LOWASA HANA HATIA HATA KIDOGO.
Muda umepita sasa tangu Waziri Mkuu aliejiuzulu Mh Edward Lowassa kujitetea kuhusu kashfa ya richmond.
Lowassa alisema bayana hadharani mbele ya waandishi wa habari na umma kwa ujumla akiwa 'live' ITV, kuwa alipokea maelekezo kutoka 'mamlaka za juu yake' kuwa mkataba wa richmond uendelee.
Mamlaka ya juu yake maana yake ni bosi wake ambaye ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh, Dr, Prof Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa kuongea vile, Lowassa alijinasua na kashfa hii ya richmond na kumtupia zigo lote aliekuwa bosi wake.
Ikumbukwe katiba inamtaka kutii, kutekeleza na kukamilisha maelekezo ya mamlaka ya juu yake. Ikumbukwe hapo kabla Lowassa hajawahi kujitetea hadharani kuhusu kashfa hii ya richmond!
Tujiulize:
1. Ni kwanini mamlaka ya juu yake haikanushi hii kauli ya Lowassa? Mbona kurugenzi ya habari inayoongozwa na Ndg Salva Rweyemamu imekuwa ipo 'sharp' kukanusha masuala mbalimbali yanayoelekezwa kwa rais kama taasisi hata kama ukanushaji wake ni wa 'ukakasi'?
2. Kuendelea kumuita Lowassa fisadi ni kumtendea haki?, wakati tayari amesema ukweli na kuwekwa wazi?. Tena akaenda mbali kwa kusema yeyote mwenye ushahidi na apeleke mahakamani!
3. Kama hili la ufisadi kwa Lowassa 'si chezo' ni kwanini tume ya Mwakyembe haikumhoji kipindi kile? Kulikuwa na nini?
Ni ukweli gani na ni kwa kiasi gani mtu anatakiwa kusema ili asiendelee kutuhumiwa?!
Simple conclusion:
Kwa muktadha huu wale wanaondelea kumuita Lowassa fisadi badala ya kumuita Jakaya Kikwete fisadi ni wale waliopofuka kifkra!
Ikulu yenyewe imekaa kimya kwa utetezi huu, wewe ndo uhangaike kumuita Lowassa fisadi! Umepofuka kifkra!