TeamLowassa
JF-Expert Member
- Nov 30, 2013
- 1,495
- 936
Ikulu haina ubavu wa kumjibu Lowasa maana kufanya hivyo watazidi kuchafua hali ya hewa
Nakubaliana nwe, wakaona isiwe kesi ngoja wao wa'mute' tu!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ikulu haina ubavu wa kumjibu Lowasa maana kufanya hivyo watazidi kuchafua hali ya hewa
Richmond ni dili la mkulu.
Hakika mtu huyu hana hatia!!!!
Tutamfuta machozi ya kusingiziwa October
Hakika wewe ni jinga lao. CCM wanakutumia kama chambio. Na kwa vile kweli hamnazo unajipeleka tu kama poyoyoNyie Team lowassa tumeanza kuwaita
#Teamdodoki
Watajibu nn, kwani wako tayari kushuhudia Balali akifufuka km ilivyokuwa kwa Lazaro wa biblia?
Kwenye vitabu vitakatifu kuna maandiko yanasema mchagulie mtoto jina zuri ....... ....... sasa wewe kujiita jingalao lina maana ya kuakisi namna ulivyo mjinga wao!
Wewe unatumika na lowassa?Hakika wewe ni jinga lao. CCM wanakutumia kama chambio. Na kwa vile kweli hamnazo unajipeleka tu kama poyoyo
Nyie Team lowassa tumeanza kuwaita
#Teamdodoki
Wanajukwaa!
Muda umepita sasa tangu Waziri Mkuu aliejiuzulu Mh Edward Lowassa kujitetea kuhusu kashfa ya richmond.
Lowassa alisema bayana hadharani mbele ya waandishi wa habari na umma kwa ujumla akiwa 'live' ITV, kuwa alipokea maelekezo kutoka 'mamlaka za juu yake' kuwa mkataba wa richmond uendelee. Mamlaka ya juu yake maana yake ni bosi wake ambaye ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh, Dr, Prof Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa kuongea vile, Lowassa alijinasua na kashfa hii ya richmond na kumtupia zigo lote aliekuwa bosi wake. Ikumbukwe katiba inamtaka kutii, kutekeleza na kukamilisha maelekezo ya mamlaka ya juu yake. Ikumbukwe hapo kabla Lowassa hajawahi kujitetea hadharani kuhusu kashfa hii ya richmond!
Tujiulize:
1. Ni kwanini mamlaka ya juu yake hayakanushi hii kauli ya Lowassa? Mbona kurugenzi ya habari inayoongozwa na Ndg Salva Rweyemamu imekuwa ipo 'sharp' kukanusha masuala mbalimbali yanayoelekezwa kwa rais kama taasisi hata kama ukanushaji wake ni wa 'ukakasi'?
2. Kuendelea kumuita Lowassa fisadi ni kumtendea haki?, wakati tayari amesema ukweli na kuwekwa wazi?. Tena akaenda mbali kwa kusema yeyote mwenye ushahidi na apeleke mahakamani!
3. Kama hili la ufisadi kwa Lowassa 'si chezo' ni kwanini tume ya Mwakyembe haikumhoji kipindi kile? Kulikuwa na nini?
Ni ukweli gani na ni kwa kiasi gani mtu anatakiwa kusema ili asiendelee kutuhumiwa?!
Simple conclusion:
Kwa muktadha huu wale wanaondelea kumuita Lowassa fisadi badala ya kumuita Jakaya Kikwete fisadi ni wale waliopofuka kifkra! Ikulu yenyewe imekaa kimya kwa utetezi huu, wewe ndo uhangaike kumuita Lowassa fisadi! Umepofuka kifkra!
Kwa anayejua dhamana ya uongozi Lowassa hajajibu kitu. Kacheza na akili za wadanganyika tu. Eti simu ilipigwa kwa mwanasheria halafu akaja kusema uongozi wa juu umesema mkataba uendelee. Waziri mkuu anaongea utumbo kama huu halafu mnauita utetezi?
Kila nikitafakari sentensi hii naona kwamba Lowassa hafai kabisa kuwa rais. Kiongozi asiyejua mamlaka aliyonayo katika ofisi yake. Anayepokea maelekezo ya simu pasipo kuwapo ushahidi wa maandishi. Hiyo simu ilipigwa kwa mwanasheria, kwa nini maelekezo asipewe yeye moja kwa moja? Je alifanya juhudi gani kuthibitisha Kuwa kweli uongozi wa juu umeagiza hivyo?
Akiwa kiongozi mwenye dhamana na uchungu wa kuwatumikia watanzania, kwa nini hukuchukua jukumu la kujiuzulu nafasi yake ili kuepusha kujihusisha na kulihujumu taifa? Hii ingemjengea heshima kubwa pamoja na kuaminika na watanzania. Badala yake akaamua kutumikia maslahi ya uongozi wa juu. Hebu na atueleze yeye alinufaikaje na dili hilo. Ni wazi kwamba hakuishia kuidhinisha tu, kwa sababu alishaufahamu mchezo mzima.
Lowassa ni kiongozi dhaifu tofauti na baadhi ya watu wanavyomdhania. Hafai hata kidogo kupewa madaraka ya juu kabisa ya nchi
Hakika wewe ni jinga lao. CCM wanakutumia kama chambio. Na kwa vile kweli hamnazo unajipeleka tu kama poyoyo