Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Utaisha pale madudu aliyoyasababisha fisadi Lowasa na Genge lake yatakapokuwa cleared, Kumbuka Mgao wa Umeme unatokana na kwamba Tanesco imefilisika kabisa kwa sababu za kulipa madeni ya kampuni hewa iliyoletwa na fisadi Lowasa na Genge lake, hivyo hakuna fedha tena za kuwekeza kwenye Umeme na tunalipa madeni tu sasa hivi na ndiyo maana mtu kama fisadi Lowasa na genge lake walipaswa wawe shot at close range kwa maana kwa matendo yao watu wengi wamekuwa masikini, wamepoteza maisha, wengine wanashindwa kusoma, wawekezaji wanaondoka kwa sababu hatuna umeme, kujibu jibu lako ni kwamba hali hii tutaendela nayo kwa muda mrefu tu ujao na hayo ndiyo madhara ya ambayo fisadi Lowasa na Genge lake wameifanyia nchi hii achilia mbali wizi wa dhahabu zote ambazo Rostam ambaye ni genge la Lowasa wameiba mgodi wote wa Buzwagi wafaidika ni fisadi Lowasa na genge lake na wananchi wa Kahama wanaambulia saratani tu kutokana na vumbi kwa sababu ile ni open pit mining!

Hivyo tutachukuwaa muda mrefu ku-recover!

Wakati hayo unayoeleza yanatokea LICHAMA ALILOKUWA NALO lilichukua hatua gani kuzuia hayo yote yasitokee kumbuka mwenyekiti wake ndo raisi wa JMT.
 
Wakati hayo unayoeleza yanatokea LICHAMA ALILOKUWA NALO lilichukua hatua gani kuzuia hayo yote yasitokee kumbuka mwenyekiti wake ndo raisi wa JMT.

Hatua zimeshachukuliwa na zinaendela kuchukiliwa na ndio maana fisadi Lowasa ameondolewa kwenye Kugombea Uraisi na Tume ya Maadili na Mahakama ya kushughulikia Mafisadi akiwemo yeye fisadi Lowasa na Genge lake inakuja...
 
kazi kweli kweli jamani muda hautoshi kumsafisha Lowasa mmeangukia Pua poleni
 
Hatua zimeshachukuliwa na zinaendela kuchukiliwa na ndio maana fisadi Lowasa ameondolewa kwenye Kugombea Uraisi na Tume ya Maadili na Mahakama ya kushughulikia Mafisadi akiwemo yeye fisadi Lowasa na Genge lake inakuja...
Huu ni ulaghai tu mafisadi CCM wameisha.
 
Lowassa amesingiziwa katika kashfa ya Richmond, ILA CCM MAMEIBA FEDHA NYINGI SANA ZA MALI YA UMMA KUPITIA MIKATABA MIBOVU KAMA EPA,Dowans,Kiwira n.k na bado wanalindana na kuendelea kutudanganya wananchi kwa ahadi za uongo. HATUDANGANYIKI TENA. Hatutamchagua mgombea wa CCM.
 
Hatua zimeshachukuliwa na zinaendela kuchukiliwa na ndio maana fisadi Lowasa ameondolewa kwenye Kugombea Uraisi na Tume ya Maadili na Mahakama ya kushughulikia Mafisadi akiwemo yeye fisadi Lowasa na Genge lake inakuja...

Ulishawahi sikia popote licha ya mbwembwe na kejeli nyingi Ulishaona JK anamwita LOWASA FISADI? Lowasa ni clean.Kama Lowasa ni fisadi wambie Magufuli,Mkapa,Mwinyi,na JK wamwite hadharani kuwa Lowasa ni fisadi
 
Kwani lowassa alishadai kua kikwete ni fisadi,,zaidi ya kusema mamlaka ya juju..waitane basi tujue moja
 
dah!! watu walipiga hela hadi wajukuu wao watakuwa matajiri kweli kuna watu hutumia fursa zao
 
Ni kuwa mjadala wa Richmond ndio unaanza japo mbunge wa Kigoma Mjini ndugu Peter Serukamba alimtaka spika kumpa ufafanuzi kwanza kuwa ni kwanini Waziri mkuu hakupewa nafasi ya kujitetea kwenye kamati husika.

Waziri mkuu kaamua kujitoa kwenye meza na amekuwa mchangiaji wa kwanza kuchangia, nitawaambia kile ambacho yeye amechangia binafsi.

A *****************Mchango wa Waziri Mkuu******************

Ameanza kwa kumpongeza Mwakyembe na kusema amekuwa na mbwembwe nyingi sana .

Anasema hakuridhika na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa na anamponda sana mwakyeme kwa yeye ni mwqanasheria na hakumfanyia Natural Justice, yeye binafsi kwani hawakumhoji hata siku moja.

Analalamika Waziri Mkuu kuwa hakupewa Natural Juctice kwani hakuitwa na anasema kuwa alikuwa tayari kwenda hata kwa miguu kwenye kamati husika za bunge.

Anasema kuwa ameonewa sana na amedhalilishwa sana na kamati na kuwa ametuhumiwa bila hata ya kuulizwa hata jambo moja.

Anasema kuwa yeye ameonewa na anasema kuwa kwenye taarifa yao hakuna hata taarifa moja iliyotoka kwenye ofisi ya waziri mkuu , na anasema kuwa ingekuwa heshima kama angepewa nafasi ya kujitetea.

Analaumu kuwa kama wanaweza kumponda Waziri Mkuu kiasi hicho je?mwananchi wa kawsaida anaweza kutendewa haki?

Waziri mkuu ametangaza kuwa amejiuzulu na amemwandikia barua Rais Kikwete.

Zitto anataka mwongozo wa spika juu ya Waziri Mkuu kujiuzulu na anasema kuwa kama Waziri Mkuu amejiuzulu basi na baraza zima lazima lijiuzulu kwani Rais aliteua baraza kwa kushauriana na Waziri Mkuu.

Spika anakataa kuwa baraza zima haliwezi kujiuzulu , mpaka apate barua ya Rais.

Ni kuwa bunge bado linajikanganya sana na hali inawatisha hata wabunge na kwa sasa spika anajiuliza anawezaje kuliendesha bunge kaomba kupewa ushauri na wabunge .

Kuna hali ngumu sana kwa spika na haswa baada ya Zitto kutaka baraza zima lijiuzulu ili kuwweza kumpa rais muda wa kutangaza baraza jipya la mawaziri .

Mbunge wa CCM masilingi anasema kuwa jambo hilo lipelekwe kwenye kamati ya wabuinge wa kamati ya CCM ili wakajadili sijui kama hapo kuna mwelekeo kwa sasa .

Masilingi anatak bunge liahirishwe ili wakajadili kwenye kamati ya CCM .

Zitto anatoa hoja kuwa bunge liahirishwe kwa muda kwanza ili kuweza kuijadili hoja hiyo hapo baadae ,kamnyima mdee halima nafasi ya kutoa taarifa .

Ni kuwa bunge limeahirishwa hadi saa kumi na moja jioni na wabunge wa CCM wameenda kujipanga sijui watakuja na ajenda ipi na rais bado hajajibu barua ya Lowassa ya kujiuzulu.

Naitafuta barua hapa nikiipata tuu naiweka wakuu kaeni mkao wa kula humu leo.

Hakuna waziri ambaye ameenda kumpa pole isipokuwa Batilda tu, hapa kuna ujumbe mzito sana na umejificha.

Nitaendelea kuwapa yanayojiri hapa

B. Hotuba Kamili ya Mheshimiwa Edward Lowassa

==================
C. Vyombo vya Habari vya Kimataifa

D. Rais wa JMT aridhia maombi ya Waziri Mkuu Kujiuzulu

E ****************** Maoni ya wanaJF *******************

F

G. Naziri Karamagi na Dr. Msabaha nao wajiuzulu

H

Lowassa atueleze kwa ujasiri anavtoijua Richmond kama ambavyo Mwakyembe ameapa jana kumwaga mboga.
 
Last edited by a moderator:
Utangulizi: Lowassa alijiuzulu Uwaziri mkuu wa JMT mwaka 2008 kufuatia kashfa ya Richmond. Mwaka 2010 ulifanyika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, ambapo Mh. Edward Ngoyai Lowassa aligombea ubunge jimbo la Monduli. Team CCM ilipanda jukwaani na kumnadi mgombea ubunge huyo na alishinda.

Swali: Ni kitu gani Team CCM mliwaambia wananchi wa Monduli wakamchagua Lowassa ambacho leo kinakuwa dhambi Team UKAWA ikiwaeleza Watanzania?
 
Hawatajibu badala yake watakutukana. Hawana hoja za kujibu hoja strong kama hii badala yake watatoa povu tu.
 
Utangulizi: Lowassa alijiuzulu Uwaziri mkuu wa JMT mwaka 2008 kufuatia kashfa ya Richmond. Mwaka 2010 ulifanyika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, ambapo Mh. Edward Ngoyai Lowassa aligombea ubunge jimbo la Monduli. Team CCM ilipanda jukwaani na kumnadi mgombea ubunge huyo na alishinda.

Swali: Ni kitu gani Team CCM mliwaambia wananchi wa Monduli wakamchagua Lowassa ambacho leo kinakuwa dhambi Team UKAWA ikiwaeleza Watanzania?

Walikua na shida ya kura ya Raisi.
 
Huu uzi hautafikisha hata comments 200...ingaweje kimsingi ulitakiwa upate mjadala mpana sana...mnajua kwa nini???umewashika pabaya...
 
Wewe muuliza swali huna huruma, walau ungewauliza swali jepesi kwa mfano: Baada ya magufuli kuwakamata wale wavuvi wa asili ya asia na kuwafungulia kesi na hatimaye magufuli akashindwa kesi vibaya na wizara yake ikapigwa faini kubwa waulize je taifa limepata hasara kiasi gani kwa uzembe wake?
 
Back
Top Bottom