Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kwa kifupi utetezi wa Lowassa ni wa kimaslahi zaidi kuliko uhalisia. Binafsi niliacha kazi katika taasisi moja ya umma Tanzania kwa kutokuheshimiwa kwa utaalam wangu nilioutoa ambao ndio msingi wa mkataba wangu. Lowassa alipaswa kuachia ngazi ili kukataa kuitia hasara nchi kama aliona dili ilikuwa ni ulaji/ maslahi binafsi ya bosi wake. Kitendo cha kuridhia na kujiuzulu kwa shinikizo la Kamati ya Mwakyembe, kisha kujitetea baada ya kuenguliwa nafasi ya urais ni unafiki na ubinafsi uliopitiliza. Only fool people ndio wataweza kumuelewa.

Mkuu watanzania waliowengi inaonekana wanamatatizo ya akili,,, ni ngumu sana kufikili hiyo point ila ni rahisi kukubali utetezi dhaifu kabisa wa lowassa,,, kwa mtu mzalendo anaeipenda nchi yake hawezi kuona uozo akafumba mpaka mambo yakaharibika na tume ikaundwa,,, huyu mtu ni mtafuta maslahi tu kama wengine...
 
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa ni mchapakazi,mvumilivu,mwenye ujasiri na hufanya maamuzi magumu pale inapobidi.
Ukweli huu unaweza kuchagizwa na kisa hiki; Wakati huo Mh.Lowassa akiwa Waziri wa Ardhi, Ndugu yangu mmoja aliwahi kuwa Afisa ardhi mkoa mmoja , alitumia madaraka yake vibaya kwa kujimilikisha viwanja na kugawa ardhi kinyume na taratibu katika mkoa huo, Mh.Lowassa alipata taarifa hizo na kumfukuza maramoja.Ndugu yangu huyu anamchukia Lowassa mpaka leo, lakini ukimuuliza ni kweli alitumia madaraka yake vibaya anakiri ni kweli lakini analaumu uamuzi uliokuwa umechukuliwa dhidi yake.

SWALI;
1.Je, ana usahihi wa kumlaumu na kumchukia Mh.Lowassa?
2.Je, ni wangapi wanaomchukia Lowassa sababu tu ya uzembe, uvivu na kulewa madaraka vilivyomo ndani yao?

My take;
Tuache chuki binafsi, tuwe wazalendo na tutangulize maslahi ya taifa mbele.

Mkuu LOWASSA ndio sio mzalendo kwani angekuwa mzalendo kumbe tusingeibiwa richmond huku yeye akiwa waziri mkuu,,, maana alijua mkataba feki yeye akaendelea kuwa waziri mkuu huku akijua tunakuja kupata hasara na yeye kesi itamuhusu,,, kwa nini asiseme kuliokoa taifa na sababu hiyo ingetosha kujiuzulu na kuwaambia watanzania anajiuzuru kwa kuwa kuna dhambi abc na sio kujiuzuru baada ya kukatwa,, je asingekatwa??? si angeendelea kuwa kimya bila ya taifa kujua??? Nimegundua kwa hili JK ndio mzalendo....
 
EL ni dhaifu , ameshindwa kutekeleza wajib wake akiwa kama mtendaji wa serikali [w/mkuu] kwa kumuogopa mkuu wake,
ilipaswa auvunje mkataba wa richmond au angejiuzulu ,

Uko sahihi sana*** mzalendo kumbe ni JK aliyemkata na kumshauri ajiuzuru..
 
Lowasa angekua mhusika asingeweza kutoka ndani ya sisiemu(ccm)coz ccm ndo ingekua imemhifadhi dhidi ya kashfa hiyo ya Richmond
 
kp29072015.jpg Yaliyopita si ndwele yanagangwa yajayo
 
waziri mkuu mzima jambo linakushinda unaenda kuomba ushauri kwa rostam azizi huyu hata ajitee vipi Richmond anayo chu wandishi wanawea mapezi wanashind kmuuliz mawali magumu
 
hamna kitu apo! Lowasa anahusika direct, kwani sahihi ni ya nani? sheria inambana 1 kwa 1.
ni sawa na wewe umuue mtu afu useme mamaako ndo alikwambia uue tena bila ushaidi! nan atahukumiwa?

hujui order and command:what: siku zote ulikuwa hujui mkulu anahusika na upo nchi hii😱 kathibitisha bado unajifanya kihelehele dah😎 chuki imekujaa punguza
 
Muda huu katika kukakiribishwa na kukabidhiwa kadi MH.LOWASSA ndani ya CHADEMA ,ameulizwa swali moja kuwa

Swali: Mh. Edward Lowassa unazungumiaje kuhusu kashfa ya Richmond?

Majibu Lowassa:
Nipende tu kusema mimi kama waziri mkuu kwa kawaida ya sheria huwa ninaletewa mkataba muda wa mwisho kuupitia na kuupitisha huwa sihusiki na kuandaa mikataba,mwenye mamlaka ni waziri husika.

Hivyo baada ya kuletewa mkataba husika wa Richmond niliupitia na kiukweli niliuwekea shaka kwa sababu nilishawahi kuwa waziri wizara ya maji nina uzoefu na kuandaa mikataba, nilishauri mkataba huo uvunjwe lakini waziri wa nishati akawasiliana na "NGAZI YA JUU" na kulazimishwa kuupitisha mkataba huo.

Baada ya kugundulika kuwa mkataba huo ulikuwa na mapungufu mengi, "NILICHUKUA MAAMUZI MAGUMU KWA AJILI YA SERIKALI, na kubeba mzigo wote ndio maana hadi leo wanasema mimi ni FISADI WA RICHMOND, nipende kumaliza kwa kusema kwamba MWENYE USHAHIDI WA RICHMOND AENDE MAHAKAMANI AKANISHTAKI.

mwisho.

Duuuuh. Jibu hili linapaswa kutolewa na mtoto wa miaka 5. Nadhani IQ ya huyu mzee ni ndogo sana. Waziri mkuu na waziri wa nishati ni nani yupo karibu zaidi na NGAZI YA JUU? Ilikuwaje yeye akapokea maelekezo ya waziri wa nishati bila kuthibitisha kwa hiyo ngazi ya juu? This is none sense
 
Tumia akili unapo argue. Kulieweka hadharani jambo kubwa kama hilo linahitaji uwe na platform sahihi kwa wakati sahihi na haswa ukizingatia mwizi mwenyewe ndiye aliyeshikilia mpini. Hata Mwakyembe mwenyewe alipofika mamlaka ya Waziri mkuu, alipochungulia na kukuta kumbe barabara haishii pale ilibidi afunge breki za mbuzi!


Kwa hiyo haya yote Dr.Slaa aliyajua ,ila alikuwa anatupigia kelele na kutujazia screen zetu za TV bila sababu since 2008???
 
ivi unaweza kumsema vibaya rais pindi akiwa madarakani ndio mana hata leo ameshindwa kumsema moja kwa moja amebali kusema mamlaka ya juu ndio uelewe hivyo acha unoko elewa haraka uclete mahaba

Kujiondoa CCM au kustaafu wadhifa wa Uwaziri mkuu hakuhitaji kumsema vibaya JK au raisi. Ni jambo ambalo lingeweza kufanyika bila kusubiri kuumbuliwa na mwakyembe.

CDM muwe na aibu, hakuna anayemzuia Lowassa kuwa CDM na UKAWA ila kumtetea mtu mliyekuwa mnamnanga kwa miaka 8 kisa amepenyeza rupia ni kitu kibaya sana.hii dhambi haitawaacha vivi hivi..., watu waliokufa kwenye maandamano yenu ya kupinga ufisadi damu zao hazitaenda vivi hivi..,karma will certainly strike back.
 
What changed is that ...Kwa sasa Tunaye Lowasa huku CHADEMA
Hata Dr Slaa alitoka CCM baada ya Kukatwa kwa tuhuma zake alizotungiwa na CCM...Its Just timing
This is Politics....Kule Field watu wanamwelewa sana Lowasa


haha.., subirieni muone mmtakachofanywa kwenye sanduku la kura.., maana mnawafanya watanzania mabwege...,
 
Dr Slaa bado tuendelee kukuamini?
tunaendelea kumwamini kwa sababu Lowasa hakupewa nafasi na kamati ya mwakyembe kujitetea, hata kule nec alitaka kubwaga manyanga Mkapa akamzuia, hili linaeleweka, ndio maana walishindwa kumvua gamba.
 
Lowassa: Nilipeleka documents kuwa kampuni ya Richmond haikuwa halali. Hizo documents nilizipeleka kwa mwanasheria mkuu Johnson Mwanyika. Lakini baada ya siku tano nilipoona mwanasheria mkuu hatekelezi niliamua kuitisha kikao kilichoongozwa na katibu mkuu kiongozi pamoja na makatibu wakuu wahusika akiwemo mwanasheria mkuu. Tuliongea mengi ila mwanasheria mkuu akaomba pumziko la masaa mawili. Alitoka nje kuongea na simu na aliporudi ndani akasema kuwa mamlaka ya juu imeagiza kuwa Richmond ni halali na kila kitu kiendelee kama ilivyokuwa. Mimi Lowassa ningeongea tena nini?
Huwezi kupingana na mamlaka iliyokuteua!
 
Asingekatwa tungejuaje?

Kuna watu wamezaliwa na wazazi wa ccm na wameapa kubakia humo humo hata iweje. Nadhani we ni mmoja wapo.
Ila kama we sio ccm basi lazima utakuwa ndugu yao mtoto wa baba mdogo ACT
 
Back
Top Bottom