Kash Patel Mkurugenzi Mpya wa FBI aliyeteuliwa na Rais Trump, mama yake ni Mtanzania!

Kash Patel Mkurugenzi Mpya wa FBI aliyeteuliwa na Rais Trump, mama yake ni Mtanzania!

Raia wetu wote tuwaenzi mfano Captain Arif Jinnah , rubani aliyerusha ndege ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 3. Rubani Atif Jinnah alisomeshwa na Mamlaka ya Usalama wa Anga katika chuo cha Afrika ya Mashariki nchini Soroti Uganda kisha kujiunga Air Tanzania mwaka 1987 na baada kupeleka kitengo cha ndege za serikali za viongozi wa Tanzania ambapo alikuwa rubani wa rais B.W Mkapa kwa miaka 3 ..

View: https://m.youtube.com/watch?v=XgsJvPp-Ock
 
Watanzania mbona tupo kila mahali, kwenye kila issue duniani hutukosekani. Mtanzania vita ya Russia ya ukraine Kuna aliyefia huko, vita ya Israel na hamas watanzania walifia huko. Na leo hii tena kwenye uongozi wa trumps aliyepenya kimiujiza Mtanzania yupo
 
Hii ni Habari Njema kwa watanzania kwamba mkurugenzi mpya wa FBI Kash Patel mama yake alikuwa Mtanzania na baba yake ni Mganda

Tembeeni vifua mbere 😄
Hicho ndicho mlichobakiza waafrika. Unafiki tu, hao jamaa hawana unafiki hadi jeshi unaajiriwa. Bongo kuiba kura ndiyo kazi waliyobakiza
Bongo mchina kafungua duka kariakoo kelele nyingi, wanataka wabongo wauze wenyewe. Bidhaa inayouzwa China 15,000, mbongo anataka kukuuzia 60,000.
Mtu kapambana na maisha yake mpk kafika Marekani unakuja na uzi kuwa ni mtanzania. Kabla ya hapo ulikuwa humjui.
Davido ni raia wa Marekani na muziki anafanya Marekani na kupitia muziki anaipatia Marekani kodi. Kwanini Marekani isiwe nchi yenye nguvu duniani?
 
Naona haya mashangilio karibu sehemu zote za kujianika. Huko Facebook na X pia Insta eti mama yake alikuwa mtanzania... So what😀😀
Sisi bwana kwa kuokoteza...
Kwanini tusipambane kwaajili ya vizazi vyetu vijavyo ili wawe na watu wa kuwapigia mfano? 😀
Jamaa ni mmarekani ndio maana kapewa hicho kitengo na hakupewa sababu mama yake ni mtanzania. Usikute kwenye maelezo yake hakuna Tanzania😀😃
 
Hii ni Habari Njema kwa watanzania kwamba mkurugenzi mpya wa FBI Kash Patel mama yake alikuwa Mtanzania na baba yake ni Mganda

Tembeeni vifua mbere 😄
His name is Kash Patel, is Indian whose parents once lived in TZ and Uganda, Hana tofsuti na Obama, alizaliwa US, 1980
 
Back
Top Bottom