Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

LOWASA HANA HATIA HATA KIDOGO.

Muda umepita sasa tangu Waziri Mkuu aliejiuzulu Mh Edward Lowassa kujitetea kuhusu kashfa ya richmond.

Lowassa alisema bayana hadharani mbele ya waandishi wa habari na umma kwa ujumla akiwa 'live' ITV, kuwa alipokea maelekezo kutoka 'mamlaka za juu yake' kuwa mkataba wa richmond uendelee.

Mamlaka ya juu yake maana yake ni bosi wake ambaye ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh, Dr, Prof Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa kuongea vile, Lowassa alijinasua na kashfa hii ya richmond na kumtupia zigo lote aliekuwa bosi wake.

Ikumbukwe katiba inamtaka kutii, kutekeleza na kukamilisha maelekezo ya mamlaka ya juu yake. Ikumbukwe hapo kabla Lowassa hajawahi kujitetea hadharani kuhusu kashfa hii ya richmond!

Tujiulize:

1. Ni kwanini mamlaka ya juu yake haikanushi hii kauli ya Lowassa? Mbona kurugenzi ya habari inayoongozwa na Ndg Salva Rweyemamu imekuwa ipo 'sharp' kukanusha masuala mbalimbali yanayoelekezwa kwa rais kama taasisi hata kama ukanushaji wake ni wa 'ukakasi'?

2. Kuendelea kumuita Lowassa fisadi ni kumtendea haki?, wakati tayari amesema ukweli na kuwekwa wazi?. Tena akaenda mbali kwa kusema yeyote mwenye ushahidi na apeleke mahakamani!

3. Kama hili la ufisadi kwa Lowassa 'si chezo' ni kwanini tume ya Mwakyembe haikumhoji kipindi kile? Kulikuwa na nini?

Ni ukweli gani na ni kwa kiasi gani mtu anatakiwa kusema ili asiendelee kutuhumiwa?!

Simple conclusion:

Kwa muktadha huu wale wanaondelea kumuita Lowassa fisadi badala ya kumuita Jakaya Kikwete fisadi ni wale waliopofuka kifkra!

Ikulu yenyewe imekaa kimya kwa utetezi huu, wewe ndo uhangaike kumuita Lowassa fisadi! Umepofuka kifkra!
100% your right
 
Namba 3. Mwakyebe alisema walificha siri ili kuikoa serikali isiporomoke yote. Hiyo siri waliyoificha ndiye muhusika mwenyewe hvyo wakambambikia kesi Lowassa. Unapombambikia kesi mtu humpi nafasi ya kujitetea kwasababu atakushinda kwakuwa wewe unakuwa huna hoja au ushahidi wa kumtia hatiani moja kwa moja. Polisi wanajua hili vizuri ukichukulia mfano wa yule mkenya aliyedaiwa kumtesa dr Ulimboka kule Mabwe pande. Ile ilikuwa mbinu ya kumlinda mhusika kamili ili asiporomoke. Walipoona MWA-NA-HA-LI-SI linaendelea kutoa siri kuhusu mhusika kamili ikabidi walifungie wakidai limeandika habari za kuvitaka vyombo vya dola polisi na wanajeshi kutokutii amri wakati gazeti hilo halikuwahi kuandika habari hizo. Wakati wa kampeni tutayapata yote haya kwa uwazi.

mwanahalisi
 
Kujipa moyo kivipi wakati huo ndo ukweli!

Magamba kama kuna kitu kingine wanategemea sawa ila hii single ya Richmond imechuja.

Kuna TeamLowasa, 4Umovement, M4C,UKAWA wapenzi wa ccm wenye kumkubali Lowasa.Maccm mwaka huu umewaendele vibaya. Mwambieni huyo Mzee ashone suti ya siku ya kuapishwa hii kazi imeisha.
 
Kwa anayejua dhamana ya uongozi Lowassa hajajibu kitu. Kacheza na akili za wadanganyika tu. Eti simu ilipigwa kwa mwanasheria halafu akaja kusema uongozi wa juu umesema mkataba uendelee. Waziri mkuu anaongea utumbo kama huu halafu mnauita utetezi?

Kila nikitafakari sentensi hii naona kwamba Lowassa hafai kabisa kuwa rais. Kiongozi asiyejua mamlaka aliyonayo katika ofisi yake. Anayepokea maelekezo ya simu pasipo kuwapo ushahidi wa maandishi. Hiyo simu ilipigwa kwa mwanasheria, kwa nini maelekezo asipewe yeye moja kwa moja? Je alifanya juhudi gani kuthibitisha Kuwa kweli uongozi wa juu umeagiza hivyo?

Akiwa kiongozi mwenye dhamana na uchungu wa kuwatumikia watanzania, kwa nini hukuchukua jukumu la kujiuzulu nafasi yake ili kuepusha kujihusisha na kulihujumu taifa? Hii ingemjengea heshima kubwa pamoja na kuaminika na watanzania. Badala yake akaamua kutumikia maslahi ya uongozi wa juu. Hebu na atueleze yeye alinufaikaje na dili hilo. Ni wazi kwamba hakuishia kuidhinisha tu, kwa sababu alishaufahamu mchezo mzima.

Lowassa ni kiongozi dhaifu tofauti na baadhi ya watu wanavyomdhania. Hafai hata kidogo kupewa madaraka ya juu kabisa ya nchi

Kweli kabisa mkuu majibu ya Mh.Lowasa hayajitoshelezi.huwezi ukajibu maswali magumu kwa majibu rahisi kama alivyo Fanya. Angejiuzulu kabla ya kutia sahii . Ilionesha kuwa naye alishiriki kwenye hilo deal hata kama JK ndo alikuwa Engineer wa hilo dili. Kwakweli naona hafai . kwanza majibu aliyoyatoa dahhhhh! yaani ndo alijimaliza. Ingawa na JK kama mamlaka ya juu anatakiwa ajibu hizi tuhuma.
 
Wacheni kigugumizi,Muulizenu mbona akulisema hilo toka mwanzo aseme baada ya kukatwa?au kauli ya mfuga mbwa wazimu unamrudia mwenyewe...
 
Watu wenye hekima huwa hawajibizan na wendawazim. lko waz tu kuwa mkataba ule ulikuwa na sahihi ya lowasa na kama kwel aliagizwa na rais alipaswa kujionyesha hiyo document ya maagizo. naagizi hayatolew kwa mdomo. na kama kwa akili yake aliona c sahihi alipaswa kujiuzulu. Ni mwendawazimu tu anaeweza kuamin maneno ya fisad lowasa.
 
kikwete ndio muhusika mkuu wa wizi woote Tanzania na Richmond niyake pia hakuna asiye juwa ndio maana amekuwa kimya
 
Watu wenye hekima huwa hawajibizan na wendawazim. lko waz tu kuwa mkataba ule ulikuwa na sahihi ya lowasa na kama kwel aliagizwa na rais alipaswa kujionyesha hiyo document ya maagizo. naagizi hayatolew kwa mdomo. na kama kwa akili yake aliona c sahihi alipaswa kujiuzulu. Ni mwendawazimu tu anaeweza kuamin maneno ya fisad lowasa.

Kuleni malimao kwa kuwa mwaka huu mmekanyaga mavi mnachechemea wakati sio mwiba
 
Hivi mfanyakazi akiambiwa na bosi wake aachane na jambo fulani. kikinuka huyo mfanyakazi hapaswi kusema hayo? Atakuwaje ameshirikiana na mkuu wake kama huyu zemarcopolo anavyobwabwaja? Bongo zingine utadhani ni usaha badala ya ubongo. Nyooo
 
Ikulu haina ubavu wa kumjibu Lowasa maana kufanya hivyo watazidi kuchafua hali ya hewa

Haya ndio mawazo ya wazee wa makapi. Viraka kila kukicha mmevibandua vya kuna shibuda mnabandika kina msindai. Siasa njaa kama hizi ccm itawale milele.
 
Wanajukwaa!

Muda umepita sasa tangu Waziri Mkuu aliejiuzulu Mh Edward Lowassa kujitetea kuhusu kashfa ya richmond.

Lowassa alisema bayana hadharani mbele ya waandishi wa habari na umma kwa ujumla akiwa 'live' ITV, kuwa alipokea maelekezo kutoka 'mamlaka za juu yake' kuwa mkataba wa richmond uendelee. Mamlaka ya juu yake maana yake ni bosi wake ambaye ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh, Dr, Prof Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa kuongea vile, Lowassa alijinasua na kashfa hii ya richmond na kumtupia zigo lote aliekuwa bosi wake. Ikumbukwe katiba inamtaka kutii, kutekeleza na kukamilisha maelekezo ya mamlaka ya juu yake. Ikumbukwe hapo kabla Lowassa hajawahi kujitetea hadharani kuhusu kashfa hii ya richmond!

Tujiulize:

1. Ni kwanini mamlaka ya juu yake hayakanushi hii kauli ya Lowassa? Mbona kurugenzi ya habari inayoongozwa na Ndg Salva Rweyemamu imekuwa ipo 'sharp' kukanusha masuala mbalimbali yanayoelekezwa kwa rais kama taasisi hata kama ukanushaji wake ni wa 'ukakasi'?

2. Kuendelea kumuita Lowassa fisadi ni kumtendea haki?, wakati tayari amesema ukweli na kuwekwa wazi?. Tena akaenda mbali kwa kusema yeyote mwenye ushahidi na apeleke mahakamani!

3. Kama hili la ufisadi kwa Lowassa 'si chezo' ni kwanini tume ya Mwakyembe haikumhoji kipindi kile? Kulikuwa na nini?

Ni ukweli gani na ni kwa kiasi gani mtu anatakiwa kusema ili asiendelee kutuhumiwa?!

Simple conclusion:
Kwa muktadha huu wale wanaondelea kumuita Lowassa fisadi badala ya kumuita Jakaya Kikwete fisadi ni wale waliopofuka kifkra! Ikulu yenyewe imekaa kimya kwa utetezi huu, wewe ndo uhangaike kumuita Lowassa fisadi! Umepofuka kifkra!

Hui ndio ukweli, JK analijua hilo kwamba zigo la Richmond ni Lake na familia yake, ajue kuna siku ya kujibu
 
Na hizo memo alizokuwa anawapa watu wake wa chini watekeleze zilikuwa za nini teamLowasa a.k.a team dodoki. tena kwa handwriting yake na evidence zote zipo. asicheze na akili za watu, Kwa taarifa yako Mbowe keshavuta $2million na Mtei keshavuta $2.5million toka kwa Lowasa kupitia Bank moja uko Middle East kwa sasa hivi tunatoa hint tu. Hivi kwa akili ndogo tu ukimweka Lowasa na Dr. Slaa kwenye Jukwaa na utendaji nani ni Zaidi, si ni Dr. slaa. Kwanza Lowasa hajui hata kujitetea au kuongea kwenye majukwaa sema pesa yake ndo inaongea tu kwa kuwapa pesa ndogodogo kama nyiwe hili kuwapumbaza watu.

Dr, slaa alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kuliko Lowasa. Pia hatuwezi kurudia uchaguzi Mwaka kesho kwa maana afya yake sio nzuri kabisa. Mwambiye anyanyuwe mkono juu kwa dakika moja uone kama hajapanda ndege kwenda Ujerumani kwa matibabu.

Pia matokeo ya uchaguzi wa October yatakuwa hivi= Magufuri/CCM 76% Lowasa/Ukawa 33%, Zito/ACT 0.6% waliobaki 0.4%

Hivi kulingana na mtandao wa Forbes Lowasa ni tajiri wa ngapi hapa duniani? Maana anasemwa mno kwa pesa yake, watu wanamsimanga utadhani wanamdai.
 
Kwa anayejua dhamana ya uongozi Lowassa hajajibu kitu. Kacheza na akili za wadanganyika tu. Eti simu ilipigwa kwa mwanasheria halafu akaja kusema uongozi wa juu umesema mkataba uendelee. Waziri mkuu anaongea utumbo kama huu halafu mnauita utetezi?

Kila nikitafakari sentensi hii naona kwamba Lowassa hafai kabisa kuwa rais. Kiongozi asiyejua mamlaka aliyonayo katika ofisi yake. Anayepokea maelekezo ya simu pasipo kuwapo ushahidi wa maandishi. Hiyo simu ilipigwa kwa mwanasheria, kwa nini maelekezo asipewe yeye moja kwa moja? Je alifanya juhudi gani kuthibitisha Kuwa kweli uongozi wa juu umeagiza hivyo?

Akiwa kiongozi mwenye dhamana na uchungu wa kuwatumikia watanzania, kwa nini hukuchukua jukumu la kujiuzulu nafasi yake ili kuepusha kujihusisha na kulihujumu taifa? Hii ingemjengea heshima kubwa pamoja na kuaminika na watanzania. Badala yake akaamua kutumikia maslahi ya uongozi wa juu. Hebu na atueleze yeye alinufaikaje na dili hilo. Ni wazi kwamba hakuishia kuidhinisha tu, kwa sababu alishaufahamu mchezo mzima.

Lowassa ni kiongozi dhaifu tofauti na baadhi ya watu wanavyomdhania. Hafai hata kidogo kupewa madaraka ya juu kabisa ya nchi

KIJANA HUJUI SERIKALI INAVYOFANYA KAZI...UNAYAJUA MADOKEZO WEWE...! lowasa kaongea kidogo tu. Boss wako ni beyond you think..!mkurugenzi/au mkuu wa idara kakupa maelekezo fanya moja mbili tatu..acha hiyo..ipo safi, utafanyaje? Kikwete na lowasa walikuwa washikaji..lakin ushkaji unakufa pale mtu anakuwa boss wako.
 
ukimya ni silaha kubwa sana, wengine husema jibu la mjinga ni.....
 
Kwa anayejua dhamana ya uongozi Lowassa hajajibu kitu. Kacheza na akili za wadanganyika tu. Eti simu ilipigwa kwa mwanasheria halafu akaja kusema uongozi wa juu umesema mkataba uendelee. Waziri mkuu anaongea utumbo kama huu halafu mnauita utetezi?

Kila nikitafakari sentensi hii naona kwamba Lowassa hafai kabisa kuwa rais. Kiongozi asiyejua mamlaka aliyonayo katika ofisi yake. Anayepokea maelekezo ya simu pasipo kuwapo ushahidi wa maandishi. Hiyo simu ilipigwa kwa mwanasheria, kwa nini maelekezo asipewe yeye moja kwa moja? Je alifanya juhudi gani kuthibitisha Kuwa kweli uongozi wa juu umeagiza hivyo?

Akiwa kiongozi mwenye dhamana na uchungu wa kuwatumikia watanzania, kwa nini hukuchukua jukumu la kujiuzulu nafasi yake ili kuepusha kujihusisha na kulihujumu taifa? Hii ingemjengea heshima kubwa pamoja na kuaminika na watanzania. Badala yake akaamua kutumikia maslahi ya uongozi wa juu. Hebu na atueleze yeye alinufaikaje na dili hilo. Ni wazi kwamba hakuishia kuidhinisha tu, kwa sababu alishaufahamu mchezo mzima.

Lowassa ni kiongozi dhaifu tofauti na baadhi ya watu wanavyomdhania. Hafai hata kidogo kupewa madaraka ya juu kabisa ya nchi

Unashangaa nini serikalini kupokea maagizo kwa jnjia ya simu au kimemo tu? CCM inafanya hayo
 
Back
Top Bottom