikusita kuwapongeza Yanga kwa kumsajili na yeye mwenyewe kwa kupata timu na kwa sababu naamini kabisa Juma anajitambua na anajua kazi yake hataleta mambo ya kwamba ooh sijui sina mapenzi na hii timu kwa hiyo nicheze chini ya kiwango.

Mimi nilikuwa namhurumia sana Kaseja kwa jinsi alivyokuwa anafanyiwa na mashabiki wa Simba hasa zile mechi za Mtibwa na Polisi mwaka jana, hata kwenye ile mechi na Yanga mliyoshinda 2-0, mtu anapiga free header halafu lawama anapelekewa Juma.

Tukiacha mambo ya ushabiki na kutumia ubinadamu lazima uone ni jambo la heri kwa mwenzako kupata ajira kwa sababu mimi mwenyewe najua hali anayokuwa nayo mtu asipokuwa na kazi maana mimi mwenyewe ilishawahi kunitokea.

Narudia tena nawapongeza sana Yanga pamoja na Juma kwa kukamilisha hilo deal na najua asilimia kubwa ya Mashabiki wa Simba wapenda maendeleo ya vijana wenye vipaji watakuwa wamefurahishwa na Juma kupata timu bila kujali ni timu gani na kuthibitisha hili hutaona mashabiki wa Simba wakimzomea Kaseja labda kwa wachache wang'oa viti. Hata kama Yanga wamemsajili baada ya kuona Simba wanamtaka sawa tu maana yeye ndo kazi yake na ana haki ya kucheza kokote na watu wa Simba hawatakiwi kumlaumu na kwa uwezo wake lazima atapata nafasi tu ya kucheza hata kama si kila mara kama alivyokuwa akicheza wakati akiwa Simba.

Sawa Mkuu.
 
Back
Top Bottom