Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Mzee TZnjema,

Bigups bro, ila tu nimeshidnwa kuimaliza hii article lakini nitaitunza mpaka weekend niisome tena, lakini ina some points, na ninasema hivi Wa-Tanzania tunahitaji kuamuka, hizi siasa chafu are here to stay, haziendi kokote na the fact of the matter is hata Mwalimu alikuwa akizitumia hizi games, lakini wananchi tulikuwa tunamuamini na kufikiri kuwa it was the best for the country,

Aliyeyahalalisha haya makundi ni bm, kwa sababu wakati wa utawala wake ni wale tu waliokaribu na yeye ndio waliokuwa na free pass, kwa hiyo watengwa wakajikusanya na kuwa a team, na haya ndio matokeo yake!
 
Ningelikuwa Ziito Na Amina

Nimekuwa nikifuatilia maisha ya kisiasa ya ndugu zangu hawa wawili yaani Dada Amina binti Chifupa na Kaka yangu Zitto mwana wa Kabwe kwa muda mrefu sana. Zitto tangia akiwa pale Mlimani na Amina tangia alipoanza ule utundu wake katika Radio Clouds. Ni wazi kuwa haiba, ujuzi na fikira za ndugu zangu hawa wawili ni tofauti lakini sina shaka na kushabihiana kwao kuhusu upendo wao wa dhati kwa binadamu wenzao na Tanzania yao, utayari wao wa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa letu na zaidi vipaji vyao kisiasa.

Sitaongelea sana kuhusu Zitto lakini kuhusu Amina ambaye ndiye mpaka sasa amekuwa muhanga mkuu wa kadia hili ambaye nathibitisha kuwa nipo tayari kuzama naye. Hapo mwanzoni mimi kama walivyo watanzania wengi mijini ambao tunajiona usomi wetu ni kigezo tosha cha kuamua nani atuongoze na nani asituongoze, nilikuwa mmoja wa watu ambao walikuwa wanapinga kabisa kwa Amina kuwa mbunge.

Kutokana na kugubikwa na taswira ya uchafu dhidi ya dada yangu Amina aliyokuwa akipewa na watu wachache wanaojiona kuwa wao ndio wasafi na wana haki ya kutumia uwezo wao wa umiliki na uandishi wa vigazeti mbalimbali vya udaku, nilikubali kabisa kuwa Amina hafai kuwa kiongozi katika jamii yetu.

Hata hivyo baada ya kuangalia undani wa mwenendo wa uandishi wa habari za kumchafua Amina katika magazeti mbalimbali ya udaku ambayo baadae nikagundua kuwa mengi yanamilikiwa na kusimamiwa na mtu mooja ambaye alikuwa na vita binafsi na Amina niliweza kufungua kichwa changu na kujenga ushawishi wa kutaka kumjua zaidi Amina.

Ndipo siku mmoja mahala fulani nilipopata bahati ya kumsikia Amina akiwa jukwaani mbele ya umati wa vijana wenzake wengi wao wakiwa ni wasomi wanaochipukia. Baada ya kusikiliza kwa makini hotuba ya Dada Amina nikagundua kuwa ni wazi Amina niliyekuwa nalazimishwa na vijigazeti vya udaku na maneno ya watu si huyo ninayemuona mbele mbele. Huyu ni Amina mwenye kipaji kikubwa cha kisiasa na Amina mwenye uthubutu mkubwa wa kusema yale anayoamini bila ya kujali madhara yake kwake binafsi. Ni Amina ambaye yupo tayari kuwa yeye bila ya kujaribu kuwa mtu mwengine kama wanasiasa wetu wengi tuliowazoea walivyo ama watanzani wengi wengelitaka awe.

Kuanzia siku hiyo niligundua kuwa hata kama dada yangu Amina ana mapungufu yake, ni wazi kuwa ana sifa ambazo kama zitathaminiwa, kujengwa na kutumiwa ipasavyo ni hazina kubwa ya taifa letu linalohitaji vijana wenye kuwa na moyo na haiba ya uthubutu kama aliyonayo Amina.

Wengi wamekuwa wakimwona Amina kama kijana mdogo ambaye amekosa wasifu wa kuwa kiongozi katika jamii. Wengi wanamuona Amina kama ni mtu anayependa sifa na asiye na umakini. Wapo wanamuona Amina kama ni mropokaji anayepaswa kudhibitiwa mapema. Wapo wanamuona Amina kuwa ni mfano mbaya wa kimaadili katika jamii yetu. Wapo wanaomuona kuwa ni hatari kwa maslahi ya Taifa. Wapo wanao muona kuwa ni hatari kwa maslahi yao. Wapo pia wanaomuona kuwa ni hatari kwa maslahi ya Chama chake.

Hawa wote wana haki ya kumuona hivyo lakini vilevile ni wazi hawana haki ya kumuhukumu na zaidi wengi wao hawana hata uhalali wa kumuonyesha kidole Dada yetu mpendwa Amina. Waanze kujinyoshea wao kwanza!!!!

Kuhusu haiba yake ya udogo ama utoto ni wazi kuwa wanao kuwa hivyo kunamuondolea uhalali wa yeye kuwakilisha vijana wenzake wwa CCM wanashindwa kuelewa nini maana ya uongozi na zaidi nini maana ya uwakilishi bungeni. Udogo wa Amina ama ukitaka utoto wake ni mchango muhimu katika bunge letu. Maana ya BUNGE kama historia inavyoonyesha ni kuwa mahala ambapo kuna mkusanyo wa uwakilishi wa mawazo ya raia wa aina zote. Udogo ama Utoto wa Amina ni hazina na chachu muhimu kwa maaendeleo ya kimawazo katika jamii na nchi yetu. Kama ni busara za Uzee wapo kina Mzee Malecela, Kingunge, Kabuye, Mama Mongela, Mama Anna Abdalla na wengine wengi tu ambao daima wamekuwa wakitekeleza wajibu huo. Na zaidi pia wapo vijana kama kina nanihii ambao wakiwa na umri chini ya miaka 40 wanacho kiongea hakina tofauti na wazee wa miaka 80 na hawa wameteuliwa eti kwa kigezo cha kuongeza uwakilishi wa vijana bungeni. Wanashindwa hata na Mzee Mzindakaya ambaye ingawa naye tayari amemua kujiunga na kundi la viona mbali kimaslahi, bado maoni na michango yake ina uthubutu wa kiujana akiungana na Rais wetu aliyechaguliwa na asilimia 80 ya watanzania waliopiga kura mwezi desemba 2005.

Kwa wale wanaomuona ni mtu wa kupenda sifa na asiye na umakini ni wazi wanawakilisha utamaduni mbovu wa watanzania wasiokuwa tayari kujitokeza mbele kutenda na kusimamia kile wanachoamini kinahitajika kufanyika katika jamii yetu. Bahati mbaya utamaduni huu unawafanya kila atokeapo mwenzao aliyetayari kuthubutu kutenda na kusimamia kile wangelipenda kitendwe huishi kumuona ni mpenda sifa. Amina ameonyesha kuwa tofauti na wengi wetu kwa kuwa tayari kutenda yale anayoamini anapaswa kuyatenda bila ya watu watasema. Inasikitisha kuwa watu hao hao wanaokimbilia kusema kuwa Amina ni mpenda sifa ndio wasiokwisha kulalama kuhusu mapungufu katika jamii yetu.

Kiongozi mmoja mstaafu barani Afrika aliwahi kunifundisha ni jinsi gani bara letu linavyokwazwa na kile kinachoitwa umakini ama busara. Kwake yeye na nakubaliana naye kwa dhati kuwa mara nyingi tumekuwa tukitumia dhana za umakini na busara katika kuulinda na kuukingia kifua uozo mbalimbali katika jamii zetu. Kijana kama Amina ni wakati wake kuripua yasiyotakiwa kuripuliwa bila ya kujali kile tunachokiita umakini. Umri unamruhusu na maslahi ya jamii yetu yanamhitaji kufanya hivyo. Kama Amina ama Zitto akianza kujizuia kusema ama kutenda yale ambayo yanapaswa kusemwa ama kutendwa eti kwa kuonyesha umakini, Wazee kama kina Mzee Malecela, Kingunge, Mzee Sitta, Mama Mongela, Anna Abdallah na wengine wanafanya nini katika uwanja wa siasa? Hao ndio wenye jukumu la kusimamia kile kinachoitwa Busara na Umakini na mchango wao tunauthamini kama tunavyopaswa kuthamini na kutetea michango ya Amina na Zitto.

Na wale wanaomuona Amina kuwa ni mfano mbaya kwa maadili kwa jamii yetu napenda kuwauliza kosa la ndugu hawa kama kweli wametenda wanachoshutumiwa, ni hilo tendo lenyewe ama kutokana na wao kushindwa kulizuia suala hilo lisifikishwa katika vyombo vya habari kama ambavyo wakubwa wao walio wengi katika ulingo wa siasa na uongozi walivyfanikiwa kufanya. Tunataka kujifanya kuwa haya yanayosemwa kuhusu ndugu zangu hawa wawili ni mageni kwetu? Hivi tumekaa tukajiuliza ni lini suala hili limekuwa dhambi katika jamii yetu iliyojaa ufuska wa kila aina katika kila kona?

Hivi hivyo vinyang'au vidogo walioamua kutumia muda wao kubomoa Nyumba ya dada yetu Amina ambayo ukweli ni kuwa ilishabomoka tangia wakati wa ujenzi wake wanataka kutuambia kuwa wao ni wasafi na ndio maana wengine wanajigamba kwamba piga ua ni marais 2015. Hivi vile vyumba vya uzinzi wanavyomiliki na kulipia kodi za pango kila kukicha katika mahoteli na nyumba kadhaa katika kila pembe za jiji na nchi hii wameshavigeuza makanisa na misikiti kuanza kutubia? Hivi ………… ngoja tu ninyamaze nisije na mimi pia nikahukumiwa kwa kutokuwa na hekima na umakini.

Kwa kweli inasikitisha kuona ni jinsi gani hivi vinyang'au vyeneye nia ya kulinda uozo wao na mabwana zao wanavyoweza kuchezea akili za watanzania kiasi hiki. Ningelikuwa mimi ndio Amina na Zitto ningelifanya yafuatayo.

Kwa kuwa ni wazi sehemu jamii imeshakubali ulaghai wa hivi vinyang'au vinavyochipukia ambavyo vinajitahidi kulinda kulinda uozo wao na wa wengine wa wazazi wao, kwa kuwa jamii imeshaamua kuwahukumu kama wanavyokimbilia kuwahukumu viongozi wetu wengine kutokana na kile kinachoitwa hulka zao, kwa kuwa wao ni vijana na tofauti na hao vinyang'au wao wana nafasi kubwa ya kulibadilisha taifa hili na siku moja tukajivunia, na kwa kuwa kwa muda mchache walio upata wameweza kutusemea vijana wenzao tunachotaka watusemee na kututhibitishia uchungu wao kwa taifa letu sisi vijana wa taifa la leo, na kwa kuwa wao ni vijana waliothibitisha kuwa wapo tayari kujitoa muhanga kwa ustawi wa taifa letu.

Ningewashauri baada ya kushauriana na wale wawapendao na sio wale malaghai waliokuwa wakiwatumia kwa maslahi yao binafsi na kuwakimbia mara tu mambo yanapoeleka kuharibika. Kwa pamoja watoke mbele vichwa juu na hata kama hawajafanya hicho wanachotuhumiwa, wakubali na kuwaomba radhi wale wote waliojenga matumaini kwao kwa kutokuwa waangalifu dhidi ya mbinu za maadui wa masalahi ya watanzania yanayoendelea kukanyagwa na manyang'au wakubwa na hivi vinyang'au vidogo vinavyoota kuwa hadi 2015 watanzania bado tutaendela kulea uozo wao na wao wakawa marais wa nchi hii.

Baada ya kukubali kujitwika kafara hilo wawashukuru watanzania wote waliojitokeza kulizungumzia suala hilo na kuwaomba waendelee kulijadili kwa mapana yake na kuhoji uhalali wa kuendela kunyamazia mambo kama hayo katika jamii yetu ambayo sisi wenyewe tunayafanya na kuyafumbia macho kila kukicha. Wawaombe Watanzania wengi zaidi kujitokeza kuungana nao katika misa na sala maalumu za maungamo binafsi na halafu wajiunge nao katika kuanzisha ukurasa mpya wa kimaadili katika taifa letu. Waungane nao katika kuhoji yale yote yasemwayo vichochoroni kuhusu mporomoko wa maadili katika jamii yetu na zaidi miongoni mwa wale ambao tumewaamini kuwapa madaraka ya kuliongoza taifa letu.

Mimi naamini kuwa kuanzia viongozi mpaka waongozwao kwa pamoja tunapaswa kuchukua hatua za haraka na za kishujaa kusimama kidete kupambana na tatizo la uporomokaji wa maadili binafsi miongoni mwetu. Badala ya kutumia muda wetu mwingi kuwasulubu ndugu zetu hawa tunapaswa kutumia nafasi hii kuleta mabadiliko ya kinyakati ambayo yatatusaidia kulinda utanzania wetu na Tanzania yetu kwa ujumla. Pamoja na hali kuonekana kuwa ni ya kusikitisha naamini kuwa kilichotokea ni nafasi adimu kwa jamii yetu kuweza kuamka na kuukabili ukweli kuwa jamii yetu ina tatizo sugu la ukosofu wa maadili binafsi.

Kaka Zitto na dada Amina, Simameni vichwa juu na shikeni usukani kutuongoza katika mpambano huu muhimu katika kulinda Utanzania wetu. Amkeni tuwakabidhi ufunguo wa Tanzania mpya. Amkeni ndugu zangu tujenge Tanzania iliyo njema kwa wote. Tupo pamoja yenu na daima tutakuwa pamoja.

Pamoja tutajenga Tanzanianjema
 
Katika hili ninachoona ni tabia ya "mfumo dume" wa jamii yetu ambapo mwanamke anayetembea na wanaume wengi anaitwa "malaya" na hadhi yake kijamii inashushwa wakati mwanamme mwenye kulala na wanawake wengi anaonekana mwenye sifa na jina lake linatangaa. Mwanamme ambaye anatembea na mwanamme zaidi ya mmoja anatakiwa ainamishe kichwa chini kwa haya wakati mwanamme anayetembea na wanawake wengi inampasa atembee kichwa juu na wakati mwingine ni sifa ya wazazi wake!

Makala hiyo inathibitish hilo. "sifa mbaya" ya Amina ni kwa vile ni msichana ambaye anadaiwa kuwa na maamuzi yake binafsi ya nani analala naye na hivyo kuonekana binti malaya. Wale wahukumu wa tabia hiyo watumie kigezo hicho hicho kuwaabisha viongozi ambao tunawafahamu hadi leo hii ambao wamekuwa na tabia hiyo. Namfahamu mmojawapo wa wabunge ambaye ni WAZIRI katika serikali ya sasa ambaye amekuwa akichukua vitoto vya shule ya sekondari kabla hajaukwaa Ubunge.

Nafahamu wabunge kadhaa wa chama tawala ambao miaka nenda rudi wamekuwa wakitembea na wake za watu, walimu wa shule za msingi n.k Na wengine wamezaa hadi watoto mitaani!! Lakini kwa vile hawa ni wanaume tabia hiyo inaonekana ni sifa na imezoeleka. Watu wanasema Amina hakufuaa kuwa Mbunge kwa sababu "amekuwa akiwavulia watu nguo"!! Vipi wabunge wanaume na mawaziri ambao wamekuwa wakiwavulia watu nguo na kila kukicha wanapewa sio Ubunge tu bali hadi uwaziri!!!? This is a classic example of double standard!

Wakati Ditopile alipofumaniwa na mke wa mtu na kutoa lile jibu la dhihaka ni nani alisema hastahili kupewa Ukuu wa Mkoa? Ni nani aliyesema kuwa hicho kilikuwa ni kitendo cha aibu na asingestahili kupewa uongozi wa aina yoyote? Bila ya shaka kama angekuwa ni mwanammke na amefumaniwa hivyo na kutoa jibu la namna hiyo watu tungesema huyo mwanamama "chizi"!!

Narudia tena sitetei hata kidogo kitendo wanachotuhumiwa kufanya, ila nakataa kabisa kumfanya Amina aonekane kuwa ni "malaya mkubwa" tangu enzi za Clouds FM na hakustahili kuwa kiongozi wakati leo tunao wabunge, mawaziri, mawaziri wakuu wastaafu, n.k ambao wamelala na makumi ya watu!! na wengine wamezaa nje ya ndoa zao kama utitiri na bado wanatamba a uongozi wa vyama vyao!!

Kama kweli hili ni dili na ni kosa, nitafana iwe misheni yangu kuwaumbua viongozi wote wenye maadili machafu ya ngono na tutawataja kwa majina yao na nyadhifa zao ili tuone kama watapewa hukumu ya Amina. !!

Makala hiyo juu ya Amina ni ya kibabe, kinyanyasaji kijinsia, na yenye kutaka kuwafanya wanaume wajisikie wao bora kwa vitendo vyao wakati wanawake walaaniwe. Katika ulimwengu wa sasa mawazo ya namna hiyo yamepitwa na wakati!! Kama kweli tunatetea maadili tuwe wa kweli kwa nafsi zetu na kulaani, na kuwaumbua viongozi wengine wote ambao maadili yao ngono yamepotoka! Tunaposema Amina na Zitto hawastahili kuongoza kwa vile wameshtumiwa kuhusiana kimapenzi basi tutumie kipimo hicho hicho kuwapima viongozi wengine. Kipimo kiwe:

a. Kiongozi yoyote aliyeenda nje ya ndoa yake, hastahili kuwa kiongozi
b. Kiongozi yoyote ambaye amekuwa na mahusiano ya mapenzi na kiongozi mwingine wakati yeye au huyo mwenzake yuko kwenye ndoa, naye hastahili kuwemo kwenye safu ya uongozi.
c. Kina mama wote ambao wamezaa na viongozi wajitokeze hadharani na kudai fidia ambayo itakatwa kutoka katika mapato na mafao ya viongozi husika.
 
Hili la kukubali kwamba wamefanya hata kama hawakufanya na wawaombe Watanzania Msamaha si dhani kama ni Ushauri MZURI,Mimi nasema ushauri huu utaendana tu Kama kweli wamefanya Lakini Kama Hawakufanya Basi waendelee na msimamo wao wa kile wanachokisimamia na chenye ukweli juu ya tukio hilo.Huwezi kuomba Msamaha kwa kitu ambacho hukutenda tena kitu chenyewe Kama hicho ambacho kimekuchafulia jina,waombe msamaha kwa kosa gani?Kama wamesingiziwa basi wao ndiyo wa kuombwa msamaha tena si wale waliowazushia hilo bali hata wale tuliyodiriki kuwahukumu kwa hilo bila ya kufanya uchunguzi na uchambuzi yakinifu..
 
tuanze na igp mahita, kazaa na housegirl wake mbona magazeti hayakumshupalia kama huyu dada?
 
mtu mwitu si ndo hapo sasa... ila angekuwa waziri wa kike kazaa na House Boy.. ingekuwa habari! na angeitwa Malaya!!
 
tuanze na igp mahita, kazaa na housegirl wake mbona magazeti hayakumshupalia kama huyu dada?

Mzee Ben naye si inasemekana ana mtoto wa nje so is Mrs...
Muungwana naye. hapo tusiende.
 
JOSEFU KUSAGA hana maana hata kidogo
Kamfanya yule binti wa KINGAZIJA kawa kama AMMY WINEHOUSE !!!
 
samvula bado sijakupata hapo? ina mahusiano na hapa au mkono ndugu?

ama kuhusu kuomba radhi kwa usilofanya no, cha msingi kuwa wa kweli na kuthibitisha ukweli wao, ikiwa wamefanya wathibitishe na waombe radhi la hawakufanya wathibitishe kwa jamii na waendelee na msimamo wao.

suala la maadili na la wote, kwa hiyo sote tujitahidi kuwa waadilifu, na tunatakiwa kusoma makosa ya wenzetu ili tujirekebishe au kuendelea na tabia njema
 
Wakuu Mpakanjia nimemuona leo kwa Michuzi blog yuko fit kiasi. na zile fulani za kampeni ya Amina zinapatikana wapi? au Michuzi ndio dalali?
 
Udaku unafurahisha kweli.

Jina la Joeseph Kusaga niliw2ahi kulisoma kule kwa Michuzi kuwa ni Mkurugenzi wa FM Clouds alikokuwa akifanya Amina Chifupa na kuwa alitembea na AC sana wakati huo kabla hajawa mbunge. Sijui kama ni kweli ila nadhani CholeSemvula alikuwa anaunganisha stori hiyo hiyo.
 
kuna tetesi kuwa Nchimbi mchawi jee ana kamati yake ya ufundi au yeye mwenyewe ana mkoba wa babu yake?
kama ndivyo tumtumie atusaidie timu ya Taifa na senegal june 2.
 
Kama ana hiyo neutron power, basi anaweza kutusaidia sana kuondokana na umaskini huu kwa vile ataitumia kuyafanya mataifa tajiri kuja na kuwezekeza hapa kwetu hata kwa hasara.
 
Kuna Kusaga na mwenzie anaitwa Ruge... Anyways issue ya Amina na Zitto naona imeshaanza kuisha radha sasa...
 
Tuendelee tu kukumbushana kuwa hata ukiunganisha makosa mia yatabaki kuwa ni makosa na wala hayawezi kubadilika kuwa ni sawa!
 
mwanasiasa, kama hilo ni kweli kwanini kosa moja linaonekana ni kosa kubwa zaidi!!! na hayo mengine hata kutajwa hayatajwi? tutumie kipimo kile kile...
 
Ndugu wana jf. nimekaa kimya kuhusu hili ila kwa kuwa naona wakina Nchimbi na wenzake wanalivalia njuga ngoja nami nije uwanjani.

Kwanza hapa simtetei yeyote yule kwani sina ushahidi wa upande wowote, Ila napenda kumwambia Nchimbi kuwa akumbuke wakati wa mchakato wa mgombea urais wa ccm kule Dodoma kwenye ofisi kuu ya ccm alimlaza JENIPHER ........ aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu elimu ya siasa na utawala kwenye bench na kumfanya vibaya .......

Ukiendelea nitaziweka picha za usiku ule hapa na kwenye mitandao mingine.

kwani nilikuwepo baada ya sisi wanafunzi wa chuo kikuu kuja kwa ajili ya kumpigia jk kampeni.

Nimeona nije kwenye mstari wa mbele live ili kuweza kuuonyesha uozo huu. Ila napenda kuwaambia kuwa ninayo mengi zaidi ya kusema kwenye hili

Wana JF naomba mnilinde sana ili kutoboa haya yanahitaji kifua kwa kweli .
 
Amina, Zitto ruksa !

2007-05-14
Na Usu-Emma Sindila, Jijini


Waheshimiwa wabunge, Amina Chifupa wa CCM na Zitto Kabwe wa CHADEMA ni ruksa kwao kujivunia uhuru wao binafsi kama katiba inavyosema.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, amesema anawashangaa watu wanaolivalia njuga suala kwamba wabunge hao vijana wana uhusiano wa kimapenzi na kusahau katiba ya nchi inasemaje kuhusiana na uhuru wa mtu binafsi.

`Ninawashangaa hawa watu wanaolivalia njuga suala hili? yawezekana hawajui na hawajawahi kusoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kipengele kinachozungumzia uhuru wa mtu binafsi na maisha yake,` akasema Bw. Tumbo.

Kwa mantiki hiyo, Bw. Tumbo amesema kuwa CHADEMA haiwezi kujiingiza kwenye masuala binafsi ya wabunge hao kwani wana ruksa ya kufanya watakacho ilimradi hakiingilii masuala ya chama.

Akasema mbunge Zitto hawezi kuchukuliwa hatua yoyote na chama chao kwa sababu, CHADEMA haiwezi kushughulikia tuhuma zozote ambazo ni za kizushi.

Amesema hivi sasa, Bw. Zitto mwenyewe hajalifikisha suala hilo mbele ya chama ili liweze kushughulikiwa na hiyo ni sababu nyingine inayowafanya wasione sababu yoyote ya kujadili tuhuma za kizushi mbele ya vikao vyao vya chama au kamati.

`Ni mambo yanayoonekana wazi kuwa ni ya kuzushwa? isitoshe, yanahusiana zaidi na watu binafsi na wala siyo chama. Chama chetu kinazingatia uhuru binafsi wa kila mtu,` akasema Bw. Tumbo.

Mapema wiki iliyopita vyombo vya habari mbalimbali vilinukuliwa vikisema kuwa Mheshimiwa Amina Chifupa amelimwa talaka na mumewe Mohamed Mpakanjia baada ya kubainika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mheshimiwa mwenzie, Bw. Zitto Kabwe wa CHADEMA.

Hata hivyo, ilidaiwa baadaye kuwa huo ni uzushi uliotengenezwa? na wapinzani wa Amina ndani ya CCM ili kumtibulia mipango yake ya kuwania uenyekiti wa umoja wa vijana ndani ya CCM.


SOURCE: Alasiri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom