Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Nyinyi mnafikiri mnampenda Lakini hamuelewi ukweli ya yale yanayomsibu au ya yale ambayo yangemsibu Mzazi wake ndiye anyejua yale ambayo yangemkuta kwa yale anayoyafahamu yeye kutokana na habari alizozipata.Mzee Ametumia busara na Nyinyi mnashabikia na FREE AMINA Kwasababu hakuna anayejua kwa undani yanayomsibu huyo Mh.Amina kwasasa na Ambayo yangemsibu baada ya kuwaweka sawa wapinzani wake kwamba anataka kulipua bomu.
Hulka ya wanadamu waliowengi ni Ubinafsi, Mnachoshabikia nyinyi ni kutaka kusikia kile Mh.Amina alichotaka kukitoa hadharani na ndiyo kelele zote za FREE AMINA,Lakini wale wenye Mapenzi ya kweli na wenye uchungu na wanaomthamini Na watakaoathirika zaidi na matokeo ya maamuzi ya Mh Amina na Wanaolijua litakalomfika Mh.Amina endapo ataendelea kupayuka kwasasa ndiyo wanaoguswa zaidi na hiyo hatua waliyoichukua ndiyo wao wanaona ni muafaka kwasasa.Nani Kama Mzazi au Wazazi.?

Tusiyafanye ya wenzetu kuwa rahisi,tuangalie na athari za yale yanayowakuta au yatakayowakuta wenzetu kutokana na matendo wanayokusudia kuyafanya au waliyoyafanya au watakayofanyiwa au waliyofanyiwa.Fikra kila mmoja na zake Lakini wachache wenye kujaliwa BUSARA.[/QUOTE]
 
Jamani mimi ninaamini ni haki yake AC ya kikatiba kuwa na mahusiano na yoyote yule amtakaye. Hebu mwacheni Amina. Kama vile ambavyo ni haki yake ya kikatiba kwa mumewe kumtaliki.Waacheni hao. They are celebrities who enjoy media attention. Hiyo yote ni sehemu ya uasanii. Hamuoni nyie watu?
 
Sawa Mkjj lakini si unajua kuwa dunia ya leo ni kijiji?
 
Ngoja kwanza, hivi kwani Amina ametekwa au namna gani? Mimi nilifikiri amejificha tu kwa kuogopa mkwara wa CCM au? Mnataka kuniambia issue yake ni kama ya Alan Johnson huko Gaza? Kama ni hivyo basi wana harakati kama Mnyika waandae maandamano makubwa Dar ya kumkomboa huyu binti mikononi mwa watekaji na hizo T-shirt zisambazwe kikwelikweli sio kwenye internet!
 
Ndiyo hapo sasa Masatu, wao wanalifanya gizani wenzao tunaliona kama mchana kweupe!!
 
Nyinyi mnafikiri mnampenda Lakini hamuelewi ukweli ya yale yanayomsibu au ya yale ambayo yangemsibu Mzazi wake ndiye anyejua yale ambayo yangemkuta kwa yale anayoyafahamu yeye kutokana na habari alizozipata.Mzee Ametumia busara na Nyinyi mnashabikia na FREE AMINA Kwasababu hakuna anayejua kwa undani yanayomsibu huyo Mh.Amina kwasasa na Ambayo yangemsibu baada ya kuwaweka sawa wapinzani wake kwamba anataka kulipua bomu.

Machumo... kama wewe hujui haina maana wote hawajui...


Hulka ya wanadamu waliowengi ni Ubinafsi, Mnachoshabikia nyinyi ni kutaka kusikia kile Mh.Amina alichotaka kukitoa hadharani na ndiyo kelele zote za FREE AMINA,Lakini wale wenye Mapenzi ya kweli na wenye uchungu na wanaomthamini Na watakaoathirika zaidi na matokeo ya maamuzi ya Mh Amina na Wanaolijua litakalomfika Mh.Amina endapo ataendelea kupayuka kwasasa ndiyo wanaoguswa zaidi na hiyo hatua waliyoichukua ndiyo wao wanaona ni muafaka kwasasa.Nani Kama Mzazi au Wazazi.?

yaani unahalalisha mtu kushikiliwa kwa vile kuna watu wachache ambao wataathirika endapo Amina atasema alichotaka kusema?


Tusiyafanye ya wenzetu kuwa rahisi,tuangalie na athari za yale yanayowakuta au yatakayowakuta wenzetu kutokana na matendo wanayokusudia kuyafanya au waliyoyafanya au watakayofanyiwa au waliyofanyiwa.Fikra kila mmoja na zake Lakini wachache wenye kujaliwa BUSARA.

Wamuachile tu Amina, kama anataka kusema aseme kama hataki kusema basi asiseme yeye ni mtu mzima! Kama wanaona Amina "hana akili timamu" za kuweza kuamua la kufanya basi watake ajivue au avuliwe Ubunge.
 
hili la sasa naogopa hata kusema (na mimi si mwoga hivyo...)... Mwe Majira haya ni ya kiangazi huku kijijini, na joto limezidi..!!
Mwanakijiji!
Si unaona wewe upo Marekani Lakini una habari ya huyu Mheshimiwa Lakini Bado hutaki kuisema unasubiri wakati muafaka kufanya hivyo,Lakini mlitaka Mh. Amina ambaye yupo kwenye mazingira ya KARIBU NA MAADUI ZAKE AFANYE HIVYO,HATA BAADA YA MZAZI KUIONA HATARI ILIYOPO AU ITAKAYOMKABILI MWANAE NA KWENDA YEYE MAELEZO NA KUOMBA MSAMAHA,Ili Kutafuta njia muafaka wa kulizungumzia.Huyu Mzee mbali na kupokea simu aliyopigiwa kuhusu mwanae kutoka kwa kiongozi mmoja Mwanza kama ulivyoeleza awali LAKINI Amekua askari na kada wa muda mrefu anakielewa chama chake kwa undani na anayaelewa yanayomkabili mwanae kwasasa jamani Damu ni Nzito kuliko Maji.
 
Ngoja kwanza, hivi kwani Amina ametekwa au namna gani? Mimi nilifikiri amejificha tu kwa kuogopa mkwara wa CCM au? Mnataka kuniambia issue yake ni kama ya Alan Johnson huko Gaza? Kama ni hivyo basi wana harakati kama Mnyika waandae maandamano makubwa Dar ya kumkomboa huyu binti mikononi mwa watekaji na hizo T-shirt zisambazwe kikwelikweli sio kwenye internet!


Mwanasiasa, kushikiliwa kwa Amina siyo kama kwa Alan Johnson bali ni kama kwa yule mama wa Burma. Siyo kwamba ameshikiliwa kwa kufungwa kamba n.k bali ananyimwa uhuru wa kukutana na mtu yeyote anayetaka kukutana naye, amenyang'anywa simu zake zote, na hawezi kwenda mahali popote pasipokuwa na mtu wa kuangalia afanyacho. Kwa ufupi, "ndugu" hawataki Amina aseme hadharani masahibu yake kwani anatishia "pensheni" yao. Sasa hivi kundi la watu hawa wameingilia uhuru wa Amina na pia wanatishia majukumu ya vyombo vya habari kutafuta na kupata habari.

Kama Amina hana la kusema basi wamuachilie ili aendelee na shughuli zake za kila siku!!
 
Nimegundua kuwa Zitto alichukua ushauri wa kula sahani moja na Chifupa kutoka kwenye forum hii hasa kwa vile yeye pia ni active member. Kuna mwanaforum aliwahi kumshauri hivi:

Tanzanianjema said:
Ndugu wana JF

"ninachomuomba na kumshauri Bw. Kabwe, yeye afuate nyayo za Amina Chifupa ili aweze kujinadi na kueleweka katika anga za siasa" Mtoaukweli? Ar u serious?
Mimi nimmoja wa vijana wachache wanaoamini mchango wa dada yetu Amina lakini sidhani kama ni vizuri kumshauri Zitto kufuata staili ya Amina. Calibre ya Zitto ni nyingine na Amina ni nyingine. Wote wanawakilisha aina mbalimbali za Utanzania na ndio maana ya kuwa na Bunge

"Ushauri wa bure kwanza aache kutoroka bungeni!" Ndugu zangu kwani Zitto ni mtoro. Acheni kumuonea.
...........................

Kwa habari zaidio angalia hapa
 
Padri asababisha kifo akimtoa mimba binti




na Ramadhani Siwayombe, Manyara



PADRI mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu (jina linahifadhiwa), anatuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Dongobesh wilayani Mbulu.
Kama hiyo haitoshi, inadaiwa kuwa baada ya kubaini kuwa binti huyo ni mjamzito, padri huyo alimtorosha na kwenda naye mjini Babati kwa lengo la kuitoa mimba hiyo lakini kwa bahati mbaya binti huyo alifariki dunia wakati wa zoezi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, shangazi wa binti huyo, ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuhofia usalama wake, alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Veneranda Anthony Yessaya, ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na padri huyo kwa muda mrefu.

Shangazi huyo alisema kuwa padri huyo alifanikiwa kumrubuni binti huyo kwa njia ya kujifanya mfadhili wake, ambaye atamgharimia masomo.

Alisema padri huyo alijitokeza wakati marehemu Veneranda akijiunga na kidato cha kwanza mwaka 2006 katika Shule ya Sekondari ya Gidhim, iliyopo wilayani Mbulu.

Alibainisha kuwa, padri huyo aliamua kumhamisha na kumpeleka Shule ya Sekondari ya Endaraftal, iliyopo wilayani Karatu.

Alisema baada ya muda, walishangaa padri huyo akimhamisha tena binti huyo na kumpeleka Dongobesh Sekondari, ambako aliendelea kuwa na mahusiano naye kimapenzi.

Akisimulia zaidi, shangazi huyo alisema walianza kuhisi uhusiano usiofaa baina ya binti yao na mfadhili wake Aprili 20, mwaka huu, baada ya padri huyo, ambaye alihamishiwa Kiru akitokea Dongobesh, kufika kijijini Dongobesh na kuonekana akiwa na binti huyo.

Na baada ya kuulizwa, padri huyo alidai amefika hapo kumchukua ili akamnunulie vitu muhimu vya shuleni.

Aprili 26, binti huyo aliomba ruhusa kwa uongozi wa shule, kwa madai kuwa alikuwa anakwenda nyumbani kwa wazazi wake, ambapo baba yake ni mwalimu katika Shule ya Msingi ya Dumanangw na alipofika nyumbani alipewa fedha na wazazi wake na kuaga kuwa anarejea shuleni.

Shangazi yake huyo alisema hata hivyo, binti huyo hakufika shuleni tena na badala yake alikwenda Babati, ambako inadaiwa alikutana na padri huyo na walikwenda katika moja ya nyumba ya kulala wageni mjini hapo.

Ilielezwa kwamba baada ya siku kama mbili, padri huyo alimfikisha binti huyo katika hospitali moja (jina tunalo), iliyopo mjini Babati, akiwa mahututi. Baadaye, padri alimpigia simu mama mzazi wa binti huyo, ambaye kwa wakati huo alikuwa mjini Arusha.

“Baada ya kuona hali ya binti huyo ni mbaya, kabla hata ya wazazi wa binti huyo kufika, padri huyo alitoroka na kumwacha binti huyo katika hospitali hiyo na baadaye alifika mama yake na baba yake ambao walilazimika kumchukua na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi,” alisimulia shangazi huyo.

Uchunguzi uliofanywa na daktari katika Hospitali ya KCMC ulibaini kuwa binti huyo alikuwa ametolewa mimba lakini kitendo hicho hakikufanywa ipasavyo kwani kulikuwa na uchafu uliokuwa umebaki tumboni na kufanya sehemu za mwili wake zianze kuoza.

Akisimulia mkasa huo kijijini kwake Dongobesh juzi, baba mzazi wa marehemu, Mwalimu Anthony, alisema: “Uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya KCMC umegundua kuwa utumbo pamoja mfuko wa uzazi navyo vilianza kuoza.”


Mwalimu Anthony alisema kutokana na hali hiyo, familia yake imeamua kufungua kesi Polisi dhidi ya padri huyo. Hata hivyo, alidai kuwa uongozi wa kanisa jimboni Mbulu unamkingia kifua padri huyo ambaye amejificha.

Mmoja wa madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa binti huyo, ambaye alikataa kutajwa kwa vile si msemaji wa hospitali hiyo, alisema binti huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi mitano, alikuwa ametolewa mimba kwa vifaa vichafu.


uchafuzi si lazima uwe wa hewa na hali ya hewa duniani.....hata huu pia...ni uchafuzi....wa mada!
 
Eeh bwana Chifupa ni maneno ya Sumbawanga bro, ogopa ndugu yangu kwa Dr. Majiyatanga Mzindakaya huko, yaani Mwera watu hutembea uchiii wa mnyama mchana lakini huwezi kuwagusa!

Au hujasikia Mwalimu alivyopewa zawadi ya gunia la mchele, kuingiza kwenye gari likayeyuka!

Lakini uzuri Mpakanjia ni mtoto wa Goba huyo, hakuna noma kabisaaa, muulize bm siku ya uchaguzi wa mgombea Chimwanga ilikuwaje!
 
Mwanakijiji kumbe na wewe umeshtukia ama umemegewa habari kutoka jikoni.

Jamaa ndiyo katengeneza ile spining ya kwenye majira kuhusu wana Chadema kuhoji uaminifu wa Zitto kwa siri za Chadema. Hilo gazeti hivi karibuni litakabidhiwa rasmi kwa MANJI kwa kumtumia "Fulani" hivyo hayo ndio maandalizi tu. Inabidi jamaa wote wa lile gazeti "letu" la HOJA wahamie MAJIRA maana ndiyo hivyo tena limeshachukua kibarua chao.

Anachofanya huyu jamaa ni kujaribu kuanzisha mjadala ndani ya umoja wa vijana wa CCM kuhusu uaminifu wa AC kwa "SIRI" za CCM kwa kujifanya kumlenga Kabwe. Hayo ndiyo aliyokuwa akiyatumia mwanzoni na wenzake ambao mpaka sasa bado hakuna ulazima wa kuanikwa. Baada ya kuona mwanadada anaendelea kuvuma ingawa tayari alishamwaga hiyo sumu ndipo akaamua kutumia hiyo Nyuklia yake ambayo tayari imeshaanza kumrudi.

Anyway ndiyo mambo ya POWER BY ANY MEANS NECESSARY!
 
whatever their case is, has no to be covered by national news, so i call upuuzi ( public stunt ) kupata headlines tu kwenye magazeti !! sasa dada unataka umaarufu kwa nguvu, watu watakuchoka mapema !!
 
hili la sasa naogopa hata kusema (na mimi si mwoga hivyo...)... Mwe Majira haya ni ya kiangazi huku kijijini, na joto limezidi..!!


Mwanakijiji tunakuamini kwa uwezo wako wa kupata stori bila kutoka huko kijijini kwako. Kama utashindwa kutuangushia stori hii tutakuvuta mjini kwa vile utakuwa umeshindwa kzai ya kijijini.

Haya tuambie, huyu DOKITA EC anafanya nini kutafuta urais wa Tanzania kwa kutumia ushirikina na uzandiki kuangamiza wengine wote wanaopingana naye kisiasa? Je ni kweli kuwa korogeo lake ni kali sana kiasi cha kumtisha hata JK? Yaani sasa hivi CCM mtandao wanashindana kwa ukubwa wa mkorogeo badala ya kushindana kwa hoja? Sijakuelewa vizuri tafadhali fafanua. This is very important, sir.
 
Hodi wanabodi! Heshima yenu wakuu! kwa kipindi kirefu mimi nimekuwa msomaji tu makala mbali mbali humu, bila kuchangia chochote, hivyo naheshimu sana mawazo na michango yenu yote, ila katika hili imenibidi nitoe maoni yangu.

Ama kwa hakika suala la ndoa si suala la kuliingilia, kwa maana kwamba, kwangu mimi sitaona ajabu baada ya muda mfupi ujao Bwana MM akaamua kumrudia mkewe Bi AC! Jambo ninalopenda kuwatahadharisha wanabodi n kwamba itakuwa ni aibu kubwa kwa wazee wenye busara kama nyie mkianza 'kusutwa' hadharani mkinukuliwa posts mlizoweka humu.

Jaribuni kulitafakari hili, nadhani Mzee mwkjj, Mkandara na wengineo wachache wamekuwa wajanja katika kutizama pande zote za shilingi bila kuwahukumu hao watuhumiwa moja kwa moja. Hii thread iendelee kujadiliwa ila, muwe makini kuwa huu ni udaku!, na itapofikia wakati wazee wetu mkianza kusutwa, hata maoni yenu mengi tu ya busara yataonekana kama ya udaku udaku tu. Heshima yenu wazee, naomba kutoa hoja!

Shukran.
Hivi kaka mchongoma umetukimbia tena? Looo acha uchoyo huo ama kazi ya kulinda urithi wa babu inazidi kuwa ngumu. Usiwe na shaka kaka kwa pamoja tutatoka tuu katika kipindi hiki kigumu.

Tanzanianjema
 
I wish this was made much clearer.

(a) Majira ni spinning machine; OK, nitaiondoa kwenye boomarks zangu. Kwana huwa wanachelewa ku-update news kwa karibu wiki nzima. Kwa nini ichukuliwe na Manji? Ili aweze kupambana na Mengi?

(b) hii sehemu ya pili niyo sikupata
Anachofanya huyu jamaa ni kujaribu kuanzisha mjadala ndani ya umoja wa vijana wa CCM kuhusu uaminifu wa AC kwa "SIRI" za CCM kwa kujifanya kumlenga Kabwe. Hayo ndiyo aliyokuwa akiyatumia mwanzoni na wenzake ambao mpaka sasa bado hakuna ulazima wa kuanikwa. Baada ya kuona mwanadada anaendelea kuvuma ingawa tayari alishamwaga hiyo sumu ndipo akaamua kutumia hiyo Nyuklia yake ambayo tayari imeshaanza kumrudi.
Kuna mtu anaweza kufafanua? Ni kama ninakosa conection mahala fulani hapa.

(i) Alikuwa akifanya mwanzoni na wenzake: akina nani? JK dhidi ya SAS
(ii) Mwanadada aliendelea kuvuma pamoja na kumwaga sumu: ipi, "list ya madawa ya kulevya?" au hii ya "kugawa free samples"
(iii) Kutumia hiyo nyuklia: ipi hii ya juzi ya AC Vs ZK? Kuna taarifa kuwa wabunge wengi wametafuna huyu binti, kwa hiyo ni kwamba EC alitafuta nafasi ya kumwaibisha AC kwa kutumia mbunge wa nje ya CCM? na hivyo kuhoji uwezo wake kiuongozi kuficha SIRI? Kwanza: Siri ni ninini na siri kwa nini na ni kwa nini ni siri.
(iv) Imeanza kumrudi: Hapa ndipo sielewi kabisa. Inaanza kumrudi nani AC, EC au ZK. Na inamrudi vipi?
 
nasaha kwa wadogo zangu AMina na kabwe

nnazituma kwa njia za ushairi nilioquote mzee wetu Abbasi Mzee

akufanyae ubaya bora umnyamazie
usichukue hatua nafasi yake mwachie
kama hujamkosea fahamu ajidhuru mwenyewe
atakalo kusudia mungu si pamoja nae
-----------------------------------------------
usimfanye lolote ingawa una machungu
mikono juu iweke bora umwachie mungu
mwache ende pande zote hata juu ya mawingu
ubaya una mwisho wake mwache ajigawe mafungu
atapa haja yake zawadi ya ulimwengu

-----------------------------------------------
nguvu usiitumie ndugu yangu nakwambia
utajidhuru mwenyewe ukiifata duniya
haki ya mtu ujuwe wala haitapoteya
wala usijisumbue mungu atakulipia
mungu si khiyana ujuwe omaba nawe utapewa

haifai kuvamia


nasaha zangu za ghali nnaomba afikishiwe ndugu yangu Amina na kwa wakati huo nnamnasihi na mdogo wangu KABWE.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom