Kashfa ya makontena TRA tena: Ni ya Silent Ocean

Kashfa ya makontena TRA tena: Ni ya Silent Ocean

GSM/S.O/HSC hawa watu inabidi wapigwe fine ya mabilioni kwa kuhujumu uchumi,wasiache,Wanaishi maisha ya anasa kwa kutolipa kodi,Uncle Magu wapige fine ya mabilioni hao watu,fedha wanazo nyingi tu,fine haitoathiri kampuni.
 
ungejua mkewe alivyowekwa ndani masaa 7,ndio utajua huyu mzee wa 5 hataniwi,mzee wa 2 ndio alienda kupiga goti juu ya hii inshu,mzee wa 4 aligoma kwenda kuongea na mzee 5 baada ya kuona itakuwa noma na kashfa,ila yamemezwa kimya kimya na hakuna alojaribu kuripoti chochote....
Yaonekana unajua kitu Fulani mkuu,wengine umande ulitushinda hesabu za mafumbo hatuwezi,MWAGA MCHELE HUO
 
Nchi hii ufisadi hautaisha awamu hii ni mkubwa zaidi ila kwa sabababu watu wamezibwa midomo mtayasikia baaddhi tu.

ukitokea ule unaomhusu kiongozi wa juu kabisa yes juu kabisa hamtasikia kamwe
 
Pamoja na tuhuma hizi kuwa hazina mashiko kwa kukosa ushahidi wowote,
nichukue nafasi hii kumhakikishia mleta mada kuwa ufisadi upo na utaendelea kuwepo mpaka mwisho,na asikudanganye mtu eti kuna siku ufisadi hapa duniani utaisha....
 
Ukiona wewe binafsi unapenda maisha ya dili, acha kutumia neno "Sisi". Hiyo inaitwa over generalization. Ndiyo tatizo la kukariri kariri kila unachokisikia. Watanzainia wengi ni decent na wanafanya kazi kwa bidii sana kwa ajili ya maisha yao na watoto wao. Wanafanya hivyo katika mazingira magumu kutokana na mifumo yetu ya utawala kushindwa kutatua matatizo ya msingi, yanayoweza kuwarahisishia wananchi wengi kujiletea maendeleo haraka. You don't need a Ph.D to know these simple facts. Jf hapa tunatoa elimu ya uraia bure pia.....Acha kabisa kuwasemea mambo ya kipuuzi watanzania kama kuwaita "wapiga dili".
Mkuu acha ubinafsi, kama wewe umeona mimi kuwasemea wengine nimekosea sawa, Je wewe unayo haki ya kuwasemea wengine, lakini mimi hakuna mahali nilipokosea. Nakuomba wewe binafsi jiondoe na usiwasemehe wengine kama ulivyonikosoa.Useme wewe sio mpiga dili sawa?? Unaniambia kuwa nakariri halafu unarudia kitu hicho hicho, sasa nani anayekariri ni mimi au wewe, Halafu unasema facts unajua facts wewe?!! Ph.D inaingiaje hapa?
 
Hata zinazo kusanywa haziwafikii walengwa. Halmashauri yangu haijapokea zaidi ya 31% ya bajeti yake miezi saba ya bajeti 2016/2017. Si ni sawa na kutokukusanywa.
 
Pamoja na tuhuma hizi kuwa hazina mashiko kwa kukosa ushahidi wowote,
nichukue nafasi hii kumhakikishia mleta mada kuwa ufisadi upo na utaendelea kuwepo mpaka mwisho,na asikudanganye mtu eti kuna siku ufisadi hapa duniani utaisha....
NEVER
 
Lakini Itakapokuwa Tofauti Na Matarajio Yenu, Msije Mkaleta Porojo Nyingine
Porojo zipi? Tusimuwekee na wala tusimchagulie maneno CAG, tumwache afanye kazi yake kwa weledi aliojaaliwa.
 
Huwezi kupambana na ufisadi kama Nchi haiendeshwi kwa Uwazi (Transparency).

Vyombo vya kukusaidia kupambana na ufisadi cha kwanza ni BUNGE halafu kuna vyombo vya Habari.

Bunge la Tanzania lipo kwenye giza totoro. Halina meno tena. Hata Viongozi wa mhimili wa Bunge wameufyata.

Vyombo vya habari vimewekewa sheria mbovu kabisa za kuvibana.

Subiri report ya CAG itakavyo tuumbua.

Exactly..
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi kubaini kashfa ya kontena tisa zenye namba za kulipia kodi TZDL 16-10-25830 zilizoingizwa nchini na Kampuni ya Silent Ocean Ltd ambazo zilinaswa na kitengo cha "Fast Team" cha TRA zikiwa na bidhaa mbalimbali za vipuri vya magari, viatu vya ngozi na nguo za kifahari...

Hivi bado watu wanaendelea na hii michezo?? Hawaoni juhudi za Rais wetu na namna alivyo serious na mapato hasa bandarini?

Ipo kila sababu ya kumuunga mkono Rais wetu katika kuyakabili mambo kama haya.. Waliohusika waadhibiwe tu..maana hakuna namna!



Ndugu Ukiwa Unaandika Tuliza Boli Kwanza, Nimesoma Sijaelewa Ufisadi Huo Ni Wa Namna Gani? Umefanyikaje? Wewe Ndugu Yangu Umetiririka Tu Kama Humu Ndani Wote Tunajua Nini Kinaendelea?

Hapo Kwenye Wekundu Sijakuelewa Kabisa

Slow Down, Digest Info, Then Tiririka Kwa Ufasaha Tafadhali Ndugu Yangu

Ahsante
 
Jamani kunamajipu mengine huwa yamekaa pabaya hayafai kutumbuliwa chakufanya huwa tunayapiga sindano za kukausha tu
 
ungejua mkewe alivyowekwa ndani masaa 7,ndio utajua huyu mzee wa 5 hataniwi,mzee wa 2 ndio alienda kupiga goti juu ya hii inshu,mzee wa 4 aligoma kwenda kuongea na mzee 5 baada ya kuona itakuwa noma na kashfa,ila yamemezwa kimya kimya na hakuna alojaribu kuripoti chochote....
Sa huoni kama wanasaidiana we mtu kapiga goti kaachiwa mbona si wanatukomalia hadi unadhulumika na kontena lenyewe..haya maisha madaraja hayawezi isha
 
Back
Top Bottom