Mikuki,
Sitegemei kamwe kwamba ulipouliza maswali yako unategemea Admin akujibu kwamba JF ni ya au inaendeshwa kwa niaba au jili ya chama teule. Frankly I'll care less hata kama atasema in the affirmative kuhusu hilo ili mradi hanizuii kutoa mawazo yangu bila ya kipingamizi. Tangia niingie humu JF sijaona mawazo ya mchangiaji yakizuiwa kwa sababu tu ni ya kukitetea chama fulani. Kwa hiyo hilo la JF kuwa na chama halinipi taabu.
Linalonitia wasiwasi mkubwa ni mtindo wa baadhi ya wachangiaji binafsi wanaohusisha mawazo ya wachangiaji wenzao na aidha, uanachama wao wa chama cha siasa, udini wao, ukabila wao n.k. Haya yameongezeka sana humu. Imefikia mahala, hata kabla mtu hajasoma hoja, kwa kuangalia jina tu mtu anaweka msimamo wa kupinga
hoja bila ya kutafakari vizuri yaliyoandikwa. Hali hii inajidhihirisha vizuri na baadhi ya majibu yanavyotolewa kwenye hoja kadhaa.
Hata kwenye mambo ambayo mtu angedhani kuwa ushabiki wa kisiasa ungewekwa pembeni na kuweka mtazamo wa kitaifa zaidi hali hii ipo. Mfano mzuri ni huu wa wanafunzi wa Ukraine. Hawa ni waTanzania; na sidhani kamwe kuwa hawa vijana hali ngumu inayowapata inatokana na wao kuwa wanachama wa CCM, CUF, Chadema, Mtikila or whatever! Lakini, kwa bahati nzuri au mbaya kwao, baadhi yetu humu JF tumelichukulia hili jambo kuwa la kisiasa, kiasi kwamba hata kuchangia tu visenti ili waweze kujikimu na hali hiyo ngumu kunachukuliwa kama kukinufaisha chama cha siasa!
Sikumbuki ni wakati gani Mwanakijiji alipotutangazia humu ukumbini kuhusu uanachama wake kwenye chama kimojawapo cha siasa. Kama yeye ni mwanachama wa Chadema, hilo halimwondolei hata sentila moja ya uTanzania wake. Wengi tumenufaika na kufarijika zaidi na juhudi zake mbalimbali alizokwishazifanya kupata utatuza wa matatizo ya wanafunzi wa Ukraine. Baadhi yetu tumechukulia juhudi hizi kuwa ni kujitafutia sifa na pengine kutafuta njia ya kuiaibisha serikali. Matokeo yake sasa yamekuwa kila mjadala unaojadiliwa hapa Mkjj anakuwa ni mjadiliwa. Kila mtu anayo mapungufu yake, na yeye kwa vyovyote anayo mengi tu; lakini tukubali pia kuwa hoja zake nyingi zimejitokeza kuwa na mchango mkubwa katika mtandao huu wa JF.
So I say, wenye vyama vyao wavitetee wanavyotaka bila ya kutukejeli au kutukana utu wetu. Sisi wengine tuna uhuru wa kutetea au kupinga bila ya kuogopa kupakwa rangi ya chama chochote kile. Tupakeni tu rangi ya UTanzania basi. Kama serikali ya Kikwete inastahiri sifa tutaisifu,na kwa kuanzia ninaanza kuandaa hongera kemkem kwa JK mwenyewe kutokana na hatua ya Taifa Stars leo. Bila ubishi wowote, mafanikio yanatokana na uamzi mahsusi aliouchukua rais wetu. Sasa tunataka iwe hivyo hivyo katika mambo yetu mengine mengi yanayotukabiri kitaifa: uchumi wetu, elimu yetu, rushwa zetu, n.k. Simsifu kwa kuwa ni mtu kutoka pwani, au kwa vile ni mwislamu/mkristu au mpagani. Na sitamsuta akiharibu kwa vile tu anazo sifa hizo.
Sifa zitamiminika kila mafanikio yatakapokuwa yanaonekana, au hata hiyo dhamira nzuri ya utekelezaji tu itakapokuwa inaonekana. Hao wapinzani nao tutawasifia kama watakuwa wanatuonyesha njia mbadala zinazoonekana kuwa na matumaini, na tutawaponda tunapoona hoja zao hazifai.